John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Ukweli mchungu Sana ni kwamba hao vijana (siyo watoto) baadhi yao walifanya uhalifu mbaya sana kupita kiasi, hivyo wanastahili kupata adhabu kali ili iwe fundisho kwao na kwa Watu wengine katika Jamii. Isipokuwa Hukumu hiyo ya kifo imetolewa kiholela kwa Vijana hao, taratibu zote kabisa za kisheria hazikufuatwa katika kuwatia hatiani. Hivyo,wapo baadhi ya vijana wameonewa, hakustahili kuhukumiwa adhabu ya kifo, ila wapo baadhi ya vijana hao kweli kabisa wanastahili kupata adhabu kali ya kuuawa kutokana na makosa yao waliyotenda.Duniani kote watoto wanalindwa why sababu they're vulnerable and naive, they're controlled by external forces, kama walikuwa wakora wao kama taifa na lina watu wazima wengi kuliko watoto, watoto hao ni zao la watu wazima ovyo. Tegemea huyo kiongozi kulipa huo udharimu wa kumwaga hiyo damu kama sio leo basi ni kesho.
Kutokana na kuwepo kwa mkanganyiko huu mkubwa sana katika mchakato mzima wa kuwatia hatiani, na kutokana na sababu ya umri wao kuwa bado vijana wadogo(wengi wao), Mimi binafsi naona kama adhabu nzuri zaidi kwao ni kuwafunga vifungo vya muda mrefu gerezani badala ya kuwanyonga. Wabadilishiwe adhabu na kufungwa gerezani kwa mfano wafungwe miaka hata kumi, hii itakuwa fundisho tosha kabisa kwao.