Huku wakiwapumbaza watanzania kwa Mpira, nyuma ya pazia wanauza Nchi

Huku wakiwapumbaza watanzania kwa Mpira, nyuma ya pazia wanauza Nchi

Simba na yanga ndio cocaine ya wabongo walio wengi Sasa kila mitaa ya nchi hii ukienda ni midahalo ya simba na Yanga si wazee si vijana ,si asubuhi si mchana nahisi kuna spiritual implications katika haya si bure.
Sasa hivi vipindi vya michezo kujadili simba na yanga ni asubuhi mpaka usiku. Na ipindi vyote vina wasikilizaji wengi. Mambo muhimu kama haya hatapewi airtime.
 
Tatizo ni huyu Mkwere, ni Kiongozi wa hovyo haijawai pata kutokea. Ameipoteza nchi kwa sehemu kubwa na bado anaendelea kuipoteza.

Watu waliondoka mpaka na vyura wa kihansi kipindi cha utawala wake.​
 
Yaaani Maisha yanakwenda kasi sana!!!Hali imekuwa ngumu tunatafuta pesa ya kula tu kwasasa.
 
Nchi imeishauzwa,ilianza kuuzwa na mkapa,natamani tuingie vitani,tutandikwe jwtz yote ife,wamteke rais na ccm wote,wachapwe Shaba!!harsfu tuanze upya.
 
Nimesoma huo mkataba, yaani ndani ya huo mkataba hakuna hata kifungu kinachoeleza namna ya Kutransfer kutoka kwa mwekezaji kuja kwetu baada ya kuoperate kwa miaka, Hii maana yake siyo miaka 100 tu, hawa jamaa wanaweza kuimiliki bandari milele!
 
Ndani ya wiki hizi mbili kuna mambo ya kutisha yanaendelea nchini. Lakini kwa kuwa watawala wamegundua akili za Watanzania ni kufuatilia vitu vyepesi, wameamua kuinvest kwenye mpira wakati huku behind the scene wakiwa busy kuuza nchi na kupalilia ufisadi. Haya ni baadhi ya mambo ya kusikitisha yanayoendelea nchini ndani ya wiki hizi mbili

1. Waziri atoa rushwa ya mitungi 100 kwa kila mbunge
Wakati watu wakiwa busy kufuatilia kama Yanga atatwaa kombe, Waziri mwenye dhamana ya nishati amegawa mitungi 100 ya gesi kwa kila mbunge bure. Dhahiri shahiri hii ni rushwa, tena imetolewa bungeni na tena bila aibu spika ameibariki na kuitetea.

Wakati mwingine unajiuliza spika ana maslahi gani katika hili, utagundua kuwa anamaslahi mara mbili. Mosi, mume wake ni bosi pale EWURA, kwa hiyo spika ana conflict of interest kwa jambo lolote linalohusu EWURA litakaloletwa bungeni. Pili na yeye spika ni mnufaika wa mitungi mia ya bure!
Hii nchi inakwenda wapi?

2. Kuuza bandari
Hii kampuni ya Dubai iitwayo Dubai Ports(DP), imekuwa ikijaribu kutwaa Bandari mbalimbali. Mwaka 2006 ilijaribu kutwaa bandari huko Marekani lakini bunge la Marekani (Congress) lilipiga kura kukataa utwaaji huo.

Hata hivyo DP ilikuwa ikipigiwa chapuo na rais wa Marekani wa wakati huo George Bush. Kutokana na pressure kubwa ililzamika kampuni hiyo iuze share zake kwa kampuni ya Marekani ndo ifanye shughuli hizo.

Leo Samia anataka kutuletea yaleyale ya George Bush.

3. Kuna kila dalili kuna mkono wa CIA katika hili deal
Katika kujaribu kucounter nguvu ya China katika uwekezaji wa infrastructures hasa Africa, USA na washirika wake wanatumia front companies ambayo wamekita mizizi yao ili kutwaa hizi assets.

Hii move nina wasiwasi inaweza kuathiri uwekezaji wa Wachina katika bandari mpya ya bagamoyo. Na ni dhahiri Mmarekani hataki mchina ajenge hiyo bandari. Sasa swala hapa siyo kwamba kwa nini uwekezaji wa China kwenye bandari ni sawa ila wa Dubai ni no!. Jibu ni simple, Dubai wanaenda kufanya kitu rahisi ambacho sisi tukiacha uzembe na uvivu tunaweza kukifanya sisi wenyewe, wakati mchina anaenda kufanya kitu kikubwa!.

Kama tumewahi kukataa mchina asijenge bandari kwa sababu angeioperate kwa miaka takriban 40, Iweje leo tuone eti Dubai ipewe deal la miaka lukuki kwa kitu ambacho kimsingi kipo?

Mkapa aliuza NBC kwa makaburu kwa bei chee akaishia kujuta, Samia sasa anataka kuuza bandari kwa ahadi feki za modernization!.

WEKENI MKATABA WAZI TUUONE!
Sifa ya mtanzania ni kuorodhesha lawama, hana hoja yenye utatuzi hata moja!.

Spika kuolewa na bosi wa EWURA sio hoja yenye mantiki ndani yake, unataka kuniambia walianza uchumba mpaka wakaoana kabla hawajapata hivi vyeo?. Vipi kuhusu Kamala Harris ambaye ni wa pili kwa ukubwa kule Marekani na yeye kwa kushirikiana na mumewe wanaiibia nchi yao?.

Kwa sababu Spika kasoma na ni mwanamke basi asipewe cheo kisa uwepo wa maslahi binafsi?, hoja ya kitoto hii.

Mkataba haupo na haujaandikwa, ni makubaliano ya awali ya namna ya kuja kushirikiana katika siku zijazo.
Mpaka mada inafikia kuwa ni namna ya kuwa na mwekezaji wa kuendesha bandari hii ni aibu yetu ya kitaifa, kwamba hatuna uwezo wa kujiendesha na ni rahisi kwetu kutumiwa na wenye maslahi ya nje kwa faida yao huku tukiambulia pesa ndogo tu.

Waziri kutoa mitungi mia ya gesi naona kama ni maneno ya kuchafuana tu, yenye msingi wa wivu.
 
Back
Top Bottom