Humphrey Polepole hajamshitua mtu yeyote, amejitekenya na kucheka mwenyewe

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Tangu lini Tanzania iliwahi kuwa na uchaguzi huru na haki? Anajua kuwa mwenyekiti wa CCM ndiye Rais wa Tanzania pia anaeteua mwenyekiti na wajumbe wa tume ya uchaguzi? Anajua kuwa matokeo ya uchaguzi hayahojiwi mahakamani?

Wakati yeye akiwa mwenezi anakumbuka kama vyama vya siasa vilipigwa marufuku kufanya kazi za siasa? Anakumbuka kuwa wakati yeye akiwa mwenezi wa CCM wagombea wa upinzani walienguliwa? Anaijua Richmond na escrow?

Ni udini tu kama wenzake hana hoja zinazoihangaisha nchi na dunia hasa katika zama hizi za migogoro mikubwa ya Gaza, Ukraine, Somalia Sudan msumbiji Niger Nigeria Mali Burkina Faso, DRC, Hait, nk. Poor timing kwakuwa dunia nzima masikio yao Yako Gaza, Iran, Israel, Ukraine, Sudan, DRC....
 
Hii picha hapo Chini ni ya watoto wa kipenzi chetu cha dhati Imam Hussain ibn Ali A.S, Ali Al- Sajjad ibn Hussain na Ali Al-Akbar ibn Husssain. Imam Hussain aliyeuwawa kikatili kuutetea na kuulinda uislamu dhidi ya dhulma ukandamizaji unyanyasaji na uonevu.

Waliposikia tu habari baba yao kuuwawa kikatili walitimua mbio huku wakilia. Yani ni simanzi siku ya Ashura.



adriz Covax
 
Tatizo lenu wavaa bakozi huwa mna inferiority complex. Ni udini udini udini. Tangu lini sifa ya mtu kuwa Rais ikawa dini yake. Lakini kwenu wavaa bakozi ni sifa mojawapo eti muislamu mwenzetu.

Sasa hivi kila siku mnaimba, ohooo mara hawampendi kwa sababu ni muislamu. Ni ujinga na upumbavu tupu.

Kuteka watu, kutesa watu, kuwapoteza watu, kuwafunga watu na kuwaua watu ni matendo yanayofurahiwa na dini yoyote???

Kama yanafanyika haya hamyasikii kila kona.???

Kwa kuwa yanafanyika kwa mtawala mwenye imani fulani ndo watu wasilalamikie mambo ya hovyo.

Kifupi hapa siyo Iran wala Yemen kwa watawala wa Jihad war au sharia.
 
We mpaka umeamua kuanzisha uzi basi umeumia sana
 
Kwa hiyo alitakiwa aendelee kuongelea kwenye hayo uliyoyasema mpaka lini?
 
Mwamba umeelekeza mashambulizi yako kutumia mizinga mikali Kwa Waislamu na Uislamu.
SoMo ; watawala wa nchi hutafuta ngao ya kujilinda hata Kwa hoja za hovyo.
Wakati wa Magu licha kuhubiri kila jumapili mwisho akaangukia kwenye Usukuma kama ngao.
So, take a tranquilizer and relax ili uache kutukana dini nzima.
 
Kwenye hizo paragraph za kwanza umeandika vizuri sana, sasa huko nyuma ulisema "Chadema kususia uchaguzi Imewaumiza wengi" sasa naona unajipinga mwenyewe (contradiction); at least ni kuwa unaamini Chadema wamefanya right choice.
Sasa kimpangilio (consistence) wa story yako, kwako wewe inategemea sana na nani asemwaye, kama ni Chadema anagomea Samia (CCM)basi hawako sawa (right), ila kama Polepole kamgomea Samia basi ni MDINI, kwa hiyo na wewe ni Mdini?

MMMMMMMMMMMMMMMMMMMMMMMM
 
Kichaka anachofichwa Samia ni Udini tu, ni kama yeye ndio mwislam wa kwanza kuwa Rais.

Hatudanganyiki!
Mbona Sioni kafanya nn kibaya kuwashinda Nyerere, Mzee Mwinyi, Mkapa Kikwete na Magufuli? Nikiwa mdogo nyumba yetu ilichomwa moto na Nyerere eti twende kwenye vijiji vya ujamaa ambako hakuna nyumba , maji chakula Wala chochote. Samia hajafikia hapo hata robo yake. Mzee Mwinyi chuo Kikuu cha dsm kilifungwa na wanafunzi wengi kufukuzwa chuo, Hawa akina James mbatia ni wahanga wa tukio hilo, na alilizika Azimio la Arusha na kuja na Azimio la Zanzibar, Samia hajafanya hivyo. Mkapa ndiyo usiseme kabisa, katuma jeshi kuua watu Zanzibar, kauza nyumba na mashirika yote ya umma kwa bei ya kutupwa, Kikwete na Magufuli ndio usiseme kabisa.

Huyu mama amekuja kufukia mianya yenu ya ulaji, ndio maana Kila mara hamuachi kutaja waarabu.

Focus ya Dunia Sasa hivi haiko Tanzania, Iko Ukraine, Israel na Iran DRC Somalia Sudan msumbiji,etc. bwanamdogo kapiga patupu kwakuwa lengo lake lilikuwa kuongeza mwangwi kimataifa kuhusu udini wao, lakini amesahau kuwa dunia Ina vipimo vyake na viwango vyake vya uhalifu ambavyo Tanzania haijavifikia hata kidogo kiasi cha kugeuzia shingo na macho.

Tanzania ndio Geneva ya Afrika so far hasa kwenye eneo la maziwa makuu.
 
Kwa taarifa yako: wewe ndio umeamua kujitekenya na kujicheka mwenyewe


لا إصلاحات لا انتخابات
Wacha tuone nani kajitekenya hapo. Huko Cameron, Uganda, Rwanda Kuna watu wako madarakani karibu miaka 40+ na dunia haisemi lolote, ndiyo useme Tanzania Kuna hali mbaya sana njooni muone.

Ukimuona mtu katekwa basi alikuwa na vigezo vyooote vya kutekwa ama na mwenye mke, aliyemdhulumu, anaetaka kuisagia kunguni Tanzania au watu wa usalama wa nchi. Ndio maana wewe na mm hatukutekwa maana tumekosa vigezo vya kutekwa. Mfano, wale akina Azori, Kombe , na wengine, Dr. Magwepande, Kasimu Hanga, Kambona, Mzee Jumbe, nk hawakupata madhira wakati wa Samia. Mama kafukia mashimo yao.

Shida kubwa hapa ni udini tu, finito.
 
Kwa taarifa yako: wewe ndio umeamua kujitekenya na kujicheka mwenyewe


لا إصلاحات لا انتخابات
Hiyo ni dhamira utashi na haki yake usimhukumu kwa lolote. Wewe endelea na maisha yako na yeye na masha yake
 
Watu mnamawazo ya ovyo, kwani amejiuzulu ili awashtue watu!?
Watu wengine wa ajabu sana. yaani kujiuzulu kiongozi mpaka eti aambiwe na viongozi wanaowataka wao, ikiwa hivyo ndio roho zenu zinakuwa kwatu. Akijiuzilu kwa utashi wake nongwa.
Mtu anakuja hoja eti kwanini hakujiuzulu kipindi kile au hizo sababu anazozitoa kwa ajili ya kujiuzulu mbona zilikuwepo kitambo mbona hakujiuzulu.... hayo ni mawazo ya hovyo sana. Kwa hiyo ukitoka nyumbani na mavi kwenye pindo la suruali, ukaja shituka uko barabarani kwamba una mavi, usijisafishe kisa ulikuwa nayo toka unaondoka nyumbani huo kama sio uhayawani ni nini.
 
Mimi ni muumini wa vyama vingi hasa bungeni kuliko Ikulu kwa Sasa. Maisha ya watanzania yanajadiliwa bungeni zaidi kuliko Ikulu. Cdm kususa kumeumiza hata wale wanaonyonga mikono yao wakipiga mayowe ya peeeeople s, lakini watu wametajirikia cdm kwa kuwa wabunge kupitia cdm. Akina sungu wana mahoteli, akina tumbili na Nasari waliibukia chadema. Kuacha kushiriki haikuwa sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…