Humphrey Polepole kuwa makini, Samaki yake maji

Humphrey Polepole kuwa makini, Samaki yake maji

Mzee Polepole, akina Nape walipoenda kwa Mzee wako wakipiga magoti wanalia wakiomba msamaha hawakuwa wajinga, walijua fika kwamba ndani ya CCM mfumo wa kukosoana waziwazi haupo, na ndiyo maana sisi na wengine tumeshalitambua hilo na tumeamua kwa pamoja kupigania katiba mpya ili tuwe na mfumo thabiti wa kukosoana wakati watawala wanapokwenda siko.

Sasa ndugu unaowaita wahuni wamekubeep ili ukiendelea na tabia zako za chokochoko wakupigie kabisa. Pole sana ndugu. - nakushauri kaa kimya mziki wa kukosoa CCM na Serikali yake hutauweza - waachie Wanaume.
Umeongea kwa hisia na hekima mpaka nimejikuta naingiwa na huruma na ndugu yetu polepole. Mifumo yetu ya Nchi haitoi room kwa wanaharakati kutoka kada ya siasa labda Rais mwenyewe kwa utashi wake aamue kuruhusu mijadala. Ndugu polepole ni opportunist kama walivyo wengine na ndio maana aliienjoy sana political atmosphere ya kipindi cha jpm. Kwa hali hii ndugu polepole alishiriki kwa nomna moja ama nyingine kuwakata mikia baadhi ya wanachama wenzake ambao kimtazamo walikuwa kinyume na JPM. Sasa baada ya kinga kuondoka kufuatia kifo cha mwanachato kibao kimegeuka watu wanataka kurevenge kwa ndugu yetu polepole. Tabia ya unafiki miongoni mwetu Watanzania inatutafuna sana polepole anajua fika kuwa tunaitaji katiba mpya kuliko matakataka yake ya shule ya uongozi
 
Angechagua kua na wananchi kipind kile cha teka, tesa, ua, funga, weka ndan, tungemuelewa sana!!
Brother ukipewa viette akili zote zinahama kutoka kichwani kwenda kusikojulikana. Polepole anatafuta sympathy tu kwa sababu watu wanarudisha mapigo hasa waliokatwa mikia enzi hizo atulie tu dawa imuingie
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Alituambia unyakuo ni 2035 - sasa hatujui kama ndiyo huo umeanzia pale kwake [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wale wote wazi wa mali za CCM. Wanaanza kutafuta namna ya kurudisha mali walizoiba. Tunaikumbuka kamati ya uchunguzi za mali za CCM. Bashiru na wezake na Polepole ni lazima waindoke kwanza. Nape na Mzee Bulembo (Jumuhiya ya wazazi) walikula sana na JPM alirudisha yote kwa CCM chama kikawa na pesa sana za kufanya uchaguzi bila ya kuomba kwa matajiri. Sasa wanataka chama kiruri kulekule kwa JMK ya Nape na Kinana. Makamba
 
ACHA MVUA INYESHE TUJUE PANAPOVUJA.

WASIMUWEKEE SUMU TU MPAMBANO HAUTANOGA AKIFA.
 
Anatakiwa aendelee kuongea ili tujue kinachoendelea katika Nchi Yetu
Anaweza kuendelea kuongea ila tukakosa kuyasikia maneno yake kutokana na wale wasiopenda kusikia maneno yake wanaweza kumzima wakati wowote.

So anatakiwa kuwa makini na kuongea kwake ili tuendelee kuwa naye!.
 
''Tusinyamazishane,kwa sababu mkininyamazisha naweza kusema hata yale ambayo hawataki kusikia"anasahau kuwa huko ndani ya chama vipo vyombo vinavyoweza kumnyamazisha ukiachilia mbali serikali,huyu anataka kupimana ubavu na nani??Anapeka mashtaka kwa wananchi akidhani bado anapendwa kama yule polepole wa Rasimu za katiba ya Warioba kumbe huyu ni tofauti kabisa kama mbingu na ardhi,alishakengeuka ni msaka fulsa tu aliyekuwa hashikiki kipindi cha mwendazake.Acha tuendelee kuangalia huu mtanange japo najua hata kaa ashinde.
 
Polepole kumbuka mshahara wa dhambi ni mauti, uliyotenda, ulivyodhulumu wengine ulipokuwa na 'cheo' utapimiwa kipimo kilekile! bazazi mkubwa
 
Mzee Polepole, akina Nape walipoenda kwa Mzee wako wakipiga magoti wanalia wakiomba msamaha hawakuwa wajinga, walijua fika kwamba ndani ya CCM mfumo wa kukosoana waziwazi haupo, na ndiyo maana sisi na wengine tumeshalitambua hilo na tumeamua kwa pamoja kupigania katiba mpya ili tuwe na mfumo thabiti wa kukosoana wakati watawala wanapokwenda siko.

Sasa ndugu unaowaita wahuni wamekubeep ili ukiendelea na tabia zako za chokochoko wakupigie kabisa. Pole sana ndugu. - nakushauri kaa kimya mziki wa kukosoa CCM na Serikali yake hutauweza - waachie Wanaume.

Kwa nini unamlazimisha kukaa kimya!?
 
Nimeikuta mahali hii

Ndugu yangu Polepole nakukumbusha Newton Third Law of Motion. Action and reaction are equal and opposite. Ajifunze awamu ya tano ilivyoshughulika na Membe na Lissu ndivyo wanasiasa wanavyoweza kufanyiana.

Siasa sio sawa na kazi za Civil Society. In politics you deal with matter in cycles not direct but in civil society you can go direct. Don't be direct in politics watakumaliza.

Kama jinsi ambavyo kuna kinga, haki na madaraka ya Bunge vivyo hivyo kuna kinga, haki na madaraka ya Rais.

Rais anaapa kulinda mambo mawili 1. Katiba na 2. Urais wenyewe. So ukigusa katiba na Urais ni sawa na umerusha jiwe kwenye makazi ya nyuki.

Bulembo ameonyesha chuki waliyo nayo unaowaita wahuni dhidi yenu. They capable of anything wasije kurudi kwenye zama za awamu ya tano.

Yupo Bwana mmoja Tanga kwenye kikao cha tadhimini ya operesheni sangara Tanga 2009 alisimama kwa sauti kubwa na madaha akamwambia Mbowe; Mwenyekiti mimi niko tayari kupambana kufa na kupona. Mbowe akamwambia kamanda pambana kupona ukifa harakati zitakufa.

Polepole kwa anavyoenda anapambana kufa na kupona, retreat man upambane kupona maana hawatanyamaza mpaka waridhike wamekumaliza.

Ulimboka ilikuwa awamu ya nne, Kombe awamu ya tatu, Lissu awamu ya tano, akina Chipaka awamu ya kwanza so awamu ya sita nayo lazima iwe na wake

My take
Polepole unaweza kufukuzwa CCM ili uwe nchikavu kwanza
Wamemfukuza
 
Back
Top Bottom