Humphrey Polepole ni miongoni mwa Viongozi wa awamu ya 5 walioua Demokrasia ndani na Nje ya CCM

Huna hoja basi , na ikiwa ni hivyo tupishe wewe nenda kwenye nyuzi unazoziweza , huu mwezi wote tunawaanika mamluki wote wa Jiwe , sasa si utajinyonga mkuu !
 
Ukweli usemwe
 
Ile biashara ya manunuzi ilikuwa aibu tupu kwa Ccm
 
johnthebaptist nawewe ulikuwa mshirika mkubwa wa kuua demokrasia. Mlishabikia UOVU/UUAJI/UTEKAJI/ DHULUMA KWA UJUMLA ya magufuli
 
Erthrocite umeeleza ukweli ambao mtu mzima yeyote ameushuhudia na bado anaukumbuka.

Atayejisahaulisha, ujue ana agenda nyingine.

Hapa ni kama unatuweka sawa kwa kumbu kumbu.

Huyo Polepole ndiye aliyeanzisha kibwagizo cha majigambo ya 'viete (V8 model Land cruiser) na hakujificha wasifu wake katika soko la kununua wapinzani huku akichekelea kwa kubinya jicho lake moja kama anakonyeza.
 
Kweli iko wapi una kiongozi muda wowote atatembelea mkongojo kwenye kiti hataki kuachia na pia amedhulumu waandishi na bado amekwenda mahakamani alipwe gharama za kesi umeshindwa kumwambia ukweli!
Hili nalo neno, mleta hoja akaliangalie na kulijibia.
 
Naam
 
Nje ya mada
Lipo ndani ya mada bhana.
Hii topic umeanzisha, yaweza kubeba title ya: ' hali ya kidemokrasia nchini kwa kipindi cha muongo mmoja'.

Halafu anapoguswa Mbowe usikae kushituka shituka kama mtoto mwenye malaria kali.

Ukitaka kueleweka vizuri na mada iwe tamu, yajibu yote unayoulizwa na hadhira, maana yanahusiana na umangimeza wa viongozi wa vyama pamoja na Serikali.

Usiwe biased.
 
Nyuzi za Mbowe zimejazana humu na huko tumeulizwa maswali haya haya , tena na watu walewale na tukajibu vizuri sana , sasa hatuwezi kurudia mambo yale yale , tuna mambo mengi sana
 

Chadema itakuwa ngumu kufanikiwa kwa kuwa mnanyooshea watu mikono kwa kutenda ubaya fulani humu mkitaka kuaminisha watu kuwa cdm inatenda mema. Kitu ambacho sio kweli.

Mfano, unasema polepole kuwa, ameua democracy. Lakin, upande wa pili mwenyekiti wa chama chenu, amekuwa mwenyekiti kwa miaka nenda rudi.Yaan yeye, hana mbadala.

Sasa, kati ya Mbowe na Polepole nani ameua democracy? Hata mtoto mdogo atasema ni Mbowe. Tanzania hii, hivi vyama vyenu Kushida dola ni ngumu.

Kwa kuwa mnatumia uongo na nguvu kuchafua watu lakin nyie ndio wachafu kabisa. Chama cha kuitoa CCM bado hakijazaliwa. Waliopo ni wahuni wahuni tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…