Kwa kuwa yeye ni muislam tena muumini,
shehe wetu, kipenzi chetu, ndugu yetu, kiongozi wetu,mahakama itamfunga tu, angekuwa ni mkristo kama lwakatare ama askofu angeshaachiwa huru kitambo.
waislamu waumini tunaishi kama watumwa ndani ya nchi hii.
wakristo wakiwa kama ndio wakoloni wetu.
INSHAALLAH ALLAH amfanyie wepesi na ndio iwe sababu ya kupata pepo.
aamin yaa rabi takabal.
Ndugu usiseme wakristo ni wakoloni wa waislamu, hapo utakuwa unakosea, kutumia makandamizo yaliyotokea kwa baadhi ya waislamu isiwe ni chanzo cha fikra yako, kufanya hivyo ni chanzo kingine cha kutofikia muafaka wa maswala kereketwa kwa waislamu (au baadhi ya waislamu)
Utakubaliana nami kuwa kuna baadhi waislamu wanaoishi maisha mema (yasiyo na bughudha) kama vile ilivyo kwa baadhi ya wakristo au baadhi ya watu kutoka tabaka jingine.
Hivi karibuni nimekuwa mfuatiliaji wa masuala ya dini, haswa kusikiliza upande wa waislamu (malalamiko ya video kutoka kwa baadhi ya masheikh) maana huu ni wajibu wa kila raia mwema. Mimi nawapenda waislamu sawa na navyowapenda wakristo wenzangu, Tanzania ni yetu sote bila kujali dini, itikadi, kabila, ukanda, jinsia na tabaka lolote lile, katika hayo masikilizo nimekubali kuwa kuna baadhi ya waislamu walinyanyaswa kutokana na dini yao na hii ni uvunjifu wa katiba (naomba nikiri sijasikiza upande wa pili). Serikali inahitaji kutolea majibu (tafadhali si majibu mepesi)
Utakuabliana nami kuwa suala la Sheikh Ponda ni la kihistoria, na lahitaji hekima katika kulitatua ambayo naamini litawezekana nje ya mahakama. Sababu sheria haingalii kama Ponda anawakilisha watu ambao wanahisia za uonevu bali inaangilia vifungu vinazungumza nini kuhusu suala linalomkabili. Rais ameshakutana na upande wa wakristo, upande wa waislamu utakapofika moja ya agenda iwe suala la Sheikh Ponda hapa ndo mwanzo wa kuanza kulizungumza nje ya mahakama, wawakilishi wa waislamu wasiwe BAKWATA tu bali wale wanaolalamika napenda na Sheikh Ilunga awe mmojawapo
Hitimisho waislamu wa Tanzania waendeleze mapenzi kwa nchi yao hivyo hivyo kwa tabaka lolote lile, tukitumia hekima tutapata majawabu sahihi, kuliko jazba, chuki, na kuendekeza udini
Wenu mpenzi wa nchi ya Tanzania