Hakuna siku hata moja giza liliwahi kuishinda nuru....
Kama watu wanahitaji kujifunza hata kwenye historia wanaweza kuwa binadamu bora kabisa kwenye maisha yao na maisha ya wengine na kamwe hawataweza kusahaulika....
Siyo jambo dogo hata mara moja unakuta mtu alishaondoka duniani miaka mingi lakini anashindwa kusahaulika na binadamu wenzake alioishi nao hapa duniani kwasababu yoyote ile,pia siyo jambo dogo kwa binadamu kuweza kujulikana na wanadamu wengi duniani....
Haya maisha siyo jambo la maana kiasi hicho hadi uanze kusababisha mazingira magumu kwa binadamu wengine kuishi hapa duniani.Ishi maisha yako kwa nidhamu maana hujawahi hata siku moja na hata hukuwaza kupewa maisha haya unayoishi leo,umejikuta tu unaishi....
Tuishi maisha ya amani sote hapa duniani na yenye upendo wa hali ya juu maana iko siko siku tutamanani leo hii ijirudie lakini haitawezekana.....