Humphrey Polepole ahubiri kuwa 2042 ndiyo mwisho wa Dunia na kurudi Yesu mara ya pili

Humphrey Polepole ahubiri kuwa 2042 ndiyo mwisho wa Dunia na kurudi Yesu mara ya pili

Katibu Mwenezi wa CCM, Hamfrey Polepole amesema mwisho wa dunia ni mwaka 2042. Akizungumza katika kipindi cha Sunday Worship cha WasafiTV amesema Yesu atarudi mwaka 2035 kulichukua kanisa (wateule wake) na kukaa nao mawinguni kwa miaka 7 hadi mwaka 2042 atakaposhuka kuihukumu dunia...
Kumbe siku hizi kawa nabii, naona nabii wa CCM.

Hakuna ajuaye muda wa la saa mwana wa Adamu atakaporudi, sasa mbona anapingana na hili.
 
Ha haa! Baada ya miaka hiyo saba ya Dunia kusafishwa, tutakaporudi, kila kitu kizuri kitakuwa cha Wasabato.. Mijumba mizuri, magari mazuri nk vyote watapewa wasabatoo.
 
Waache wendawazimu...tetesi za mwisho wa dunia zilikuwepo tangu siku nyingi..Kibwetere wa Uganda ndio hivyo alianza kuwaambia watu mwisho wa dunia unakaribia..matokeo yake aliondoka maisha ya mamia ya watu wasiokua na hatia. Shame on you!
 
Kumbe siku hizi kawa nabii, naona nabii wa CCM.
Hakuna ajuaye muda wa la saa mwana wa Adamu atakaporudi, sasa mbona anapingana na hili.

Hayo maneno angeongea Yule gwajboy wa kawe ingekuwa suala la Imani zaidi... Lkn akiongea kada wa ccm huo utakuwa uongo...
 

Mheshimiwa Polepole akihubiri kuhusu mwisho wa Dunia na Kurudi Yesu mara ya pili​

 
Huwa nashangaa Sana kwa waafrika kukomaa na imani hizi za kuja
Wooooooo.

Inabidi hata hii elimu ya kuletewa tuachane nayo sisi waafrika. Kwani kabla wazungu hawajaja, si tulikuwa tunaishi vizuri tu.

Hivi huduma za kisasa za afya, waafrika tuliletewa, ama tulijiundia?.

Huwa nawashangaa waafrika wenye mtindio wa ubongo kuponda dini huku karibu kila tunachofanya leo duniani (Cha kisasa) tumeletewa na wazungu. Mfano, dini, elimu, afya, huduma za usafiri, mikao ya ngono n.k.
 
Back
Top Bottom