Nilimsikia mtu akisema hawana makabila ila pia nilisikia history kwamba wote hao wametokea bara haswa Mtwara na Lindi lakini Ukiwasikia lugha wanayo ongea huko vijijini sio standard swahili kilichopo kwenye dictionary
Nipo interested kuwajua zaidi.
Wazanzibari ni mchanganyiko wa Watu kutoka sehemu tafauti za Afrika nå Dunia..
Kila Kabila au kikundi fulani cha Watu kina historia yake ya vipi kimefika Zanzibar
Makabila ya kando kando ya Bahari ya Hindi ndio inasemekana kuwa ni watu wa mwanzo kuhamia Zanzibar
Wazaramo,Wadigo,Wasegeju haya ni makabila yaliyokuwa na utamaduni wa kuvua Kwa kuondoka sehemu zao za asili na kwenda sehemu nyengine na kupiga kambi(dago) kwa muda mrefu
Kabila la Kimanyema hawa waliletwa Kama Watumwa na Mwarabu
Kabila la kinyamwezi hawa walikuwa walinzi wa Sultani,kwahiyo hawa waliletwa nå Mwarabu..
Wahindi waliletwa na Sultan, Kama vibarua na ufundi mwengine,Kama Vile kujenga Nyumba,usaramala nk
Sultan aliletwa na Wazanzibari wa mwanzo waliohamia Katika visiwa hivi viwili ili aje awalinde na Mreno..
Wajemi(Wairani) Hawa walifika mwanzo Zanzibar kuliko Mwarabu,baada ya hawa kuondolewa na Mreno, ndio Wazanzibari wakamwita Mwarabu..
Zanzibar imeshawahi kuwa Empire kuna Empire nne Tu zinazojulikana duniania,Roman Empire,Othman Empire,Zanzibar Empire na British Empire
1964 Wakati Karume na Nyerere wanaiunganisha Zanzibar na Tanganyika kuwa Tanzania, Zanzibar ilikuwa na watu Laki tatu tu 300,000
Dini ndio kilikuwa kichochezi kikubwa Kwa Wazanzibari kumwita Mwarabu awalinde na Mreno
Dini ndio kichochezi kikubwa Kwa kupinduliwa Sultan 1964
Dini ndizo kichochezi kikubwa Kwa Zanzibar kulazimishwa kuungana na Tanganyika
Dini ndio kichochezi kikubwa Kwa Tanganyika kuing'ang'ania Zanzibar..
Dini ndio kichochezi kikubwa kuwekwa ndani na kusahauliwa kwa Masheikh wa Uamsho
Dini ndio itayokuwa kichocheo kikubwa kuvunjika kwa huu Mungano
Mark my word,save the day and today's date,one day you'll remember this..