Humphrey Polepole: "Hatuwezi kuwa nchi inaendeshwa kama idara ya 'Fire'

Ila wabongo akili zetu sijui vp, yani mkuu watu bado wanauliwa hadi sasa ila wewe bado Ben tu?
Hiyo avatar uliyoweka ndo inakuponza..yy Hana uhalali huo wakati aliua watu wengi sana..kwakuwa kawekwa nje ya system ndo anaongea??
 
Hiyo avatar uliyoweka ndo inakuponza..yy Hana uhalali huo wakati aliua watu wengi sana..kwakuwa kawekwa nje ya system ndo anaongea??
Kawekwa nje ya system kvp wakati alikuwa balozi na kijiuzulu mwenyewe? Hakuna watu wenye uhalali na wasio na uhalali kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake hivyo ni wewe tu kuyasikiliza au kuyapuuza ila hakuna watu ambao wao ndio wenye uhalali.
 
Kuna mdau ananiuliza naishi wapi? Kuwa yote yametokea 😂

Wanashindwa kujenga hoja hata ukiwauliza simple questions wanaleta dhihaka
 
Ujinga mtupu.
 
Hana legitimacy...hyu ni mganga njaa tu...angekuwa heche ama lissu ama mnyika anatoa hxo nondo tungekaa kuelewa siyo hyu mhuni....buyu la asali limeshamponyoka tyri anatapatapa tu
Ni nani ccm mwenye legitimacy ? nitajie wa tatu tu
 
Ni nani ccm mwenye legitimacy ? nitajie wa tatu tu
Nakupa mfano mmoja tu...Mzee warioba...tangu enzi ya Jiwe alikuwa anajaribu sana kusema na mpk sasa anasema....ila ndo hvyo tena mfumo unambinya....shida yangu mm na Slow slow ni mmoja tu....hoja zooote anazoongea ni za kwli kabisa lakini je ana uhalali wa kuongea anayoyasema???....ilhali yy ndo engineer wa haya yte yanayotokea sasa....kuzima mtandao yy alikuwa ni sehemu ya timu na sasa inatokea....uchafuzi wa uchaguzi na watu kupita bilq kupingwa yy alikuwa ni sehemu ya hlo tatizo...watu kupotezwa yy alikuwepo enzi hzo....sasa huu uchungu wa sasa anatoa wapi....mm naona ni namna ya kupigania maslahi yake tu....anajua akitoka ubalozi kituo inqchofqtq ni kutupiwa virago na hlo kastukia....kaona abutue sufuria la mboga...
 
Slowslow anaweza kuwa sahihi lakini historia ina mu hukumu. Kama unakumbuka mchoro wa 1.5 tr wakati wa jiwe alichora ujinga sana. Eti sasa anajifanya mkombozi. Acha apambane na ishu zake
 
kweli
Magufuli alikuwa na mapungufu kama binadamu wa kawaida
ILA
katika swala la malezi
kwangu binafsi atabaki kuwa
MZAZI NA BABA BORA WA MUDA WOTE.

Magufuli alijua vizuri malezi ya watoto wake.
Hata huyu Jesca hadi kujulikana kipindi kile
ni baada ya kufeli shuleni.

Na siku ya msiba wa baba yao
ndipo watu waliwaona vijana wakubwa kabisa wa marehemu.

Hatukuwahi kusikia wala kuwasoma sehemu
wakirumbana na trafic barabarani, kukwepa kodi bandarini wala kutumia nafasi ya baba yao kwa manufaa yao binafsi.

Je, ni nani hakuwafahamu akina Miraji kikwete, Ridhiwani kikwete?
ama hata huyu Abdul Samia?

Kwani Magufuli alishindwa kuwapa wanae hiyo nafasi?
Hata huyu Jesca kugombea mwaka huu
huo ubunge ni kiini macho tu
kutoka ile kambi ya mstaafu
wakiwaza kura za ukanda wa ziwa.
 
Ok sawa twende taratibu sasa kukosa uhali wa kuongea kwa sababu ya term iliyopita ili faa akae kmy kwa kipndi ndo tupate uhalali wake
 
Ok sawa twende taratibu sasa kukosa uhali wa kuongea kwa sababu ya term iliyopita ili faa akae kmy kwa kipndi ndo tupate uhalali wake
Njia nzuri zaidi ilifaa ajiuzulu pasi na kuita conference Kila siku za waandishi na yoote anayolalamikia angempa whistleblower mwingine aseme asiye na makandokando....makamu wa rais,waziri mkuu wanaonekana ni watu ambao wamenyooka na wanafaa lakini na wao wakitoka na kuanza kulalamika sasahivi tutawauliza kilekile....Wana legitimacy ya kuongea?? Ilhali kwny utawala ulopita walikuwa ni sehemu ya timu na hawakuwahi kulalama kwa yalokuwa yanaendelea??
 
Angeamua kukaa kmy na akaendelea kula bata ubalozini au na hilo angekua amekosea? Au kwa mawazo yako unahisi kuna nafasi kubwa aliiwaza uchaguz huu
 
Angeamua kukaa kmy na akaendelea kula bata ubalozini au na hilo angekua amekosea? Au kwa mawazo yako unahisi kuna nafasi kubwa aliiwaza uchaguz huu
Wanasiasa ni watu ambao wanachungulia jambo kwa mbali...hyu alipoteuliwa kuwa Balozi Malawi alisema Kuna watu walimwambia mama ndo anakutupa hvyo yy akawa anakataa...alipotupwa mbali zaidi huko Cuba ndo akili ikaanza kumkaa sawa sasa na akanusa hatari....hii kelele ya kupiga kwmba Kuna wahuni sijui hawakufanikiwa kuwamaliza ni kutapatapa tu kwa kuwa mfumo walotaka kutengeneza wao umeshindikana na infact hyu ni whistleblower tu...nyuma yake Kuna powerful people ndo wanamsukuma kusema wakiwa na wao wanasukuma kete zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…