1. Hakuna mzanzibari jina Ali akaita Arii hata siku moja.
2. Maamrisho yote ya dini mwanamke hatakiwi kupaza sauti yake. Ndio maana huwezi kumsemesha mwanamke tu njiani na akapaza sauti yake.
3. Round about inaitwa round about kama ilivyo, maana ya ikipinda ni kile kitendo cha gari kupinda kutoka kwenye round about na ukute baada ya round about kuna kituo.
4. Kuna tofauti baina ya sufuria na dishi na hayo yote yanatumika Zanzibar. Sufuria ni sufuria, ( basin) ndio linaitwa beseni au dishi.
5. Kisima kinaitwa kisima, ila ninyi wa huko bara ndio kwa kutokujua baadhi ya maneno ya kiswahili ndio hamuelewi hata hodhi mnaita kisima. Kisima cha kuvuta, ndio ni kisima cha kuvuta maji kwa kamba. Lipi geni hapo?
6. Pombe inaitwa pombe, labda kama huelewi maana ya moja moto moja baridi tafuta maana, ila ukweli pombe ni pombe acha uongo.
7. Acha uongo, chupi zinaitwa chupi kwa vile huelewi maana ya hafu ndio unapotosha, hafu maana yake ni gaguro muulize hata bibi yako atakujibu.
8. Kwa vile bara ilitawaliwa na Mjerumani ndio maana mmezoea kuita shule kwa vile imetokana na neno la kijerumani Zanzibar wanaita skuli inatokana na neno la Kiingereza School.
9. Ni kweli kabisa chepe koleo wanaita pauro au beleshi ni kiswahili hicho.
10. Hela inaitwa Pesa ni kwa sababu kiswahili kimechukua maneno ya kutoka katika mataifa mbali mbali. Neno Pesa limetokana na neno la Kihindi Paisa. Sasa hata ninyi mnaotumia Hela imetokana na neno la Kijerumani Heller.
Unawaona kama Wazanzibari hawajui kiswahili kumbe wewe ndio hujui Kiswahili.Ukiachana na yote kila sehemu kuna mila, silka, tamaduni, desturi zake, hivyo usitake tamaduni zenu na mila zenu ndio zifuatwe na kila mtu au kila sehemu mnayoingia. Jifunze kuheshimu mila, silka, tamaduni, desturi, za wengine ili na za kwako ziheshimiwe. Na usilolijua jenga mazoea ya kuuliza, kwani kwani kuuliza si ujinga ila ni kutaka kujua.