Elections 2015 Humphrey Polepole: CCM ilifanya maamuzi ya kiume, Majizi na hasa kubwa lao yakakatwa...

polepole sio mnafiki ila ukiacha mapungufu madogo madogo ya kibinadamu, polepole huwa anasimamia ukweli na ukweli siku zote utasimama.

acha utoto wewe, watu wenye akili zao washashtuka.
Ficha umaamuma wako tulia usome comment zote kwa kina uelimike usikimbilie ku-comment kwa mshawasa wa akili ndogo.
 
Mmm. Naona CCM wanatupa bomu la ufisadi kwa Ukawa na Ukawa nao wanasema mbona na Ccm mafisadi wapo, hapo ngoma droo!!
 
hakukuwa na mchakato huru baada ya kulambishwa mabilioni, mgombea urais kupitia ukawa kanunua vyama vyote vinavyounda umoja huo na ndio maana ukaona waliokuwa wanajielewa kama slaa na lipumba wakaamua kukaa pembeni.

hoja nyepesi sana, kajipange zilishajibiwa hizi soma post za nyuma.
Comment zako kama hizi peleka facebook/....
 
Pole pole anazidi kujichafua....binafsi nilifikiri ni miongoni mwa vijana makini sana tulionao lakini naona anguko lake kwa kuamua kwake kutetea upande mmoja.... kipindi hiki kinahitaji kutoa maoni kwa taadhari kubwa.....utetezi wake kwa CCM na Magufuli unaelekea kumdhalilisha tu maana miaka 50 ya utawala wao inasema mengi ambayo unahitaji roho ya chuma kuyatetea....pamoja na mapungufu makubwa sana ya UKAWA ambayo kwasasa ni ngumu kueleweka kwa wafuasi wengi lakini msingi wa kuipumzisha CCM bila kujali matokeo yake utakuja kuleta manufaa vizazi vijavyo..... tunahitaji nguvu kubwa ya upinzani yenye tija ktk kuisimamia serikali.
 
Huyu Polepole lazima atakuwa mnafiki mkubwa sana. Yaani abaki ndani ya CCM akijidai kwa kujiamini kabisa kwamba yeye anawajua mafisadi kwa ukubwa wao na kwamba hivi sasa ameridhika kwamba wametoswa hivyo chama kimekuwa bora! Naweza kumwelewa akitoa msimamo dhidi ya Lowasa kuwa UKAWA (mtazamo wake) lakini si kuhusu mafisadi na ufisadi ndani ya CCM. Ni unafiki na/au ujinga uliopitiliza kutaka kutuaminisha (tena kwa jazba) uozo wa aina hiyo. Ni makosa kumpa attention mtu mwenye fikra duni kiasi hicho.
 

cho gani ainda huyo form six failure kazi yake ni koa bikira visichanavya chuo kikuu vilvyokuwa vikienda kufanya field (Msigwa alituthibitishia)
 
Njaa mbaya polepole amegeuka kuwa mwanaharakati wa kampeni ccm
 


Umeongea ya msingi, lakini kuna moja hujalizungumzia.

TWO wongs do not make its right. Kulikuwa na RUSHWA kwenye michakato ya UKAWA, na Kuna mafisadi UKAWA,waliothibitika na Bunge na waliotangazwa na wapinzani wenyewe. Hapa ndio UKAWA mlipokosea. Mlikuwa na kampeni nyepesi sana, kabla ya kunasa kwenye ndoano ya kupenda madaraka. Sasa wote mko kwenye dimbwi la tope la ufisadi na rushwa, mnatuiana vijembe nani msafi. HAKUNA. nyie wote ni wachafu toka mliporuhusu hao mliowaita mafisadi kutoka CCM kujiunga nanyi. Kutaka kuiondoa CCM hakuwasafishi hao mafisadi kw atuhuma walizorushiwa na wapinzani.

Hapa ndio ninamuelewa Dr.Slaa, na ninashindwa kuwaelewa nyie mliobakia.
 
Binafsi naona polepole siku hizi kapotea. Yule Polepole wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba si huyo tena. Amegeuka na kuonesha rangi yake halisi sasa....
 
Bwana polepole naomba utuweke sawa tafadhari;

Kwa tafsiri ya maneno yako katika mijadala kadhaa kama vile “majizi yaliyokatwa (majabali) “mmoja wao ni Mh Lowasa, Je katika wagombea 38 wa urais CCM ndani yao kuna Makamu wa rais, Waziri mkuu ,jaji mstaafu Augustino Ramadhani na viongozi wengine tena waheshimiwa tu. Je tuamini wote 33 ni majizi? (38 - 5). (Yaani wote 38 ukitoa 5 tuliowaona wakipelekwa NEC).wengine ni akina nani maana umemtaja Dr Magufuli tuvambaye kwako na CCM ni msafi sana?

Huwa unatoa definition za kauli mfano, Mageuzi,Mabadiliko,mpumbavu nk. je unavyowaita watu Majizi au mafisadi huoni kama unafanya kazi ya polisi investigator, prosecutor na hakimu? Je maana ya majizi ni nini? na unapingana na ukweli kwamba chombo kinachothibitisha mtu ni mwizi au siye ni mahakama?


Nilishuhudia ukiambiwa kuhusu tuhuma za mgombea wa CCM tena kuhusu report ya CAG kwenye wizara aliyopo Mh Dr Magufuli na tuhuma ya uuzwaji wa nyumba za selikari hukuzungumzia chochote au sio kweli kwamba kuna billions zinahitaji maelezo? Pamoja na kutetea watu kuitwa wapumbavu na malofa kwa tafsiri zako ni sahihi, kwakuwa tulikuona kama mwananchi wa kawaida mchambuzi na mpenda haki, kwanini tusiamini kwamba unachuki binafsi na mh Lowasa maana ndio pekee unamshambulia sana?

Kwakuwa kupenda chama chochote ni haki yako ya kikatiba, kwanini usivae tu sare za kijani ukaanza kupigia chama cha CCM kampeni badala ya sisi kudhania tunamsikiliza mchambuzi wa siasa kumbe ni kada tena anakayeshambulia upande mmoja tu, tutakusikiliza lakini hatutakushangaa kama vile tunavyomsikiliza Nape au Mzee Kinana.


Ni mimi mpiga kura nisiye na chama ila huwa nafuatilia hii mijadala ili nijiridhishe kura yangu haswa nimpe nani.
 
Nahisi huyu dogo sifa za rasmu mpya ya katiba zinamchanganya. Sijui hata hajiulizi hivi lowasa /ukawa wanaungwa mkono na watu wangapi? Yeye kama anatumiwa kuendelea kumchafua rais wetu hatutakubali hili hata kidogo.
 
Suala la kusafishwa sio la vyama au MTU kama wewe au polepole Mahakama pekee ndio chombo sahihi cha kumsafisha MTU ndio maana Mh.sana tena sana mpiga debe Wa CCM aliyeshindwa kuitetea rasimu akiyohangaika nayo
Tanzania nzima tunamtaka akamfungulie kesi Lowassa.
 
Polepole wewe mwenyewe unavyoongea na kutupa tupa mikono nikukosa maadili pili nawewe pamoja na mzee warioba mbona mnawapigia debe waliyoikataa katiba na kuwatukana kama si kupigwa kabisa ni njaa kutafuta maslahi binafsi au???!!
 
Polepole ni mmoja ya wanamkakati wa CCM kwa sasa...

Kama yeye alivyotupilia mbali misingi ya katiba pendekezwa na kumpigia kampeni Makamu Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba kwasababu ya mikakati ya KiCCM, ndivyo ilivyo kwa UKAWA kumchukua Lowasa kwasababu za kimkakati....

Hizo porojo nyingine nyiingi ni unafiki tu....

Siasa ni mchezo na ndio hata polepole anaucheza kwa sasa...

Huyu ni kijana ambaye hawezi kuishi nje ya mfumo wa KiCCM...
 
Eti uliwaambia ccm wawakate, kumbe wao wanafanya kazi kwa remote ya Polepole, sasa unataka na UKAWA wakusikilize,
 
Polepole alifanya kazi ya katiba tu ambayo chama chake kiliikataa huku katika midaharo hana jipya zaidi ya kuwapotosha na kuwachanganya watu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…