Hujasema bado!
Hujasema Hujasema bado.
Mada yako Mkuu ingawa inavutia, ni unalazimisha lazimisha tu. Yaani hujasema bado.
Unamchafua Balozi wakati hujaweka ushahidi wowote ule zaidi ya kuleta tetesi(kulazimisha) badala ya kuweka uthibitisho ulio thabiti.
Balozi 'Comrade Polepole' anashutumiwa na Erythrocyte na CHADEMA kujihusisha na vitendo visivyo vya kidemokrasia (Ni muuaji), lakini hakuna uwiano(correlation) wa moja kwa moja uliowekwa kati ya hatua alizochukua(kununua wapinzani) na matokeo yake(kufa kwa Demokrasia nchini).
Kwa mfano ametaka kuunganisha(correlate) matumizi ya Vikosi vya Usalama vya Serikali kana Uuaji wa Demokrasia.
Huyu bwana anajiondoa ufahamu tu, anasahau kuwa Balozi Polepole akiwa kama mtumishi wa chama na serikali, utaratibu wa kutumia vikosi hivyo ni vya kawaida haswa ukizingatia majukumu ya vikosi hivyo ni kudumisha utulivu na usalama wa viongozi, yani haipaswi kuunganishwa na "vitisho" bila ya kuweka muktadha sahihi.
Ni shutuma mbaya sana unayoweza Kumtolea/ kuwatolea Polisi au Amri Jeshi Mkuu.
Ieleweke, michakato ya kisiasa mara nyingi inahusisha mazungumzo na maelewano, yaani "Political maneuvaring" utaona kama alivyoelezea kuhusu picha aliyoambatanisha, ambayo ameelezea kuwa 'Mbunge alikuwa akinunuliwa' wakati, kwa uhakika hiyo ni sehemu ya mazungumzo ya kidemokrasia(hakuna siri hapo) Ati kulikuwa na Makubaliano ya siri na wahamaji-hiyo ni mambo jambo tu na hayana uthibitisho. Hiyo ni picha ya siri?
Wakuu, katika demokrasia inayofanya kazi, wadau mbalimbali, wakiwemo wanachama wa upinzani, wa itikadi mablimbali, wana haki ya kubadili chama cha siasa iwapo mitazamo inaendana na maslahi au malengo ya sera ya wapiga kura wao.
Mifano ni mingi tu. Mh. Membe(R.I.P) ACT, Mh. Lowassa(R.I.P) CHADEMA na hata huko Ulaya(tunapofundishwa demokrasia) haya yanatokea. Hao walikuwa 'Wahamaji'
Kuhusu kunuliwa kwa mamilioni ya hela-TShs 600 milioni iliyotajwa, mbona hii inaweza kuwa sehemu ya "legal political funding" ama "Campaign financing" ikiwa ina maana hakuna sheria yeyote ile iliyovunjwa. Na ni kitu ambacho, pia, ni kawaida duniani/ulimwenguni mwa siasa.
Mtaona humu hakuna sheria yeyote ile iliyonukuliwa kwamba ndio iliyovunjwa na kitita cha Tsh 600milioni- just-a-jest, wanasahau zao za TShs 2.7billioni-zaidi ya kusema "Katiba ya CCM ilivunjwa"😅🤔
Sasa basi, bila ya ushahidi wa wazi wa quid pro quo au kuvunjwa kwa sheria au uharamu, hiyo haiwezi kuchukuliwa kuwa ni Ufisadi, sembuse "kuuliwa kwa demokrasia"
Saa za daku hizi, nimalizie, Taswira ya kwamba Viongozi wakuu wastaafu kuwa waliongozwa kwa woga ni dhana inayodhoofisha utukutu, uzoefu na michango yao kwa Taifa
...kwamba uungaji mkono wao kwa kile kinachojulikana kama 'Juhudi'
unatokana na imani zao za kweli na za dhati kwa Hayat Rais J.P Magufuli katika sifa zake au wazungu wanasema "strategic political alignment" kwa upande mwingine.
Ni nani hapa ambaye hakuwasikia wastaafu Msibani? Walinena uwoga?
Nani hakuwaona wastaafu Ikulu? Kweli hao(katika picha) walikuwa wana woga?
...ingawa mada hii inaibua hisia kali, jazba na wasiwasi juu ya uwezekano wa matumizi mabaya ya madaraka, uuwaji wa demokrasia n.k, ni muhimu kupiga jicho la utatu tuhuma hizi za Erythrocyte na CHADEMA kwa jicho la kukosoa na kudai uthibitisho wa kina kabla ya kufikia hitimisho kuhusu hali ya demokrasia nchini.
Aluta Continua.
Magulification must go on.
Amani ikutawale.