Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Wanajamii forum, naomba kuuliza. Hivi mtu huwa anajiskia raha gani kuongea uongo au kuongelea kitu ambacho hakijui ukweli wake? Kwanini kama mtu hajui maana au tafsiri ya kitu asiulize kwa wenye kujua? Au anapata faida gani kuongea uongo??
Dunia hii ukitaka kuwa "siriasi" utaumia, Mungu mwenyewe hayupo serious!
 
Sio Tanga ndio ilifaa kuwa sehemu ya mkoa wa Zanzibar?
Tanga ina jumla ya watu milion mbili (2) hivi , zanzibari ina watu 1.5 milion.
Tanga ina jumla ya 2,045,205 ukubwa wa eneo, zanzibar ina 2,332 ukubwa wa eneo.

Mdogo anamfuata Mkubwa!
 
  • Thanks
Reactions: T11
"Konda nishushie poro langu au wanasema kiporo"😂😂 poro ni mzigo kama vile unga wa kilo 25 au mchele.. akienda dukani kununua mchele wa kilo 25 au unga wanaita poro la sembe au poro la mchele.. for the first time kwenye gari kuna mama alikuwa anashuka akamwambia konda nishushie kiporo changu 😂😂 mi nikajua uporo chakula kilicholala hatari tupu.😅
si poro bali ni polo, kipolo.

kiporo, uporo (chakula kilichopikwa jana)
 
Vikapu Wana ita SUSU unakwenda wapi Wana ita were kana kwenda wapi kijijini wanaita shamba utasikia unafanyikazi shamba gani Kuna mashamba ya BWEJUU.NUNGWI,KIZIMKAZI,MAKUNDUCHI, FUMBA, KITOGANI, ,MATEMWE, PAJE, MAHONDA, KIWENGWA, UBAGO, MICHANVI, hivi ni vijiji vya Zanzibar vilivyopo pembezoni mwa bahari na Kuna mahoteli ya kufa mtu wao kufanya mpanzi wana ita kutiana na wao Gest Hawa endi ni pembezoni mwa bahari kwenye mchanga unaweza fanya harusi ndani ya wiki inavunjika

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
1. Hakuna mzanzibari jina Ali akaita Arii hata siku moja.
2. Maamrisho yote ya dini mwanamke hatakiwi kupaza sauti yake. Ndio maana huwezi kumsemesha mwanamke tu njiani na akapaza sauti yake.
3. Round about inaitwa round about kama ilivyo, maana ya ikipinda ni kile kitendo cha gari kupinda kutoka kwenye round about na ukute baada ya round about kuna kituo.
4. Kuna tofauti baina ya sufuria na dishi na hayo yote yanatumika Zanzibar. Sufuria ni sufuria, ( basin) ndio linaitwa beseni au dishi.
5. Kisima kinaitwa kisima, ila ninyi wa huko bara ndio kwa kutokujua baadhi ya maneno ya kiswahili ndio hamuelewi hata hodhi mnaita kisima. Kisima cha kuvuta, ndio ni kisima cha kuvuta maji kwa kamba. Lipi geni hapo?
6. Pombe inaitwa pombe, labda kama huelewi maana ya moja moto moja baridi tafuta maana, ila ukweli pombe ni pombe acha uongo.
7. Acha uongo, chupi zinaitwa chupi kwa vile huelewi maana ya hafu ndio unapotosha, hafu maana yake ni gaguro muulize hata bibi yako atakujibu.
8. Kwa vile bara ilitawaliwa na Mjerumani ndio maana mmezoea kuita shule kwa vile imetokana na neno la kijerumani Zanzibar wanaita skuli inatokana na neno la Kiingereza School.
9. Ni kweli kabisa chepe koleo wanaita pauro au beleshi ni kiswahili hicho.
10. Hela inaitwa Pesa ni kwa sababu kiswahili kimechukua maneno ya kutoka katika mataifa mbali mbali. Neno Pesa limetokana na neno la Kihindi Paisa. Sasa hata ninyi mnaotumia Hela imetokana na neno la Kijerumani Heller.
Unawaona kama Wazanzibari hawajui kiswahili kumbe wewe ndio hujui Kiswahili.Ukiachana na yote kila sehemu kuna mila, silka, tamaduni, desturi zake, hivyo usitake tamaduni zenu na mila zenu ndio zifuatwe na kila mtu au kila sehemu mnayoingia. Jifunze kuheshimu mila, silka, tamaduni, desturi, za wengine ili na za kwako ziheshimiwe. Na usilolijua jenga mazoea ya kuuliza, kwani kwani kuuliza si ujinga ila ni kutaka kujua.

sina kumbukumbu kama mleta mada amedai wazanzibari hawajui kiswahili.labda uonyeshe.

halafu inaonekana umekasirika hivi?kwanini!!
 
Mgeni akifika Zanzibar, watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafuta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafuta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu, nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
Umepelekwa kufanya nini huko kipndi hiki cha uchaguzi?
 
Dalada za huku niteremshe kwa marehemi .niweke mchina mwisho.nateremka bububu huku gari Aina dyna ndo daladala
8823_Dala-dala-3.jpg
dala-dala-transport-en.jpg


Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23] Ni vituko vitupu

Siku hiyo nilikuwa Forodhani nauliza eti maeneo haya huwa wanapika vyakula kama wali au pilau! Yule dereva wa bodaboda aliyenipakia akaniambia huku sana sana wanapika bites na seafoods hasa mida ya jioni ila ukitaka vyakula kama wali harage (hapo kwenye harage nilicheka) au sembe (ugali wanaita sembe) labda utafute maeneo mengine!

Nikawaza kwani angesema tu wali maharage angekufa? Ukiwa mgeni kama haujawazoea unaweza hisi wanafanya makusudi!
Kwenye harage we ukapindua na kuweka kisimi a.k.a king'amuzi
 
sina kumbukumbu kama mleta mada amedai wazanzibari hawajui kiswahili.labda uonyeshe.

halafu inaonekana umekasirika hivi?kwanini!!
Muda mwengine ficha ujinga mkuu! Mtu anapoponda lugha wanayotumia wengine hiyo inadhihirisha wazi kuwa anawaponda hawajui kiswahili sio lazima mpaka aongee direct!! Au Zanzibar wanaongea kiingereza?
Uzushi haufai!! Nimekasirishwa na uzushi.
 
Muda mwengine ficha ujinga mkuu! Mtu anapoponda maneno wanayotumia wengine hiyo inadhihirisha wazi kuwa anawaponda hawajui kiswahili kiswahili sio lazima mpaka aongee direct!!
Uzushi haufai!! Nimekasirishwa na uzushi.

wewe una mizuka yako tu,wapi ameponda maneno yanyotumika zanzibar!!!

mada nzima mleta mada anasema anashangaa wewe unasema ameponda!!!
 
wewe una mizuka yako tu,wapi ameponda maneno yanyotumika zanzibar!!!

mada nzima mleta mada anasema anashangaa wewe unasema ameponda!!!
Anza mwanzo wa uzi! Kwanini asingekuwa anaulizia maana?! Kitu kama hukijui kuuliza sio ujinga! Kipi cha kushangaza sasa!
 
Back
Top Bottom