Mshangazi mdogomdogo
Member
- Sep 23, 2024
- 64
- 43
Kipindi hiki ambacho wamefunga shule, wamekuwa wanaanza biashara hiyo asubuhi hadi usiku wa saa tatu hadi nne katika soko la jioni maarufu kama Kariakoo, ila kwa siku za shule wanadai wanaenda shule kisha jioni ndio wanaenda kufanyabiashara ila si kweli kwasababu kuna ambao huwa wanaonekana wakati wa masomo.
Watoto wote niliofanikiwa kuongea nao wanasoma Shule ya Msingi Ruvuma na Shule ya Msingi Mbulani, hizi shule zinapatikana katika Kata ya Ruvuma, Manispaa ya Songea.
Walianza wachache na kadri siku zinavyokwenda idadi imekuwa ikiongezeka kwa maana wanaalikana pindi wanapokutana shuleni ndo maana wengi wao ni wa kutoka kata moja.
Asilimia kubwa ya wanaowawezesha Watoto hao kwa mitaji ni Wafanyabiashara hasa Wanawake wauza matunda wa soko kuu na wengine wanawezeshwa walezi wa Watoto hao.
Hawa Wafanyabiashara utoa mtaji kwa mtoto kwa madai ya kumgaia faida itakayopatikana, wakiwa wanafanya hivyo na kushinda nao sokoni mpaka usiku muda wa saa tatu hadi nne na kuwaacha warudi nyumbani kwao wao wenyewe na kukutana tena siku inayofuata.
Endapo mtoto anafanya biashara na mifuko aliyopewa haijaisha basi ukabidhi kwa bosi wake (Mfanyabiashara) na siku ya pili kuichukua na kuendelea na biashara hiyo.
Watoto wanadai kuwa pesa wanazokusanya wanakabidhi kwa wazazi au walezi wao kwa ajili ya kujinunulia mavazi ikiwemo sare za shule na vifaa vya shule.
Wafanyabiashara niliozungumza nao wamekiri kuwapa mitaji Watoto hao ambao wanakutana tu sokoni na hawawajui hata wazazi au walezi wao na mahala wanapoishi.
Pia, kuna wazazi na walezi ambao wao huwatuma Watoto wao kwenda kufanya biashara hiyo na pesa wanakabidhiwa wao.
Hivi ni kweli imeshindikana kuwaondoa Watoto hao katika shughuli hiyo hatarishi? Wananchi na baadhi ya Viongozi tena wale wa Dawati la Jinsia na Ustawi wa Jamii ndio wateja wa mifuko hiyo inayouzwa na watoto, kwa maana moja ama nyingine tunaunga mkono kile wanachokifanya.
Inadaiwa kuna vikao vya ndani vimejadili sana kuhusiana na hili lakini hakuna utekelezaji wowote unaofanyika siku hadi siku watoto wanaongezeka sokoni.
Ushauri wangu Manispaa iweke mikakati ya kuwaondoa ikiwemo kuwakamata na kuwafungulia kesi wale wanaowapa mitaji watoto hao.