Kwa sababu kiboko Yao ameshakufaKichwa cha habari chajitosheleza, yaani mambo yamelala mno ule usharpness haupo, kujali hakupo. Kitu cha dk 2 kinachukua dk30. Aisee hii ni hatari, Serikali mlala mno....
Siwezi kufanya kazi ya laana kama hiyo mkuu ila nimeandika nn kinatakiwa kifanyike unapoenda kupata huduma kwenye hizi ofisi mbali na hapo utalalamika sana muda muda muda ila ukiongea na watu viziri chap unasaidika hata kama ulikuja wamwisho😂Wewe ni mtumishi wa umma. Najua hatuwezi kumaliza
Jitahidi sana uongee na watu vizuri kuwa mcheshi mbona uchangamfu upo mimi napiga simu tu nahudumiwa kama nipo ofisi husika ila ni kitu unakotengeneza ili usiteseke na sio lazima utoe hela......
Salimia watu uhudumiwe vizuri
Hahahaha....wagonjwa hawaishagi chief...ukicheza na ww utaumwa...kisa umeshinda njaa...wagonjwa hawanaga huruma na mtu au daktari....mtu ukimuhudumia kwa dhamana..akipona anakuona takataka...pesa halipi unabaki kulipa deni kwa mhasibu.. wagonjwa hawajui kama na ww unaweza kuumwa
Usitokwe povu nimeelekeza namna ninavyopata urahisi ninapoongea na watu vizuri sio mtoa huduma kwenye maofisi ila nakwenda sana kwenye ofisi hasa za serikali kama unaona salamu sio lazima basi endelea kupata huduma mbovu wenzako wanafika wanaongea vizuri mambo yanakwenda ww utabaki umevimba na hasira na huna la kumfanya anaekuhudumia.Kwamba salaam ni lazima?
Umeajiriwa kutoa huduma kwa hiyari yako na sidhani Kama makubaliano ya malipo ni salaam kutoka kwa wahudumiwa.
Kama huwezi kufanya kazi mpaka ubembelezwe kwa salaam kheri ukae nyumbani na gozi lako mbembelezane siku iishe, ofisi waachie wenye nia ya kufanya kazi!