ngosha omuchalo
Member
- Jul 17, 2015
- 75
- 29
Bwana Polepole wewe kama msomi, mzalendo na muungwana, unapowaita watanzania wenzako tena pengine wenye umri sawa na wazazi wako unao wajibu pia na uwezo wa kuwafungulia mashtaka mahakamani. Thats what courageous and brave people do in modern civilised world. Haitoshi Bwana Polepole kupayuka kila siku bila kuchukua hatua muafaka. Ni mahakama peke yake yenye jukumu la kikatiba kuhukumu watanzania, vinginevyo unataka tuishi katika mazingira ya utamaduni wa porini/ushenzini!
Ni wazi sasa Polepole umejitishwa mzigo wa uchunguzi, mwendesha mashtaka na hakimu dhidi ya Lowasa. Sina hakika pia kama unao mpango na dhamira ya kuwashughulikia watuhumiwa wengine hasa kwa misingi ya Ripoti za CAG ambazo zimeweka bayana upotevu wa fedha za umma nyingi zaidi kuliko zile unazoshupalia kila uchao!
Kiu ya Watanzania ni kuleta mabadiliko ya dhati ili pamoja na mambo mengine kuziba mianya ya ufisadi na kuimarisha taasisi zenye uwezo wa kuchukua hatua kila matendo ya ufisadi yanapojitokea. Watanzania hawana tatizo na watu binafsi au fisadi mmojammoja, bali mifumo ya utawala ambayo kimsingi imedumu zaidi ya miaka 50 sasa ikiwemo - "imperial presidency". This is the essence of the Change we yearn for. Sasa madhalo Lowasa amekubali kutekeleza sera ya UKAWA ya kutupatia katiba mpya kwa misingi ya maoni ya wananchi, huyo ndiye anastahili kuwa Rais wa Tanzania baada ya uchaguzi wa 25th Oktoba, 2015.
Polepole sio mnafiki ila ukiacha mapungufu madogo madogo ya kibinadamu, Polepole huwa anasimamia ukweli na ukweli siku zote utasimama.Pole pole hata CCM hatukuamini maana una ndimi mbili na ni mnafiki!
Hakukuwa na mchakato huru baada ya kulambishwa mabilioni, Mgombea urais kupitia UKAWA kanunua vyama vyote vinavyounda umoja huo na ndio maana ukaona waliokuwa wanajielewa kama Slaa na Lipumba wakaamua kukaa pembeni.Kwani ninyi(mtatiro) mchakato wenu wa kumpta rais ulikuwaje????.
Kuna haki hapo ww uliona au ushabiki usiokuwa na tija...siasa za maji taka...???
Nimefuatilia kwa makini sana hoja za Hamfrey pole pole.Nathubutu kusema mwanzo nilidhani ni kijana mzalendo anaeipenda nchi yake tena mkweli lakini nimegundua yafuatayo kutoka kwa Polepole.
1. H Polepole ana chuki binafsi na Mgombea wa upinzani.kwa nini nasema hivyo kabla ya uteuzi wa wabunge Polepole alisema ccm inapaswa kuwakata wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kama hawatafanya hivyo alikuwa tayari kuisema ccm nchi nzima.Mara baada ya uteuzi kupita na wale wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi kupita Polepole amegeuka na kuacha hoja hiyo.hiyo inaonyesha ana chuki na mgombea wa Ukawa.
2. Katika nchi ufisadi uliofanyika ni mkubwa sana na waliofisadi nchi wako wengi sana na pole pole anawajuwa lakini hajawahi hata siku moja kuwataja kwa Polepole ufisadi ni Richmond pekee vipi kuhusu EPA, Kagoda, meremeta, Escrow.uuzaji wa nyumba za serikali, uuzaji wa viwanda. Tukitaka kuiokoa nchi yetu basi tuwe wa kweli bila upendeleo.Chuki anayoionyesha pole pole ni ya wazi mno.
3. CCM ni chama chetu lakini kuna mambo mengi mabaya yaliyofanyika tuyaseme ili tukiokoe chama chetu.
Mgombea wetu ametoa hotuba inayoonyesha udhaifu mkubwa katika mambo mengi yanayohitaji kurekebishwa tuyaseme kwa uwazi kama Dr Pombe anavyosema. Mgombea wetu hashambulii mtu anaongelea hoja.polepole jikite kwenye hoja za kujenga nchi si kila siku unamshambulia mtu mmoja kama vile wewe huna dhambi Acha chuki haijengi.
pole pole hata ccm hatukuamini maana una ndimi mbili na ni mnafiki!
Unachoshindwa kujua ni kwamba hawa wote walifikishwa kwenye tume ya maadili. Sihawahi kusikia Lowasa alihojiwa mahali popote kwa kukosa maadili. Km unajua utusaidie wakina siye!Kwa mjibu wa viongozi na wafuasi wa cdm ,kama lowasa angekuwa fisadi basi angekuwa kashafungwa.na wanakwenda mbali zaidi na kusema aliye na ushaidi kuwa lowasa ni fisadi auweke hadharani au aende mahakamani.kwa sababu hizo,hata chenge,mhongo,ngereja,tibaijuka,rostam,karamagi n.k sio mafisadi pia,kwa sababu nao hawajashitakiwa mpaka sasa.Hivyo ccm hakuna fisadi hata mmoja.
Pole pole hata CCM hatukuamini maana una ndimi mbili na ni mnafiki!
Hawa wote hakuna hata mmoja mwenye kosa ila Lowasa ndiyo fisadi.Andrew Chenge, William Ngeleja, Anna Tibaijuka, Profesa Muhongo hawa wamekatwa?
Njaa tuzipeleke polepole.