Uchaguzi 2020 Humphrey Polepole: Dkt. Magufuli atachukua fomu ya Urais 06 Agosti Dodoma. Mwanachama aliyepiga mazonge kwenye kura za maoni atashikishwa adabu



Hayo yamesemwa na Mzee Hamphrey pole pole ambaye ni Katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho , Kwamba wale wote waliopita kimagumashi hawana nafasi ya kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge au udiwani.

Hakufafanua magumashi anayoyasema kama ni rushwa au jambo lingine , bali inafahamika kwamba 90% ya watia nia wa ccm walimwaga rushwa , wakiwemo wale waliotoa rushwa kwa kipindi cha miaka 4 mfululizo .
 
Kumekucha
 
Mazoea hujenga tabia alisema wapinza nisawa na corona
https://www.facebook.com/
 
Humphrey Polepole mnapoteza muda chama chenu kinazidi kupasuka :


''Wagombea Ubunge ARUSHA CCM Wampinga Mgombea Mwenzao ''

Wagombea Wawili walioshiriki kwenye mchakato wa uchaguzi wa kura za maoni wa ndani ya chama cha mapinduzi katika jimbo la Arusha wamejitokeza hadharani kumpinga mmoja wa wagombea walioshiriki mchakato huo kwa kusema alitoa rushwa.
 
Mambo ya Diamond na Alikiba kugombea penseli yameanza, Polepole anagombea wimbo wa Taifa na ni 'Yeyee' ya TID. Hivi chama kilichokufa kinawapa mchamchaka hivi?
 
Kwani waandishi wa habari wapo wangapi? Je kuna kanuni inazuia kufanya kikao wakati mmoja na mwenzio?
 
Waliopora nembo ya M4C mwaka 2015 walikuwa ni chama gani?

Na je,TID ana hati miiki ya hiyo slogan?

Na,wana uhakika gani kama wameiba?

Na,slogan hiyo imetumiwa na chama kama chama au imetumiwa tu na baadhi ya wanachama kwa mapenzi yao?
Wala usingepoteza muda kujibu
 
Tatizo linaanzia hapa: Hoja za CCM zinajibika kirahisi sana ila hoja za Upinzani CCM hawawezi kuzijibu kutokana na njia walizotumia kupita. Sasa options ni 2. Kuzima wapinzani wasiendelee kusikika au CCM kujibu hoja za wapinzani ambazo zitamfanya Rais mpendwa abadili muelekeo aliokuwa anakwenda.
 
h
Nimwombe, ajikite kwenye sera za Chama Chetu. Mambo ya kujibu mapigo au kuzungumzia vyama vingine "SIYO KAZI YAKE" ni kazi ya Msajili wa vyama na NEC.
historia ya lissu ipo wazi sana kwamba uchaguzi wowote kwake hushinda mkuu sera za chama mda wake ni kwenye majukwaa but kwa aliyoyaongea jana ulikua mda mhafaka wa kuyazungumzia maana kampen bado so ulitataka aanze kuzungumzia sera za chama chake wakati kampeni bado?

itoshe kusema Mh Mbowe mungu akubariki na vizazi vijavyo vitakukumbuka umepika vijana mfano wa wazi mh mwalim iyo ni hazina nyingine katika taifa hili ,hivyo kumteua kuwa mgombea mwenza wa urais nawapa asilimia 200 japo kimahesabu hua hamna
 
mkuu upo sawa kabisa na lingune hoja za ccm ni zile zile ambanzo mwenyekiti wao amekua akizizungumza kila wakati kwa miaka mitano so wananchi wameisha zizoea na ikumbukwe prof mkandala kwenye kongamano moja aliema kitu wennda hata viongozi wa ccm hawakutilia mahanani sana japo ni jambo la msingi alilo sema ,kwamba.

Waweza kua baba mzuri katika familia na unawapa kila kitu familia ila kama hawana furaha moyoni ni kazi bure , ni maneno machache yenye wigo mpana wa kufikirisha sana na pamoja na kumlinganiasha baba wa taifa na mh rais wa sasa katika kujenga hoja zake alisema HATIMA YA CCM BADO HAIJULIKANI JAPO DALILI ZA MVUA NI MAWINGU ,VIPI ndugu zangu na viongozi wa ccm hua wanayatafakari maneno haya hata siku moja kwamba yana uzito wa kipekee na kuyafanyia kazi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…