Humphrey Polepole, ndugu zako wanasiasa wenye chuki na wewe pamoja na wataalamu wa Afya wanasema kuingiza dawa ambazo hazijasajiliwa nchini ni ndoto

Kwa nini Polepole anataka atumiwe majina ya wagonjwa??
Huyo jamaa ni tapeli sana, anashindwa nini yeye kuratibu hiyo zoezi kupitia Wizara ya Afya?! Anatumika vibaya na waCuba. Utaratibu wa kuingiza Dawa nchini unajulikana na Sheria zipo lakini Polepole hataki kufuata Sheria ya nchi. Kama upo ulazima wa kuingiza hizo Dawa ambazo hazijasajiliwa nchini Serikali ndo ina uwezo wa kuingiza kwa njia ya dharura lakini siyo kama anavyofanya huyo Balozi.
Hivi Kiongozi anayevunja Sheria za nchi ni wa nini?! Hivi majukumu ya msingi ya Balozi ndiyo hayo kweli?
 
Acheni kuaminishwa porojo za kijuha,
Cuba haifiki hata robo kwa Ulaya na USA katika matibabu ya afya. Umaskini tu ndio unawatufanya kuhangaika na Cuba.

Ulaya na Marekani ndio kitovu cha ugunduzi wa dawa, chanjo na teknolojia za kila aina za kisasa katika matibabu duniani.
 
Hizo dawa za Cuba zifuate utaratibu kama vile dawa nyingine zote mfano zinazotoka India na Ulaya zinavyofuata utaratibu kuuzwa nchini. Litakuwa taifa la kijuha na la kienyeji sana kuingiza tu dawa kwa kusikiliza maneno ya mtu au wawili watatu. Hamjachoka tu na utapeli wa kikombe cha babu na dawa za Madagascar alizokuwa anagawa Rais mwenyewe ambapo hadi ndege ilitumwa kuzichukua?!
 
Watu wenye ufahamu kama wako ndio wanakwamisha maendeleo ya nchi; Polepole katimiza wajibu wake. Hospitali ya Kairuki umejiridhisha kwamba kuna tatizo na wenye matatizo wameelekezwa kuwasiliana na hospital ya Kairuki. Ninyi mnaojiona lazima mshirikishwe endeleeni kusoma sheria na taratibu.

Wagonjwa hawana shida na sheria wana shida na kupona maumivu na makovu yanayowasumbua. Nilitoa mfano wakati wa kikombe cha babu wanasiasa na wanasheria wote waliekea kwa babu na hakukuwa na pingamizi.

Wakati mnajiandaa kufuata sheria wapo watanzania tayari wana tiketi za kwenda Cuba kupata matibabu
 
Upo sawa, ndiyo maana nikasema Wizara inashindwa nini kuagiza hiyo Dawa kwa njia ya dharura kama ulazima upo? Ninachoona hospitali binafsi zinataka kutelezea humo kwa Balozi kupindisha utaratibu wa nchi for his own interest.
 
Huyo lofa wako anatafuta cheap popularity. Atulize tako afanye kazi ya ubalozi. Kila jambo lina taratibu zake aache utoto. Polepole hajawahi kuwa na akili hafai kuwa kiongozi mkubwa. Enzi za kichaa mwenzake alikuwa anawapigia mawaziri na watendaji wa serikali saa 5 usiku eti kutatua matatizo ya wananchi. Hajui kuna muda wa kazi? Amejaa sifa za kijinga, ana IQ ndogo km Bashite.
 
Upo sawa, ndiyo maana nikasema Wizara inashindwa nini kuagiza hiyo Dawa kwa njia ya dharura kama ulazima upo? Ninachoona hospitali binafsi zinataka kutelezea humo kwa Balozi kupindisha utaratibu wa nchi for his own interest.
Wizara ina utaratibu wake wa kufanya kazi, inajua mahitaji yake siyo atokee mpumbavu moja kwa maslahi yake aanze kutumia mitandao kuwa anataka kuleta dawa. Pole×2 hakuwahi kuwa na akili, alikuwa hata hajui majukumu ya mwenezi wa chama. CCM sijui inamchekea wa nini arudishwe nyumbani.
 
Narudia tena zengwe na zengwe za dawa hizo hazijaanza leo wala jana
Nyie endeleeni kuleta mihemuko

Ova
 
Mimi kiuweli huyu Polepole ananishangaza sana. Hizo Sheria na Kanuni tumeziweka za nini kama hatuwezi kuheshimu?! Eneo sensitive kama la afya siyo ya kucompromise kirahisi namna hii. Tuna Wizara husika na Idara zake, nini kinashindikana yeye kupitia huko?! Balozi unabagaza Wizara ya Serikali yako?! Kweli?

Huyu ni Balozi wa hovyo kuweza kutokea Tanzania.
 
Pamoja na kazi nzuri ya Polepole, lazima sheria, kanuni na taratibu zinazohusu uingizaji dawa zifuatwe.
Dawa zaweza kusababisha madhara zaidi ya kutibu, hivyo weledi unahitajika na siyo siasa.
Huko ndio afrika utaijua vizuri kwenye taratibu na sheria.
 
Adui mkubwa wa taifa hili ni CCM
 
Hivi zile juice alizofuataga muokotwa jalalani

Hivi zile juice alizofuataga muokotwa jalalani kwa ndege yetu kule Madagascar ziliishia wapi mkuu?
Maana promo yake ilikuwa baabu kubwa.
Lakini si zilikuja? Sasa hizi za Cuba mnazbania kwanini? Kwavile zinampandisha Chati Pole pole au mnataka kujipendekeza kwa Marekani kuwa nyinyi nanyi mnawawekea embargo Cuba? Acheni ujinga huo ; Rais wenu mstaafu “Kamando” pengine angewahi kupata dawa hizo saa hizi angekuwa anaona!!
 
Polepole ni kati ya watu wajinga ambao huwa wanaona Tanzania ni mali binafsi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…