Humphrey Polepole, ndugu zako wanasiasa wenye chuki na wewe pamoja na wataalamu wa Afya wanasema kuingiza dawa ambazo hazijasajiliwa nchini ni ndoto

Yeye atupe tu sisi binafsi wenye kuhitaji watakitafutia. Hata kuleta hii information tu ni faida kwetu.
 
Huyu mtaalam anasema dawa haziwezi kuingia nchini, mpaka zifanyiwe utafiti na wataalamu wa Tanzania. Je, wataalamu wa Cuba na wa Tanzania ni wataalamu wapi wapo juu kitaalum? Obviously jibu ni wa Cuba. Aidha niongeze tu kuwa Cuba kuna mabingwa wa udaktari wengi sana. Na ni wa viwango vikubwa. Nakumbuka wakati wa Vita na Idd Amin miaka ya 1978/79 madaktari wa Cuba walifika kwenye uwanja wa mapambano outta huduma ya tiba kwa askari wa ki Tanzania . Pia, niongeze kwa kumpongeza baloz polepole kwa Kaz nzuri anayofanya kama baloz. Yaan anawaonyesha viongoz wetu kwamba baloz anatakiwa afanye nn. Sio hawa ma baloz wa vimemo wanaokwenda Kumar na kustarehe. Nakumbuka Baloz Polepole alipokuwa Malawi aliwaletea Chuo Kikuu Huria dili la kufundisha ki Swahili. Huyu akipelekwa Italia au France au UK atawaletea wazazi dili la watoto kwenda kwenye academy za ulaya. Ni so innovative guy. Chaos.
 
Duh...!. Wabongo kwa husda, fitna na majungu.
Nimemsikia Balozi Polepole, amesisitiza utaratibu utafuatwa.
P
Ila Paulo kwani hujasikia kwamba WHO wamekataa kusajili dawa zao nyingi? Nchi haiwezi kujiingiza kwenye huo utaratibu, ambacho kinhmgefanyika kama viongozi wetu wanatumia akili hilo swala lingekuwa la ki intelligencia kisha likaratibiwa ki informal na serikali na ikafanywa as if watu binafsi ndiyo wanaohusika na siyo serikali. Tatizo ni huo wivu wa wabongo na roho mbaya yetu watu weusi tusiojipenda.

Hata wangewaunganisha na traditional medicine basi ikafanywa kama tiba ya asili bila ku raise voice za kisiasa kama hivi.
 
Mkuu Ame, WHO ni mabeberu, wanatoa ithbati kwa madawa ya ulaya tuu!, nchi nyingi zilitengeneza dawa za covid, lakini WHO walizigomea because its a big business!.

Cuba is more advanced kwenye medicine kuliko Marekani!. China is most advanced kwenye traditional medicine na clinics za CTM zimetapakaa dunia nzima, WHO hawazitambui lakini hata hapa zipo, wataalam wetu hawana uwezo wowote wa kufanya clinical test. Leo ndio hawa madaktari wetu mburu matata wagomee dawa kutoka Cuba kwasababu hazijapata ithbati ya WHO!.
Huu ni ujinga!. South Afrika wametengeneza HIV vaccine, WHO, wameigomea, wanawajibu watu wao wanapona hiv, who the hell is WHO?!
P
 
Ukisikiliza maelezo ya Polepole kwenye clip inayozunguka mtandao inaacha maswali kadhaa:-

1. Kulikuwa na sababu gani ya yeye kuja hadharani? Yeye kama balozi ameshindwa kabisa kupata takwimu za watu wenye changamoto hizo kutoka wizara ya afya na maeneo wanakopatikana hadi atumie mitandao ya kijamii kuwatafuta?? Huo ndo utaratibu wa serikali wa kufanya kazi?

2. Kwa hoja zako anaweza kukosa uungwaji mkono wa wizara kwasababu hili jambo anataka kulifanya kibnafsi na sio kiserikali. Yeye kama balozi kazi yake ilikuwa kutafuta fursa na kuishawishi wizara ya afya kuchangamkia fursa

3. Tuseme ameileta hiyo fursa serikalini/ wizara ya afya wakaipiga danadana au waka reject kabisa. Kama aliona option ni kuwashirikisha hospitali binafsi bado hakuwa na sababu ya kuja kwenye mitandao! Angeweza kutumia mifumo iliyopo huko huko hospitali binafsi halafu wakatumia mifumo yao kuingiza hizo dawa nchini na kufikisha taarifa kwa wenyechangamoto. Yeye kuja public anaweza kuwachonganisha na mamlaka husika kama kweli wame ignore hoja zake kama unavyohisi

PolePole ni mchapa kazi lakini pia anapenda sana kuonekana. Wakati mwingine unatakiwa kupiga kazi halafu una maintain low profile hasa kama umenusa hali ya mizengwe kwenye unachotaka kufanya wakati wewe unaamini kinamanufaa
 
Sasa hapa kama hoja ni serikali kukataa kujiingiza kwenye biashara ya dawa ambazo WHO hawapendezwi nazo, aliyekosea ni PolePole! Kwa yeye kuja public na kutaja moja ya hospitali huoni atawafanya hao waanze kufuatilia kimya kimya? Kumbuka balozi ni sehemu ya serikali

Kama ameona kuna walakini alitakiwa avishawishi vyombo vya kiitelejensia nyuma ya pazia viwasaidie watu binafsi kupata hizo dawa, sio yeye kuja public

Tunafahamu WHO ni ya mabepari na cuba ina mlengo wa kijamaa kamwe hawawezi kuiva hasa kwenye ishu kubwa kama biashara ya dawa ambayo kila bepari anaitolea macho

Story za vijiweni zinasema kuwa hata corona imeisha kwasababu wakubwa walianza kugombania soko la chanjo. Kila mmoja aligundua chanjo yake na akataka WHO aidhinishe, ikatumika hekima kama ile ya "Berlin conference" ikabidi ugonjwa upishe kwanza malumbano

Dawa ni siraha na biashara kubwa sana, ni vizuri zingetumika mbinu za medani kusaidia wahitaji kuliko kuingiza siasa
 
Nakubaliana na wewe. Hii ya kuja public kweli hata Mimi sikumwelewa kusudi lake ni lipi...
 
Kwa nini Polepole anataka atumiwe majina ya wagonjwa??
Nyie ndio watu mnaojifikiria nyinyi tu badala ya kuwafikiria maelfu ya wananchi ambao wanateseka na maradhi ambayo hayana tiba nchini. Pole pole kwa maono yake anataka kuwasaidia wananchi hao na ndio maana anataka majina yao ili idadi Yao ifahamike. Idadi Yao ikifahamika itakuwa rahisi kujua kiasi cha dawa kinachoweza kuletwa nchini ; dawa zikiletwa itakuwa rahisi kuwasiliana na wagonjwa ambao majina yao yameorodheshwa.
Ikumbukwe kwamba hao waganga wanaotaka kuhujumu huu mpango wa dawa kutoka CUBA ni wale waliosomeshwa Kufuata ya western countries ambao hawataki kusikia kuwa nchi ya Cuba ina ubingwa wa kutibu kuliko mabwana zao wa America na Uingereza. Hao hao mabwana zao kutoka Ulaya na America wanazunguka kwa watindiga na wamasai wakitafuta madawa ya asili ambayo wanakwenda kuyafanyia utafiti na kuyauza as supplements!!
Mama Abdul ni lazima aje openly kuunga mkono initiative hii kwani wananchi wengi wa Visiwani wakiwemo ndugu zake wa karibu na viongozi wa Serikali wanasumbuliwa na maradhi ambayo dawa hizi zitawasaidia!!
 
Nakubaliana na wewe. Hii ya kuja public kweli hata Mimi sikumwelewa kusudi lake ni lipi...
Kuja public kusudi lake ni kuona wananchi wa chini wanafahamu uwepo wa dawa hizi ili nao wafaidike!! Ama sivyo mafisadi wataingilia kati na walengwa wa Polepole hawatafaidika!!
Serikali haina sababu ya kuingilia na kuweka vikwazo ; waache dawa ziingie na wananchi wazijaribu kama zinafanya kazi na kuwasaidia wananchi. Kama hazitafanya kazi biashara itakufa naturally!
 
Kwani WHO wanakataza kutumia dawa za kienyeji hapa Tanzania? Au kufuatana na mabwana zao wa Marekani WHO are part of the enforcement of the embargo on CUBA! Hapana kuingiza Siasa kwenye afya ya wananchi waache dawa zije!! Kwani WHO waliwakaza kunywa kikombe cha BABU?
 
Pamoja na kazi nzuri ya Polepole, lazima sheria, kanuni na taratibu zinazohusu uingizaji dawa zifuatwe.
Dawa zaweza kusababisha madhara zaidi ya kutibu, hivyo weledi unahitajika na siyo siasa.
Mnatamani tusinywe mitishamba!!! Kwa staili hii. Chanjo ya COVID mlifanya clinical trials lini?
 
2. Kwa hoja zako anaweza kukosa uungwaji mkono wa wizara kwasababu hili jambo anataka kulifanya kibnafsi na sio kiserikali. Yeye kama balozi kazi yake ilikuwa kutafuta fursa na kuishawishi wizara ya afya kuchangamkia fursa
Kuna Balozi alikuwa China Kila mara akawa anakuja front/ mitandaoni kutangaza furusa zilipo China kuanzia Mihogo mpaka nafaka. Naye alikuwa anafanya ubinafsi?

Mpoje ninyi? Dawa inauzwa laki 9 wakati mtu kagundua chimbo la dawa ya laki na hamsini, Wewe unamuona mgudua chimbo anazingua?

Kwanza Kuna uwezekano, hao Big Pharma watakuwa wananunua dawa hizo kutoka Cuba kisha wanazirepackage kisha kutuuzia laki 9!!! Hawashindwi kwa jeuri walioyonayo ya kuthamini fedha kuliko utu!
 
Tatizo mnataka kuiondoa ccm mkiwa hamna mbadala wa ccm.

Wale wengine bado hawako serious! wao kwa wao hawaelewani sababu ya tamaa za madaraka!
 
Akina nani wanafanya kazi pasipo kutajeti Vyeo?
 
Ni lini polepole amekuwa mtaalamu wa afya? Jamaa ni mbabaishaji sana.
 
Polepole hafai kuendelea kuwa balozi.
 
Hivi zile juice alizofuataga muokotwa jalalani
Hivi zile juice alizofuataga muokotwa jalalani kwa ndege yetu kule Madagascar ziliishia wapi mkuu?
Maana promo yake ilikuwa baabu kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…