Humphrey Polepole aelezea sababu za Kibeberu ya nchi moja kufunga ubalozi

[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Nimemsikiliza Humphrey Polepole, nimegundua ni kijana makini sana nchi yetu imewahi kumpata,

Ni msomi anayezingatia misingi, sio msomi njaa

Natamani aje kua Kiongozi mkubwa hapa nchini, atasaidia.
Wewe ni mganga njaa kama yeye tu.
 
wewe, waambie wenzako watanzania wanahitaji katiba mpya - acha porojo!!

kwanza ushachanja?
 
(Kuanzia dakika ya 37:40): Story kuhusu Laurent Kabila kwamba ali-mobilize majeshi kutoka nchi mbalimbali siyo ya kweli. Ukweli ni kwamba (na unaujua vizuri) walioivamia Zaire ni majeshi ya Rwanda, Uganda na Burundi kwa kumtanguliza mbele Laurent Kabila kama kibaraka wao ili kuwahadaa wana Zaire na nchi jirani.
Nchi hizo zilipata support kutoka US, Canada, UK, Israel na Australia.
 

Sasa umeongea nini hapo mkuu..tofauti ya ulichokisema na alichokisema ni nini
 
Sasa umeongea nini hapo mkuu..tofauti ya ulichokisema na alichokisema ni nini
Maana ya Polepole ni kwamba Laurent Kabila aliunda jeshi. Kabila Sr hakuwahi kuunda (mobilize) jeshi ambalo lilipigana kumuondoa Mobutu madarakani. In fact hakuwahi kuwa na jeshi.
Majeshi yaliyoivamia Zaire yalikuwa ya serikali za Rwanda, Uganda na Burundi yakimtanguliza mbele Laurent Kabila ili kuwahadaa wana Zaire!
 
Huyu jamaa ana matatizo makubwa sana kichwani , yaani mtu anahangaika na mambaazi yake ili arefusha maisha leo hii mnasema sijui uzalendo, Hivi kuna nchi zinakula bata na zina demokrasia kama Nordic countries? kwa taarifa yenu hao jamaa sio wanafiki kabisa wameona kuliko kuendelea kuwa na ubalozo kwewnye nchi ya hovyo ni bora wajiondoe tu, mbona kenya hawajafunga ubalozi, na ukitaka kujua Tanzania bado kidiplomasia angalia wale mabalozi Mama Samia aliopokea hati zao za utambulisho juzi kati hapa, wooote Makao makuu yao ni Nairobi, Jiulize ni kwasababu gani? yaani mwaka jana enzi za mwendazake tulifungua balozi kibaaao tukijidai tunataka kukuza utalii, leo ubalozi unafunga shughuli hapo kwentu mnasema sijui mabeberu, akili za Dawa ni tofauti za kawaida za binadamu.
 
Hii sababu pole pole kaitoa wapi? Wenyewe wamesema ni kutoka na sababu za kiuchumi, kwanini tusikiamini kile walichosema wao
 
Mwenye kujua elimu ya huyu zwa zwa tafadhari.
 
Anazungumza matatizo ya nchi na nchi Kama Nani? Watu Kama Hawa walopokaji wasiachwe wahakaharibu mahusiano yetu
Huyo aliaminishwa na magu kuwa wahisani Ni mabeberu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…