Humphrey Polepole, Rais akihitaji muongee ana kwa ana Ikulu upo tayari?

Humphrey Polepole, Rais akihitaji muongee ana kwa ana Ikulu upo tayari?

Ndugu Polepole,
Salaam!

Tangu ujihuzuru nafasi ya Balozi huko Cuba umekuwa na mlolongo wa ushauri kwa Rais wa Tanzania na watanzania. Ushauri huo umefuatana na baadhi ya malalamiko ktk maeneo kadhaa, ikiwemo:-
(a). Uchaguzi ndani ya CCM;
(b). Haki za kibinadamu;
(c). Kalenda ya Uchaguzi Mkuu; na
(d). Kuunda upya uongozi wa CCM.

Kimsingi ushauri wako ni mzuri ingawa njia unazotumia kumfikishia ujumbe huenda zina kasoro kidogo.

SASA, nauliza

Rais wa Tanzania akiwa tayari kusikiliza ushauri wako mkiwa ana kwa ana ofisini Ikulu au kwenye Ofisi za CCM Makao Makuu upo tayari kufika?

Msakila Kabende
(MKULIMA)
Kakonko - Kigoma.
Umetumwa na nani? Ujumbe unafika, ndio maana baada ya kuanza kuongea, akafukuzwa rasmi kwa manufaa ya rais!
 
No, mazingira yataratibiwa vizuri - hakuna haja ya kutia hofu - kutano ni muhimu sababu kuvuana nguo hakulisaidii taifa letu
Ndugu, hawa jamaa hawana uvumilivu kabisa,
Unaposhindana kuheshimu uhai wa mtu kisa ametofautiana kimtazamo, utaaminika kwa lipi ndugu yangu?
Of course Polepole amewahi kuwa sehemu ya uongozi huu usioaminika, japo kwa sasa anajitanabahisha kuzaliwa upya. Kama anaamini kuwa na wenzake wamebadilika positively then aende at his own risk.
Waliotekwa, potezwa, uawa, bambikiwa kesi kwa kutofautiana kimtazamo na viongozi wa kipindi chake na cha sasa ni binadamu kama yeye. Hazikuwa mbuzi.
 
Umetumwa na nani? Ujumbe unafika, ndio maana baada ya kuanza kuongea, akafukuzwa rasmi kwa manufaa ya rais!
Nadhani ni vizuri mkamshauri vema - mambo haya ni mepesi sana. Rais anampenda sana HP ndiyo maana ipo haja ya kufanyika mazungumzo mezani ili kuepuka kuvuana nguo hadharani.

Aje ayajenge na mama
 
Ndugu Polepole,
Salaam!

Tangu ujihuzuru nafasi ya Balozi huko Cuba umekuwa na mlolongo wa ushauri kwa Rais wa Tanzania na watanzania. Ushauri huo umefuatana na baadhi ya malalamiko ktk maeneo kadhaa, ikiwemo:-
(a). Uchaguzi ndani ya CCM;
(b). Haki za kibinadamu;
(c). Kalenda ya Uchaguzi Mkuu; na
(d). Kuunda upya uongozi wa CCM.

Kimsingi ushauri wako ni mzuri ingawa njia unazotumia kumfikishia ujumbe huenda zina kasoro kidogo.

SASA, nauliza

Rais wa Tanzania akiwa tayari kusikiliza ushauri wako mkiwa ana kwa ana ofisini Ikulu au kwenye Ofisi za CCM Makao Makuu upo tayari kufika?

Msakila Kabende
(MKULIMA)
Kakonko - Kigoma.
Atakwambia kwani Hapa ni wapiii ?
Na huyu Mjomba Hapa ni wapiii ?!
 
Nadhani ni vizuri mkamshauri vema - mambo haya ni mepesi sana. Rais anampenda sana HP ndiyo maana ipo haja ya kufanyika mazungumzo mezani ili kuepuka kuvuana nguo hadharani.

Aje ayajenge na mama
Aje kufanya nini, mama hastahili tena kuwa rais kipi hakieleweki hapo? Na waliomuua Magu Polepole lazima awataje. Ni juu yao na wao kuwataja waliouliwa na magu. Inaonekana unaona ikulu ni mahali pa maana sana. Afuate anachoagizwa, aruhusu mchakato wa mabadiliko tuwe na uchaguzi wa kweli sio hizi chaguzi za wizi.
 
Polepole anakua live mama anaweza piga simu wakaongea na juzi vikao vya chama tulifanya online sasa waonane kufanya nini?
 
Tunahitaji Wewe Kwanza Ndio Uonane Na Polepole.....Kabla Ya Polepole Kuonana Na Mama....
 
Nimemaliza kumsikiliza pole pole naona taifa linaandaliwa vema kisaikolojia kujisimamia mwaka huu.

Nukuu za Pole pole.

1/ Mama ukichukua form na kugombea Urais utakuwa umetutukana watanzania wote.

2/Mama unataka kugombea na Salum Mwalimu wa chauma, Mama unataka kugombea na Mpina wa Act. Kweli mama unataka kugombea na hawa na moyo wako una amani kabisa?

3/ Kwani Act sisi ccm hatuijuhi? Pole pole anatufumbua macho na kututhibitishia jambo hapa kuhusu Act.

4/ Pole Pole anashauri mama amuachie Mh Lissu bila masharti aende kwenye familia yake. Kisha aitishe muafaka wa kitaifa kabla ya kuingia kwenye uchaguzi. Amesema vyombo vya dola vitajipanga kutokana na maamuzi ya wananchi ambao ndio wenye nchi. Hapa maana yake tume isituambie muda umekwisha. Kila jambo linawezekana waamuzi wa mwisho ni wananchi sio ratiba za serikali na vyombo vyake.

5/ Kuhusu Hayati magufuli sizumgumzii chochote kila mmoja ameelewa code za Pole pole.

6/ Kuhusu Ndugai na kobe wa uvvccm kupandishwa juu ya mti ili kumtukana Ndugai na kumlazimisha ajiuzulu pia sisemi.Mtu yule kutoka kundi la mtandao anayeogopeka na kutisha. Aliyekwenda Dodoma kwa Ndugai na kumwambia jiuzulu na kisha mzee akasema.Nimekosa mimi...Nimekosa sana..Nisameewe huyo naye simzungumzii.Pole pole Amesema kundi hilo linatisha sana.

Hamphrey Pole pole you made my day.

Chadema wako sawa tukatae wahuni kwanza ndipo twende kwenye uchaguzi.This is our country.

Wale mnaodharau msimamo wa chadema muwe na adabu mmeelewa sasa nchi iko wapi.

Wale mnaosema wana chadema wanamezwa na hoja za pole pole muwe na adabu.Huyu jamaa ametujengea nguvu ya mapambano leo kiasi kwamba tunaona kabisa huu ndio mwaka wa mabadiliko.

Kataa wahuni ponyesha Tanzania.
Ilitakiwa uwe uzi ankal
 
Aje kufanya nini, mama hastahili tena kuwa rais kipi hakieleweki hapo? Na waliomuua Magu Polepole lazima awataje. Ni juu yao na wao kuwataja waliouliwa na magu. Inaonekana unaona ikulu ni mahali pa maana sana. Afuate anachoagizwa, aruhusu mchakato wa mabadiliko tuwe na uchaguzi wa kweli sio hizi chaguzi za wizi.
Naona yako mengi ya kushauriana
  • Kumbuka hawa si maadui;
  • Wote wanajenga nyumba 1
 
Namba za polepole zinajulikana
Na account zake zinajulikana
Nadhali ungemuuliza kupitia huko ingeleta mantiki zaidi kuliko kuja kuziuliza IDs fake huku
Na yeye anajua ofisi zote alitakiwa aende ikulu au white house ya ccm kuliko kutumalizia mb humu.
 
Back
Top Bottom