Uchaguzi 2020 Humphrey Polepole: Dkt. Magufuli atachukua fomu ya Urais 06 Agosti Dodoma. Mwanachama aliyepiga mazonge kwenye kura za maoni atashikishwa adabu

Asante sana, huwa tunashindana na watoto wangu kila wakati kukiwa na kive event kwenye TV huwa tunashindana Elimu bure zimeenda shs ngapi, Zimejengwa zahanati ngapi, Wanafunzi wa Chuo pesa kiasi gani,. Uchumi unapanda kwa asilia ngapi, ndege ngapi. So predictable.

Kingine kwenye front line hakuna talkers. Hakuna watu watatu mfano wa Mzee Yusuf Makamba watapanda kwenye stage wafikishe msg kwa njia ya utani n.k Front line yote iko Serious and cold, eg Jafo, Lukuvi, Zungu, Majaliwa even Mama Samia sio mwongeaji japokuwa ana haiba ya kupendwa.

Watanzania wanapenda watu waongeaji, wachekeshaji n.k ukiwa mkali watanzania wana tabia ya kukuogopa na kukukwepa kwa sababu hawajui kumface mtu na kumwambia ukweli.
 
Summary ya press ya Polepole:

1.kuwafokea wananchi waliompokea Lissu Airport.
2. kufokea chadema kuhusu ubeti wa nyimbo ya taifa.
3. Kupiga kampeni kabla ya uchaguzi.
4. kuwafokea chadema kwa kutumia neno ambalo yeye anasema ni mali ya T.I.D.
5. Kutaja list ya wasanii kama kivutio cha kuongeza wahudhuriaji kwenye kampeni za CCM (hapa kamtaja hadi man walter ambaye sio msanii)

My Take:
(a)CCM wamepanic baada ya ujio wa Lissu nchini hususani baada ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya Chadema.
(b) CCM wamepandwa na jazba kwa spana walizoonjeshwa kidogo kwenye vikao vya Chadema vilivyofanyika Mlimani City.

NB:
Mataga safari hii mmejiingiza kwenye kina kirefu chenye mamba wakali mnoo 🤣🤣🤣
 
Your browser is not able to display this video.
 
Mbona kama ilikuwa ni press ya kuwachamba cdm?
 
Hisia zimeanza kuwa kali na kwa mara ya kwanza nasikia CCM wakikiri kupungukiwa uvumilivu. Polepole amekerwa na CHADEMA kuuchezea wimbo wa taifa na katika hilo amekiri hakuna uvumilivu wa kisiasa.

Naye Tundu Lissu amedai NEC hawawezi kumkata kwa sababu hajavunja sheria yoyote ya maadili na kwamba atamuwekea pingamizi Dr Magufuli.

Kiufupi dalili zote zinaonyesha kwamba kampeni za mwaka huu hazitakuwa za kitoto maana Polepole kaishiwa uvumilivu na kusema Maalim Seif amekomaa usoni ampishe kijana Mwinyi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Polepole amedhalilisha Maalim Seif amuombe radhi hadharani. Waingereza wanaita ile ni “age discrimination.”
 
Muumba mbingu na nchi ampe afya njema na maisha marefu muheshimiwa Polepole kwa hekima na busara zake zilizotukuka.
 
tuendelee kulisha familia zetu hao jamaa mmhh achaneni nao tu..wanaumiza vichwa juzi tu lowassa tulikuwa nae ukawa leo anasema tumuunge mkono magufuli..ukiwa na hasira sana kunywa sumu ni jambo la dakika moja tu
 
kijana anaipenda ccm hata baada ya miaka 60 ta uhuru namuonea huruma
 
Fomu chukueni lakini Rais wa Tanzania ajaye ni Tundu Antipas Lissu, inyeshe isinyeshe. Hata kama mtaamua kumtangaza JPM kwa kutumia NEC na Polisi, mjue nguvu ya umma itatumika kumchomoa JPM Ikulu kama Ivory Coast walivyomchomoa Laurent Bbagbo mwaka 2012
 
Bwana Polepole muanzie na Jimbo la Rorya. Namba 1,2, na 3 nafasi zao zina walakini.
 
Mwenezi wa CCM ndugu Polepole amesema chama chake kimesikitishwa na kitendo cha Chadema kupora kaulimbiu ya TID ijulikanayo kama Ni Yeye

Polepole amesisitiza kuiburuza CCM mahakamani ili TID apate haki yake.

Maendeleo hayana vyama!
Angalia ulichoandika
 
Hili eti ndiyo jembe la CCM. Ndiye katibu wa itikadi na uenezi. Kutoa taarifa tu za mgombea wao kwenda kuchukua fomu mpaka tukio lirushwe live na TV....

Ama kweli CHEMA CHAJIUZA, KIBAYA CHAJITEMBEZA CHENYEWE USIKU NA MCHANA ILI KIJIUZE...

å Chema ni CHADEMA na ACT - Wazalendo. Vinajiuza vyenyewe hivi...

å Kibaya ni CCM, kinajitembeza na kujiuza hiki mithili ya changudoa.....!
 
Polepole atuambie hapa alitolea tamko gani? Au kunya anye kuku, bata atakuwa kaharisha?

Your browser is not able to display this video.
 

[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] ila Siasa Bana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…