Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Mgeni akifika Zanzibar, watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafuta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafuta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu, nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
Sasa kumbe umeshawaelewa unapataje shida. Komaa nao
 
Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi
N'tie dole [emoji52]daah
 
mara zote wanodai kuvunjika muungano huwa na maslahi yao nje ya wananchi wa zanzibar.

raia wa kawaida ukimwambia muungano uvunjike,anakushangaa.anagalia walivyojaa kkoo,ilala nk kote huko wanafanya biashara zao kama nyumbani.

Hahahahaha haaa, Wazanzibar mbona wapo sehemu nyingi tu ambako hata hawajaungana nao, Similar na Zanzibar wapo watuwa makabila mengi tu nje ya zanzibar na hata nje ya tanzania na watu wanapiga shughuli za bukheir wa surur. Sasa hapa suala la muungano linaingiaje!!!? Mleta mada naona anaongelea zanzibar ya miaka 50 nyima, lakini kwa zanzibar ya sasa hata hao wazanzibar halis unawatafuta
 
Itapendeza sana siku Muungano unavunjika sababu naona mnatulemea sana, Zanzibar ni kaeneo kadogo sana lakini uwakilishi wake hauakisi ukubwa wake geographically, hizo gharama za kuwahudumia ni kodi zetu, fikiria idadi yenu pale bungeni na kwenye taasisi za Muungano tunaenda sambamba wakati watu wa tatu tu wangetosha kukiwakilisha kaeneo kenu.
Mkuu,nafikiri Wazanzibari kelele zao za Kila Siku ni kuojiondoa Katika Mungano

Maalim Seif kila siku yuko juu kisiasa hapa Zanzibar Kwa Sera zake za kuitoa Zanzibar Katika huu Mungano,ambao anauita batili,na Watanganyika ni Wakoloni Weusi..

Mkuu,nyinyi ndio mnaielemea Zanzibar,Mpeni Maalim Ushindi,achieni Zanzibar ijiendeleze wenyewe..

Mkifanya hivyo ndio utajua Zanzibar nini na Wazanzibari ni Nani..

Zanzibar iliyokuwa Empire hivi sasa imekuwa omba omba kutokana na kushirikiana na kuungana na Waafrika wasioweza kujitawala..
 
Hivi wanaongea kikabila hao?
Kiswahili kimeanzia Zanzibar,hata hichi ulichokiandika Kama sio Zanzibar usingeliandika

Nyerere alilazimisha Watanganyika lazima wajivunze Kiswahili baada ya kuipatia Tanganyika Uhuru

Zanzibar hakuna makabila, Wazanzibari halisi wamechanganyika damu na Warabu,Wahindi,Wasomali,Waafrika nk..

Lugha moja Tu Kiswahili..
 
Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi
Douta[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
mara zote wanodai kuvunjika muungano huwa na maslahi yao nje ya wananchi wa zanzibar.

raia wa kawaida ukimwambia muungano uvunjike,anakushangaa.anagalia walivyojaa kkoo,ilala nk kote huko wanafanya biashara zao kama nyumbani.
Hamna Mzanzibari anaeupenda Mungano,Kama utamsikia Mzanzibari anaushangilia Mungano basi mgeni huyo..

Wafanyabiashara wengi wa Kariakoo ni Wazanzibari kutoka kisiwa cha Pemba

Wapemba ndio wanaongoza kuupinga huu Mungano
 
Nilimsikia mtu akisema hawana makabila ila pia nilisikia history kwamba wote hao wametokea bara haswa Mtwara na Lindi lakini Ukiwasikia lugha wanayo ongea huko vijijini sio standard swahili kilichopo kwenye dictionary

Nipo interested kuwajua zaidi.
Wazanzibari ni mchanganyiko wa Watu kutoka sehemu tafauti za Afrika nå Dunia..

Kila Kabila au kikundi fulani cha Watu kina historia yake ya vipi kimefika Zanzibar

Makabila ya kando kando ya Bahari ya Hindi ndio inasemekana kuwa ni watu wa mwanzo kuhamia Zanzibar

Wazaramo,Wadigo,Wasegeju haya ni makabila yaliyokuwa na utamaduni wa kuvua Kwa kuondoka sehemu zao za asili na kwenda sehemu nyengine na kupiga kambi(dago) kwa muda mrefu

Kabila la Kimanyema hawa waliletwa Kama Watumwa na Mwarabu

Kabila la kinyamwezi hawa walikuwa walinzi wa Sultani,kwahiyo hawa waliletwa nå Mwarabu..

Wahindi waliletwa na Sultan, Kama vibarua na ufundi mwengine,Kama Vile kujenga Nyumba,usaramala nk

Sultan aliletwa na Wazanzibari wa mwanzo waliohamia Katika visiwa hivi viwili ili aje awalinde na Mreno..

Wajemi(Wairani) Hawa walifika mwanzo Zanzibar kuliko Mwarabu,baada ya hawa kuondolewa na Mreno, ndio Wazanzibari wakamwita Mwarabu..

Zanzibar imeshawahi kuwa Empire kuna Empire nne Tu zinazojulikana duniania,Roman Empire,Othman Empire,Zanzibar Empire na British Empire

1964 Wakati Karume na Nyerere wanaiunganisha Zanzibar na Tanganyika kuwa Tanzania, Zanzibar ilikuwa na watu Laki tatu tu 300,000

Dini ndio kilikuwa kichochezi kikubwa Kwa Wazanzibari kumwita Mwarabu awalinde na Mreno

Dini ndio kichochezi kikubwa Kwa kupinduliwa Sultan 1964

Dini ndizo kichochezi kikubwa Kwa Zanzibar kulazimishwa kuungana na Tanganyika

Dini ndio kichochezi kikubwa Kwa Tanganyika kuing'ang'ania Zanzibar..

Dini ndio kichochezi kikubwa kuwekwa ndani na kusahauliwa kwa Masheikh wa Uamsho

Dini ndio itayokuwa kichocheo kikubwa kuvunjika kwa huu Mungano

Mark my word,save the day and today's date,one day you'll remember this..
 
Hamna Mzanzibari anaeupenda Mungano,Kama utamsikia Mzanzibari anaushangilia Mungano basi mgeni huyo..

Wafanyabiashara wengi wa Kariakoo ni Wazanzibari kutoka kisiwa cha Pemba

Wapemba ndio wanaongoza kuupinga huu Mungano

mzanzibar anayeponda muungano ni maamuma anayesubiria kuelekezwa na wachumia tumbo,hakuna mzanzibar timamu anaukataa muungano.

kwanza wao wanapata zaidi kuliko wabara amabo wanazushiwa kuwakandamiza.

zanzibari ina wajinga wawili watatu wanalilia ijitawale ili waishi kwa kutegemea ufadhiri wa nchi za kiarabu ziingie mifukoni kwao.ujinga kabisa.
 
Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi

hahaha[emoji23] amiiii
 
kuna mmama fulani wa kizanzibari alikuja home akawa anasema “bwana ...kafiliwa mwanae” nilistuka mpaka badae nilipoambiwa anamaanisha “bwana...kafiwa mwanae”
 
mzanzibar anayeponda muungano ni maamuma anayesubiria kuelekezwa na wachumia tumbo,hakuna mzanzibar timamu anaukataa muungano.

kwanza wao wanapata zaidi kuliko wabara amabo wanazushiwa kuwakandamiza.

zanzibari ina wajinga wawili watatu wanalilia ijitawale ili waishi kwa kutegemea ufadhiri wa nchi za kiarabu ziingie mifukoni kwao.ujinga kabisa.
Ni kikundi cha Wazanzibari wanaoitwa CCM ndio wanaofagilia Mungano..

Kuna maslahi makubwa Sana Kwa hichi kikundi cha Wana CCM wa Zanzibar,Tanganyika imewafadhili sana hawa watu,..

Mzanzibari wa kweli hawezi kuufagilia Mungano,hakuna anaekubali nchi yake iwe Mkoa..

Mamlaka kamili ndio ndoto ya Mzanzibari
 
Hiyo sio standard swahili, sababu hata mengi ya maneno yao hayapo kwenye dictionary, halafu nani kasema zanzibar ndio yenye mandate ya kuclaim lugha ya kiswahili? Yapo maneno kibao toka kwenye lugha zetu za makabila zipo kwenye kiswahili.
Tafuta maana ya Swahili kwanza, Zanzibar hawaclaim kuwa ni wamiliki wa kiswahili bali ni lugha iliyokuwa ikitumika katika kufanya biashara maeneo ya mwambao na imechanganya misamiati kutoka katika lugha mbalimbali za kibantu na lugha za mataifa mengine pia, ikiwemo kireno, kifarsi, kihindi, kiarabu. Kama katika kusoma kwako uliwahi kukutana na kujadili mada za kiswahili ikiwemo:
1. Kiswahili ni Kibantu
2. Kiswahili ni Kiarabu
3. Kiswahili ni Pijini/Krioli zilizokomaa

Basi utakuwa umeelewa ninachomaanisha.
 
Kwani we nani mpaka tafsiri yako tuiamini yake tuikatae? Kuna kipi cha tofauti labda hapo? Sababu naona wote ni wanaJF tu hamna cha ziada, yeye pia anauwezo wa kusema wewe ndio mpotoshaji na tikamuamini.
Wote ni wanaJF hakuna cha ziada lakini uongo au kupotosha hakusaidii, mimi ni mzaliwa wa huko na bahati nzuri naelewa jinsi ilivyokuwa/jina lilivyotokea, sasa huwa sikubali pale mtu anapotoa/kuongelea kitu isivyo sahihi.
 
Hahahaha we jamaa akili zako timamu kweli?

Hoja yako ni ipi hasa kwa kupitia hiki ulichoweka? [emoji16][emoji16][emoji16]

This is too shallow to be serious.
Ni vyema ungemuachia niliemquote, naaamini tumeelewana na anajua nilichomaanisha.
 
mzanzibar anayeponda muungano ni maamuma anayesubiria kuelekezwa na wachumia tumbo,hakuna mzanzibar timamu anaukataa muungano.

kwanza wao wanapata zaidi kuliko wabara amabo wanazushiwa kuwakandamiza.

zanzibari ina wajinga wawili watatu wanalilia ijitawale ili waishi kwa kutegemea ufadhiri wa nchi za kiarabu ziingie mifukoni kwao.ujinga kabisa.
Sema kweli!
 
Zuchu alivyoimba Ukipenda Unibimbe Unikumbatie, nikauliza unibimbe ndo nini? Nikaambiwa niwaulize wazenji
Kubimba = kubembeleza
Mfano:
Mtoto mchanga akiwa analia, kile kitendo cha kumnyamazisha au kumbembeleza ili apate usingizi kwa njia ya kumpiga piga sio kwa nguvu tena polepole.
Au
Mtoto mchanga /mtoto mdogo mwenye miezi kadhaa baada ya kumuogesha kile kitendo cha kupitisha mikono yako makwapani kwake, kumrusha rusha na kumpiga piga sio kwa nguvu tena polepole ukiwa umemsimamisha.
 
Mkuu,nafikiri Wazanzibari kelele zao za Kila Siku ni kuojiondoa Katika Mungano

Maalim Seif kila siku yuko juu kisiasa hapa Zanzibar Kwa Sera zake za kuitoa Zanzibar Katika huu Mungano,ambao anauita batili,na Watanganyika ni Wakoloni Weusi..

Mkuu,nyinyi ndio mnaielemea Zanzibar,Mpeni Maalim Ushindi,achieni Zanzibar ijiendeleze wenyewe..

Mkifanya hivyo ndio utajua Zanzibar nini na Wazanzibari ni Nani..

Zanzibar iliyokuwa Empire hivi sasa imekuwa omba omba kutokana na kushirikiana na kuungana na Waafrika wasioweza kujitawala..
Tanganyika inawashikilia kivipi?

Kipi kutoka zanzibar kinatunufaisha sisi?

Mlishawahi kuwa na uchumi upi mkubwa toka dunia imekuwepo ambao saivi umeanguka sababu ya Muungano?

Kwani zanzibar hamna bunge lenu na serikali kamili kushindwa kuvunja Muungano?

Maalim mwenyewe haishi Dar?

Sio Maalim anasema ataboresha Muungano?
 
Back
Top Bottom