Humphrey Polepole ni nani?

Humphrey Polepole ni nani?

Duh Dr Majipu ana roho ngumu kweli kweli ina maana katika teuzi za wakuu wa mikoa hakuwepo.Basi hata ubalozi wasimsahau aisee kweli siasa sihasa.
 
Nini Maoni Yako Kuhusu Huyu Mchambuzi!

Ni chuki tu za kibinafsi (Personal Issues) zaidi , POLE POLE Ni kijana SAFI SANA mwenye uwelewa mpana sana, ana sifa zoote za kuwa kiongozi safi na mwenye msimamo , anashambuliwa na vijana kama yaliyompata mhe Mwiguru nchemba, Paul Makonda n.k , asihofie hilo hata kidogo, siku zote huwezi pendwa na wote , je ni vijana wangapi waliojitosa kwa msimamo kama hao ? ni swala la ushabiki vs wachezaji uwanjani, HAKIKA kwngu mm nashangaa kwa nini hadi sasa hajakumbukwa ? hao wanaomshambulia kwa vijembe kwani yeye amewazuia ? waingie uwanjani tuwaone basi then tuta - compare. HONGERA SANA HAMPHREY POLE POLE (niliwahi tangaza humu zawadi yako hukujitokeza)
 
swali lako ndilo swali swali langu!!.Mimi nimejua nitakutana na picha ya mtu ambaye Pole pole anatakiwa kutoa maoni juu yake,kumbe chenga tu.MCC imewavuruga watu vibayaaaa
Kama ni maoni ya MCC mbona kuna uzi aliutoa humu jana? Fuatilia utaupata na utapenda uusome zaidi ya mara moja!
 
Ndumila kuwili wa kutupwa siku zote anaangalia mkate wake utapakwa siagi na nani
 
cjawahi kumpuuza polepole ata pale tunapotofautiana kimtizamo ni mtu mwenye maono na asiyemnyenyekea yeyote huwa anatoa msimamo wake bila kujali ni wangapi watamuunga mkono
 
Hana lolote,ni mnafiki tu anaepalilia kupata ugali kwa kujionyesha mzalendo,bahati mbaya Magu bado hajamuona,namshauri asikate tamaa,ipo siku ataonekana macho mwa Jpm
 
Polepole mungu akupe maisha marefu wenzako kina baregu wamekwa mifukoni na mafisadi hawa uhuru tena
 
mie mwenyewe nashangaa kina Mwesiga baregu kukaa kimya
Ukistaajabu ya Musa....nami nashangaa watu kustajaabu ya aliyekuwa RC Moro Dkt. Rajab na kumwacha mtu kama Prof. Baregu ambaye alipewa jukumu la kitaifa(katiba mpya) lakini haijulikan alichofanya.
 
Humphrey Polepole, mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Katiba amekuwa mstari wa mbele kutoa maelezo, ufafanuzi na kukabiliana kwa hoja na Wapinzani wa rasimu katiba iliyowasilishwa.

Kipekee nampongeza sana kwani tume ilikuwa na wajumbe wengi lakini wengine wako kimya ila Bwana Polepole amekabiliana nao na anaendelea kukabiliana nao dhidi ya upotoshaji, kwangu mimi Bw Polepole anastahili tunzo ya heshima.

Nawakaribisha wadau kwa maoni.

kinara wa kuitetea ccm, sasa kazawadiwa u dc

hongera polepole, polepole utapata u rc

u dance very well ccm tune
 
Nimekuwa nikiona mijadala mingi hasa Chanel ten ikimhusisha huyu mtu hivi ana cheo gani serikalini, au kwenye chama cha mapinduzi ana cheo gani maana kuna uhusika anauvaa kana kwamba ana cheo kikubwa serikalini hasa cha msemaji wa serikali au chama.
Vilevile huyo kijana /mzee ana elimu gani? Je, elimu yake hakuna mtanzania aliyenayo? Maana naona kuna mijadala mingi sana anapotosha mambo kwa kujifanya mjuaji sana kana kwamba yeye ndio kasoma sana watanzania wengine ni vilaza wakati mambo siku hizi yapo wazi.
 
Bila kujikomba, ccm hupewi cheo..anazichanga karata mwisho utajua anacheo gani. Keep waiting
 
Nimekuwa nikiona mijadala mingi hasa Chanel ten ikimhusisha huyu mtu hivi ana cheo gani serikalini, au kwenye chama cha mapinduzi ana cheo gani maana kuna uhusika anauvaa kana kwamba ana cheo kikubwa serikalini hasa cha msemaji wa serikali au chama.
Vilevile huyo kijana /mzee ana elimu gani? Je, elimu yake hakuna mtanzania aliyenayo? Maana naona kuna mijadala mingi sana anapotosha mambo kwa kujifanya mjuaji sana kana kwamba yeye ndio kasoma sana watanzania wengine ni vilaza wakati mambo siku hizi yapo wazi.

Kwani hao Channel 10 huwa wanasema wanamwalika Humphrey Polepole akiwa kama nani?

Nafikiri suali lako lingeanzia hapo.

Channel 10 wanamwalika akiwa kama nani?

Je wanafanya hivyo kwa misingi gani?

Je wako sahihi kufanya hivyo?

Je hakuna Mtanzania mwingine ambae wanaweza kumwalika kama wewe?

Channel 10 wakijibu masuali hayo ndio sasa unahamia kwa Humphrey Polepole, je anahaki ya kualikwa, kwanini anaalikwa yeye tu?

Je anazo sifa zinazomfanya yeye aalikwe pake yake kila kipindi?

Je yeye ni mgeni maalum katika kipindi hicho?

je hakuna wageni wengine?

Anza kuwahoji Channel 10 kwanza.
 
Back
Top Bottom