Humphrey Polepole: Mambo ya machifu hayana msaada kwa taifa, yanaweza kuleta ukabila na mgawanyiko, yanapaswa kupingwa

Hivi Tanzania mtu pekee aliyekuwa na akili timamu ni mwalimu pekee?
No hata kama si kuwa ni yeye pekee lakini kama taifa tumempa hadhi ya kuwa baba wa taifa letu. So msingi wa taifa letu ni ule aliouasisi na ndiyo reference pekee tuliyonayo so far kwa nchi yetu
 
Ujinga huu unaoandika hapa wa kumuabudu mwenyekiti wa chama, ndio hasa kiu yetu kwamba uishe hapa Tanzania
Chama ni jumuia ya wengi, haiwezekani mmoja afanye Jambo na wote mulibebe eti ni mwenyekiti kaamua,
No sense!
Maamuzi ya chama yanafanywa na chama, sio mwenyekiti wa chama!
Polepole sio mbumbumbu, analijua hilo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hili hata mimi nalipinga...Kukasimu madaraka ya kitaasisi kwa mtu moja ni hatari sana....Si afya kwa yeyote hata kwa Mh. Mwenyekiti mwenyewe. Leo ni kwa mazuri je yakitokea maovu je?
 
Humphrey Polepole amesema kuwa

"Mambo ya Machifu yanatusaidia nini kama taifa?nasema jambo hili sio jema,naliona linadhoofisha Utanzania wetu,likiendelea bila kukemewa litaibua tuliyoyazika ya hisia za ukabila, usisi na uwao, Mwalimu Nyerere aliona mbali kukataa haya mambo kwani yataligawa taifa"

"Yapo maeneo uchifu ulishaondoka,haupo. Tulishakubaliana uchifu ni ukoo wenu, mna kiongozi wa ukoo mnazungumza mambo yenu binafsi ya kifamilia leo serikali ikizungumzia uchifu hawa nao wataomba kiongozi wao (wa ukoo) atambulike na apate nafasi huko serikalini"

"Mwalimu Nyerere alikataa jambo hili (uchifu), lina faida gani. Uchifu unataka kutuibulia zile hisia kwamba tuna ukabila kama hakuna wazee wataliona hili jambo, basi mawe yataona"

"Nchi yetu ina wakristo na waislamu, ikitokea mvua imechelewa kiongozi wa serikali huwa anawaomba wakristo kanisani wakaombe na waislamu msikitini wakaombe mvue zinyeshe, lakini huwezi kusikia kiongozi wa serikali akiwaomba washirikina eti wafanye namna mvua inyeshe"

"Kwenye shughuli za serikali ushawahi kuona tunawaita wanaoabudu miti waje kuomba kabla ya shughuli? sasa uchifu wa nini?. Hawa machifu walishafutwa kisheria, tunapowarudisha tunapanda nini?"

"Nenda pale Kilimanjaro, utasema Mareale ndio chifu wao, hapana wako wengi. Kwa hiyo nao wafanye uchaguzi kisha waje kumpata chifu wao wa wote. Kweli tunaenda hivi katika maendeleo"

View attachment 2104792
Kwenye hili naunga mkono hoja!
Hakuna umhimu wa uchifu
 
Hivi ile TV yake usharudi?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Polepole bado ana hasira kifo cha jiwe. Yupo kwenye psychology transition. Hakujiandaa kisaikolojia mabadiriko ya ghafla. Alidhani Jiwe ataishi kila leo.
 
Kuna wakati alikuwa anahojiwa akasema kwenye siasa kuna mambo mengi na uadui mwingi, fitna, na hata kuuana pia akaulizwa na uchawi akasema upo sana na mimi niko vizuri

Naomba mfukue hilo kaburi maana hawa mwafrika kumbukumbu yake ni kama squirrels [emoji883] anafukia chakula halafu anasahau alipoweka au kama ni mbegu inaota
 
No hata kama si kiwa ni yeye pekee lakini kama taifa tumempa hadhi ya kuwa baba wa taifa letu. So msingi wa taifa letu ni ule aliouasisi na ndiyo rederence pekee tuliyonayo so far kwa nchi yetu
Kwa 24Yrs alifanya nini cha maana?
 
Kati hili niko na Andunje uchifu ni laana,uchifu ni ushirikina,uchifu ni matambiko,uchifu ni ukoloni,uchifu ni ukabila.

Taifa likizama katika uchifu maana yake ukabila umerejea kwa kasi Tanganyika.Muasisi wake atakimbilia Mwembekiuno na kutuachia majanga.
 
Humphrey Polepole amesema kuwa

"Mambo ya Machifu yanatusaidia nini kama taifa?nasema jambo hili sio jema,naliona linadhoofisha Utanzania wetu,likiendelea bila kukemewa litaibua tuliyoyazika ya hisia za ukabila, usisi na uwao, Mwalimu Nyerere aliona mbali kukataa haya mambo kwani yataligawa taifa"

"Yapo maeneo uchifu ulishaondoka,haupo. Tulishakubaliana uchifu ni ukoo wenu, mna kiongozi wa ukoo mnazungumza mambo yenu binafsi ya kifamilia leo serikali ikizungumzia uchifu hawa nao wataomba kiongozi wao (wa ukoo) atambulike na apate nafasi huko serikalini"

"Mwalimu Nyerere alikataa jambo hili (uchifu), lina faida gani. Uchifu unataka kutuibulia zile hisia kwamba tuna ukabila kama hakuna wazee wataliona hili jambo, basi mawe yataona"

"Nchi yetu ina wakristo na waislamu, ikitokea mvua imechelewa kiongozi wa serikali huwa anawaomba wakristo kanisani wakaombe na waislamu msikitini wakaombe mvue zinyeshe, lakini huwezi kusikia kiongozi wa serikali akiwaomba washirikina eti wafanye namna mvua inyeshe"

"Kwenye shughuli za serikali ushawahi kuona tunawaita wanaoabudu miti waje kuomba kabla ya shughuli? sasa uchifu wa nini?. Hawa machifu walishafutwa kisheria, tunapowarudisha tunapanda nini?"

"Nenda pale Kilimanjaro, utasema Mareale ndio chifu wao, hapana wako wengi. Kwa hiyo nao wafanye uchaguzi kisha waje kumpata chifu wao wa wote. Kweli tunaenda hivi katika maendeleo"

View attachment 2104792
Mh Polepole nadhani kuna vitu anakosea sana. Yeye alipaswa ajikite kwenye kuelimisha mambo ya uongozi. Yaani kageuka mwanasiasa tena kwenye hiyo shule ya uongozi, I think he is not acting rationally. Mfano suala la Machief siyo la kubeza mbona hata Mkapa, Nyerere, Mwingi na Dkt Magufuli wote hata JK walishawahi fanyiwa hivyo vitu iweje kwa Mama iwe Nongwa??? Nampenda Polepole kwa ile dhana ya uzalendo ila naona ni kama ni mtu wa kuattack personality za watu badala ya kujenga hoja.
 
Mwisho wa siku mambo ya chifu sijui uchifu ni takataka...hebu angalia comment ya yule mzee kuhusu mauaji....sasa upumbavu wa namna hii ndio nini?....hawa wazee ni washirikina PERIOD.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom