Hukumu Kesi ya Ponda, ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje

Status
Not open for further replies.
"kifungo cha nje" maana yake nini? maana inawezekana wa-Tanzania wengi wamefungwa vifungo vya nje...!
 
Tunamshukuru mungu Amejibu duA zeto ponda amepewa kifungo cha nje Mwaka mmoja Ndio tunatoka kisutu
 
Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam,imemfunga kifungo cha nje cha mwaka mmoja katibu wa Jumuiya na Taasisi za KiislamTanzania Shekhe Ponda Issa Ponda,huku washtakiwa wengine wote 49 wakiachiwa huru
source ITV

Duh! Nchi hai ishi vituko hii! Halafu eti viongozi wamejizatiti kulinda amani ya nchi hii. LA KUVUNDA HALINA UBANI.
 
Lema Kesi ya Uchochezi alipewa dhamana,mbona Ponda hapewi kesi hiyo hiyo?Huu ni uonevu na double standard
Inategemea na uchochezi wa aina gani na maneno ya mchochezi yalimtoka wakati gani

Mimi smfagilii hata kidogo bwana misifa Lema lakini maneno aliyotoa ya kuropoka ukiangalia na timing ya tukio anakuwa na defence fulani kwa sababu hakuna nia ovu.

Ponda alipanga huo uchochezi na alifanya sio mara moja bali alirudia mara nyingi na anafahamika kwa uchochezi.

Unaweza kuwa umeua lakini mahakama ikagundua kuwa uliua baada ya kuwa provocked / ulichokozwa hapo kesi yako itageuzwa na kuwa manslaughter na unaweza achiwa huru lakini ukiwa umetoka nyumbani kwako maili mia na panga mkononi, ukazunguka siku nzima unamtafuta mtu umuue na ukafanikiwa kumuua basi kesi yako ni mauaji kwa sababu tayari ulikuwa na nia OVU na tendo dhahir linajionyesha. Kwa sababu kama ni hasira hiyo safari ya mail mia na kuzunguka siku nzima lazima ungeingiwa na woga wa kutenda hilo kosa.

Misifa aliropoka mara tu baada ya tukio jambo ambalo kimahakama anakuwa anasamehewa kwa sababu kila mtu pale alikuwa na hasira na jambo lililotokea . Mimi nilimhukumu kama kiongozi kwa sababu kiongozi unatakiwa uwe na gavana kwenye mdomo sio kuropoka tu
 
Breaking News:Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam,imemfunga kifungo cha nje cha mwaka mmoja katibu wa Jumuiya na Taasisi za KiislamTanzania Shekhe Ponda Issa Ponda,huku washtakiwa wengine wote 49 wakiachiwa huru
 
Inategemea na uchochezi wa aina gani na maneno ya mchochezi yalimtoka wakati gani



Ponda alipanga huo uchochezi na alifanya sio mara moja bali alirudia mara nyingi na anafahamika kwa uchochezi.
Kumbe Sheikh Ponda alisimamishwa Mahakamani kwa kesi ya UCHOCHEZI?!...mimi nilifikiri ni gogoro la "uvamizi" wa kiwanja!.

Magonjwa mengine bhana!
 
Ponda anashtakiwa kwa sababu anapingana na vibaraka wa CCM{BAKWATA} Ambao ndio kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya waislamu wa Tanzania.. BAKWATA inashirikiana na CCM kumpoteza Ponda ili waendelee kuhujumu mali za waislamu.

Nicas Mtei,mkuu sikutaka kuchangia lwenye uzi huu.lakini nimelazimika kuchangia kwa kuwa umesema ukweli ambao ndio unawatesa waislamu,ni ukweli usiopingika kwamba BAKWATA wamekuwa ni vibaraka wa maccm kwa miaka mingi sasa,huku wakiendelea kukandamiza maendeleo ya waislamu na kuwadidimiza katika maendelo ya kiroho na kielimu.Tatizo kubwa ni hao vibaraka wanaojipendekeza sana kwa magamba kila kukicha huku wakilindwa na usalama wa taifa ili waendelee kuwanyonya waislamu wenzao,mifano iko mingi na madhambi yao yako mengi,angalia nyumba za wakfu hapo kariakoo zilivyotafunwa.
Shekhe Ponda ni shujaa kwa kutetea maslahi ya waislamu wote.
 
BAKWATA na CCM dhambi mnayoifanya leo kwa mzee wa watu Shehk Ponda hakika zipo siku zinakuja mtajuta,
Kesi ya ponda si uchochezi wa kidini bali harakatiza ponda ni dhidi ya mfumo dhalimu wa BAKWATA ambao umewekwa pale kwa maslahi ya viongozi wachache wa CCM.

DONT GIVE UP SHEHK PONDA KWANI HAKI YA MTU HAIPOTEI HATA SIKU MOJA.
 
Mimi naona tuvute subira tusubiri maamuzi ya mahakama!


"UKIONA UNASHINDA KILA WAKATI, KITU PEKEE ULICHOBAKISHA NI KUSHINDWA, NA KINYUME CHAKE NI KWELI." na LUCAS, 2013
 
Kifungo cha nje? wacha utani, huyu ni mmojawapo ya wachochezi wakuu wa udini kwa kisingizio anatetea haki za waislamu nchini. Ingefaa aondolewe kwenye circulation kwa muda mrefu ili waislam wenye dhamana ya kuongoza wenzao wafanye kazi yao kwa amani na sheria.
 
Mkuu mimik ni muislam ilanimependa na kukiunga mkono hichi ulicho kiandika. Kwamiaka mingi waislam tumekua tukimtafuta mchawi wetu ninani lakini hivi sasa mchawi kajidhihirisha wazi, hii nibaada yakuamua kuja kuwanga mchana kweupee! Namchawi mwenyewe sie mwengine bali ni BAKWATA. Tatizo linakuja ninjia gani tutumie katika kuikataa Bakwata? Sababu Bakwata imesimikwa na watawala ktk kuendeleza dhulma zidi yetu waislam na viongozi wote waliopale ni usalama wa taifa. Ukitaka kulijua hilo jiulize ni jambo gani ambalo limewahi kubishaniwa baina ya waislam na serkali alafu Bakwata wakawa upande wa waislam? Kwanini kelele zote zinazo pigwa na waislam dhidi ya Baraza hili serkali imekua ikizipuuza? Hapo utagundua kuna maslahi ambayo serkali inayapata kutoka Bakwata.
 
Last edited by a moderator:
"Kama kichaa, na ukichaa wake ameweza kwenda ulaya na kufanya biashara na wateja wakamfuata, Basi wateja nao ni misukule"
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…