Humphrey Polepole naye atatungiwa msamiati kama alivyotungiwa Gwajima?

Humphrey Polepole naye atatungiwa msamiati kama alivyotungiwa Gwajima?

Muda huu kuna kitu kimemkaa kooni, atakuwa kishaagiza tukio lolote la ghafla lifanyike, apate kutema ngongo yake.

Kuna watu unawateuwa kumbe ni nyoka wa vichwa viwili, kimoja kinapuliza, kingine kinakuuma. Na kama kuna mnafiki mwingine atoke tena siyo polepole, atoke haraka mimi niko imara. Najaribu kuwaza tu 😅😅😅
Una akili kama Nyerere alisikika Babu wa Kishumundu akisema 🤣🤣
 
Yesu Anakuja haya mambo ni ya kisiasa ambayo yanaleta maswali mengi kuliko majibu yake
1- Hivi ni makanisa mangapi yamefungwa Tanzania? Na ni nini sababu ya kufungwa hizo nyumba za ibada?
hayafikirishi tu, yanaumiza moyo. makanisa yaliyofungwa ni zaidi ya 2000 (alfu mbili). kama haujui, kanisa la ufufuo na uzima limesambaa nchi nzima, kwa Tanzania kuna makanisa yaliyojengwa ambayo waumini kila jumapili wanaenda kusali yapo zaidi ya alfu mbili. hao hawaongei chochote kuhusiana na siasa, na wengine hata hawajui gwajima ameongea nini kwa sababu wapo remote huko.

sababu ya kufungia makanisa haya ni kwa sababu gwajima alikosoa utekaji na uuaji. basi tuseme gwajima alikosea kama kweli alikosea, sawa kosa la gwajima ndio waadhibiwe waumini? katiba ya nchi hii inasema tunao uhuru wa kuabudu, kwa hiyo uhuru wangu wa kuabudu ufutwe kwa kosa ambalo sio la kwangu,ni la gwajima? watu wanapigwa virungu,wanapigwa mabom kwa sababu wanataka kuabudu na wanazuiwa. tunaposema makanisa zaidi ya 2000 yamefungwa, ni pale walipofuta usajili wote, hivyo na majengo zaidi ya 2000 ya makanisa hayo hawaruhusiwi kuabudu hadi jana wameenda kukodi ukumbi walau wapate nafasi ya kumwabudu Mungu. kwa nini raia wa Tanzania wapate shida hii kwa kosa la mtu mmoja? ni rais wa nchi gani au mahakama au katiba au sheria gani inaadhibu raia wengi kwa kosa la mtu mmoja? kama gwajima amekosea kwa nini mshimshitaki na kumshughulikia yeye badala ya kuumiza waumini wake wengi ambao hawajaongea chochote na wengine inawezekana hawaungi mkono alichosema?

ili kujisafisha uonekane wewe unapenda wakristo, unaenda kwa mwamposa kama gelesha, nani mrahisi hivyo kudanganyika? tunataka haki ya kuabudu, gwajima mtajuana naye ninyi mnamalizana vipi, though najua Mungu atajibu maombi na atamtetea.
 
Polepole ndio Mwendo
Kwa sasa naona mwendo wa polepole umenza kuongeza kasi hapa Tanganyika- Oktoba imekaribia sana. Sijui nini kitatokea hapa kati kabla ya Oktoba- Mungu ajua Inaonekana mambo ni mengi yaliyo nyuma ya pazia na muda uliosalia ni mfupi sana! Tuendelee kumwomba Mungu ili yajayo yasije yakawa ni ya kusikitisha na kuumiza miyoyo ya Watanzania.
Mungu ibariki Tanzania 🇹🇿
 
Hana uwezo hata kuwa Rais wa Zanzibar! Sasa kwa nn awe Rais wa Tanganyika?
Ule urais ulimdondokea kwa bahati mbaya tu sasa kwa nn anataka na awamu ya pili?
Kama hawezi kuwa hata Rais huko kwao alikotoka kwa nn awe Rais huku kwetu? NAUMIA SANA MIMI
Endelea kuteseka mpaka 2030..
 
Tundu Lissu alipachikwa title ya Makulukhutabu. Kule Kizimkazi makulukhutabu ni mtu ambaye hapendi amani bali ni mtu wa shari na mpenda heka heka. Sawa na yule simba asiyetulia aliyekutwa kwenye zoo sijui wapi akapachikwa jina la Tundu Lissu.

Gwajima - Gwajimanized. Mtumishi wa shetani!

Polepole - .......

Ila Mama dah! Hata Mama mkwe wa Diamond akasome kwa michambo 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom