Huku mtaani kwa sasa hakuna mwanasiasa maarufu kuliko Makonda

Kwani Watanzania wanataka nini?

Mioyo ya Watanzania walio wengi, wanatamani saana kuona kiongozi mwenye kuwasemea na kuwatatulia matarizo yao

Watanzania si wasemaji sana hata kama wakiwa na lundo la matatizo, sasa inapotokea kuna mtu anaowajua, anawajali, matatizo yao anayachukua yeye na kuwasemea, inatosha kabisa kwao kumfanya ndiye kiongozi wao bora

Tusidanganyane, zaidi ya 80%ya watanzania, ni masikini na wenye hali ya chini mno, watu hao mara nyingi hukosa mtu wa kuwasemea matatizo yao

Inapotokea kama Makonda, kwao inakuwa lulu na haitajalusha makoandokando yake, hayo mtajua nyinyi wasomi na wenye maisha mazuri

Na kwa bamna hiyo, bado Tanzania inahitaji viongozi mfano wa kina Makonda nawenye chembechembe za kina Magufuli
 
Hakika ila kwangu Mimi sio Maarufu.

Kitu kizuri Kwa ccm na Samia ni Makonda kuwafunika Machadema nao wanajaribu kurudi kwenye kiki Kwa maandamano ambayo yanapuuzwa 🤣🤣
 
Makonda the chosen one
 
#makondaforpresident2025
 
Jamaa anakubalika
 
Labda una obsession na Makonda tu kama walivyo watanzania wengi zaidi ya 90% ambao ni wajinga.

Je ni kweli wananchi Wanasikilizwa ? Hilo pekee siyo suluhisho.

Hakuna mtu aliyeyatuliwa shida yake na Makonda mpaka sasa toka aanze ziara zake

Ukiamini katika uliyoyaandika unanithibitishia kuwa mfumo wa utendaji na utoa huduma wa Serikali umekufa.

Barack Obama alipotembelea Ghana Julai 11, 2009 alisema "Africa doesn't need strongmen, it needs strong institutions,”

Kwa kuwa strong men watakufa ila strong institutions zitadumu milele.

Na hiyo ambayo Barack Obama alikuwa anaiponda ndiyo "Magufulism". Nchi inamtegemea mtu mmoja kwa maguvu yake na akili zake, akifa na mfumo umekufa.

Kama unasema unasema Makonda ni mouthpiece ya prez, then the prez has shown weakness. Unawateua watendaji wewe mwenyewe, je unashindwaje kuwawajibisha hadi "mwenezi" ndiyo awafokee. ??
 
Peleka ushuzi wako uko
 
Msanii mazuri
 
Labda una obsession na Makonda tu kama walivyo watanzania wengi zaidi ya 90% ambao ni wajinga.
Ikiwa 90% ni wajinga basi nawe ni miongoni mwa hao wajinga kwa sababu nilichoandika hata hujakielewa sio ajabu imetoa maelezo marefu yasiyohusiana na uzi

Je ni kweli wananchi Wanasikilizwa ? Hilo pekee siyo suluhisho.
Wapi nimesema wananchi wanasikilizwa? Hivi unajua kusoma kwa ufahamu au unasoma kama upo kwenye mashindano ya kusoma imla kwa haraka haraka kama kasuku?
Hakuna mtu aliyeyatuliwa shida yake na Makonda mpaka sasa toka aanze ziara zake
Soma tena uzi alafu uelewe uzi Unazungumzia jambo gani.

Ukiamini katika uliyoyaandika unanithibitishia kuwa mfumo wa utendaji na utoa huduma wa Serikali umekufa.
Hapa sio Kanisani au msikitini kwamba useme ninaamini au siamini. Mimi nimeeleza ninachokiona na kukisikia mtaani. Sio Masuala ya imani kama hadithi za NONDO mla Watu.

Sasa kama unajua nchi inahitaji strong institution Kwa uelewa wako Unafikiri hiyo taasisi yenye nguvu inajengwa na nani kama sio kiongozi mmoja
Kama unasema unasema Makonda ni mouthpiece ya prez, then the prez has shown weakness. Unawateua watendaji wewe mwenyewe, je unashindwaje kuwawajibisha hadi "mwenezi" ndiyo awafokee. ??

Kwa kukurahisishia ni kuwa mada ilikuwa inasema Mpaka sasa Makonda ndiye mwanasiasa maarufu kuliko wote.
 
Kataa wahuni #Polepole !
Ngoja tuone hizi mbio zisijekuwa ni zile za kuishi a ukingoni !
 
Na huo ndio ukweli wenyewe !
JPM alizikonga nyoyo za watu wa hali ya chini hapa Nchini !!
Ndio maana hata anapotokea msanii akaigiza kama alivyokuwa akifanya Mwamba watu inakuwa ni rahisi kumwamini !
Ngoja Tusubiri tuone !!
 

Kumbe ni maarufu, nilidhani ni mwanasiasa Bora. Umaarufu wake umesababisha umeme wa uhakika kupatikana, bei ya sukari imeshuka, treni ya mwendokasi imeanza juzi mwezi wa January. Unaweza kuwa maarufu kwa mambo ya kijinga, wenye akili zetu tunapima ubora na sio kiki.
 
Naunga mkono hoja Bado kuna ubishi kuwa hiki ni chuma? Je, chuma hiki ni chuma kingine ila ni kama kile au chuma hiki ni kile kile kimerejea kivingine?
P
 
Makonda ndiyo habari ya mjini. Ana akili sana Makonda
 
Naona ukiingia YouTube trending kwenye top 20 makonda video zimejaa yeye tu kawapiku Mpaka wasanii.
 
Makonda ni ushahidi tosha huko CCM wananchi wana-miss aina ya uongozi kipindi cha Magufuli. Hawana mtu wa kumlilia shida.

Hao wapinzani wakati CCM inaachana na style ya uongozi badala ya wao kuziba gap kwa faida ya kisiasa ndio kwanza wakipata wasaa kwenye media yule mtu alikuwa hafai. Leo wamebaki kujitekenya na kucheka wenyewe wakijiaminisha wana support yenye nguvu nchini.

Watanzania hawana trust tena na uongozi wa upinzani na Makonda ndio anaenda kuudhofisha kabisa.

Siku Makonda anatangazwa katibu mwenyezi wengine tulishaiona hii move ya kisayansi inalenga nini na si ajabu msingi wake ni use of ‘big data’.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…