Humphrey Polepole aelezea sababu za Kibeberu ya nchi moja kufunga ubalozi

Humphrey Polepole aelezea sababu za Kibeberu ya nchi moja kufunga ubalozi

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
938
Reaction score
1,540
Pole pole ameelezea jinsi mabeberu wanavyojaribu kutudhoofisha lakini ameweka wazi sababu za nchi moja kufunga ubalozi na kusema ni Mambo ya KIUCHUMI kwani baada ya serikali hiyo kubanwa kupata maslai wameamua kuondoka, msikilize hapa akiongelea uzalendo wa Hali ya juu

 
Ni maslahi gani ambayo Denmark (walioisaidia Tanzania tangu uhuru) wamebanwa kuyapata hadi waamue kufunga ubalozi? Kwamba nchi nyingine zote ambako hawajafunga balozi zao hawajabaniwa kupata maslahi kama walivyobanwa Tanzania? Huyu jamaa na stori zake za kijinga anakera sana!
 
Uchumi gani tulionao kuwatisha Denmark?

Polepole bado anaishi kwenye ndoto ya awamu iliyopita, "Tanzania donor country" akija kuamka usingizini aambiwe yule bosi wake alishafariki, miradi yake mingi bado inaendelea kuwapasua watu vichwa serikalini hawajui waikamilishe vipi.
 
Mama akija kushituka,itakuwa imekula kwake.

Mama anaaminishwa Mbowe na CHADEMA ndio maaduii wake, kumbe maadui wake wamo humo humo katika chama chake na serikali yake.
Huyo aache kutudanganya, aseme ni matokeo ya ukanjanja wao na mambo yao ya hovyo , chafuzi, bambikia, nyanyasanyanyasa, uonevu na mengine yaweledi wa kibongo.
 
Back
Top Bottom