Samia atosha tukutane2030
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 17,728
- 49,762
Kwa mifumo mibovu iliyowekwa na CCM, kuna nafasi ukikaa unakutana na bahasha nyingi sana. Unakuwa kama umeshika mpini, wengine wameshika makali. Kupata mgao wa milioni 50, 70, 100 bila msingi wowote ni jambo la kawaida tu
Polepole na watu wachache ndani ya CCM wanalalamikia maamuzi ya Samia na kundi lake kujichukulia nafasi zote. Lakini huyu huyu Polepole amesahau kauli yake ya mwaka 2020 aliposema fomu ya urais ndani ya CCM ni moja tu ya Magufuli
Kama mwaka 2020 katiba ya CCM haikuzuia wengine kugombea na fomu ikatoka moja tu, kwa nini leo 2025 uone kama katiba imevunjwa?
CCM ni yenu nyie, endeleeni kufanya mtakavyo. Kiwembe mlichotumia kuwachanja wengine 2020, ndicho kinachowachanja sasa 2025
Soma pia: