Humphrey Polepole: Rais Magufuli hafurahishwi na mjadala wa kuongezewa miaka ya Urais kutoka 5 hadi 7

Mimi nipo hapa Kampala hivyo hii habari ni kama marudio kwani hata sisi waganda tuliwahi kuambiwa hayo

Kabisa ndio maana anamtuma pole pole ili akishabadili aseme mimi sijawahi kusema.....Ukishaona haya mambo ya atake asitake ujue ishaisha hiyo Mzee wa Chattle anabadili katiba hakuna jinsi.
 
Magufuli hataongeza muda, na kasema hili mara nyingi.

Ameshagundua kwamba urais si kitu rahisi kama alivyofikiria awali. Anaombea miaka yake ipite astaafu.

Ukitaka kutomuamini utakuwa humtendei haki.

Haya maneno ya rais kuongeza muda yalisemwa hata kwa Kikwete. Hakuimongeza.

Wapinzani wa Magufuli wanaoshupqlia habari hii wanajionesha hawana hoja.

Magufuki ana makosa mengi sana, qmbayo kashayafanya. Kuna ushahidi kwamba kayafanya.

Kwa nini mnaenda kumshupaliq kwa makosa ambayo mnafikiri atqyafanywa mwaka 2025? Licha ya yeye kuweka rekodi sawa kwamba hatafqnya makosa hayo mara kadhaa?

Mimi sikubaliani na Magufuli kwenye mambo mengi sana.

Lakini kwenye hili la kumhukumu mtu kwa kosa ambalo hajalitenda, nataka kumtetea Magufuli.

Mnamuonea buree.

Ni sawa na mtu kukujia wewe halafu kukuambia wewe uso wako umekaa kiwizi wizi, kuna hela utaiba mwaka 2025. Tukufunge mapema ili usiweze kuiba hizo hela mwaka 2025.

Utaona hukumu hiyo inayotolewa kabla hujafanya kosa kuwa ni sawa?
 
Time abd again amevunja katiba bila haya, hili la kuongeza muda halitamshinda kamwe. Hawezi akafanya atrocities hizi zote akeng'atuka
 
Kagame alisema hata ongeza muda na alipo ulizwa mara kadhaa alisisitiza hataongeza muda, kuna yule babu Museveni mwaka 2006 alisema hatogombea tena lakini bado anang'ang'ania.

Kunapokuwepo na vikwazo vya kuwazuia kugombea wanakimbilia kubadili katiba na ili waendelee kuwatawala wananchi.

Sidhani kama Magufuli atakuwa tofauti na kina Kagame na Museven.
 
Wapinzani kama wapo.....waache kuogopa hisia bali waanze maandalizi ya 2025....! Muda hauchelewi. Itafika muda chama tawala kimejiandaa kwa kuwa na candidate mwingine sahihi, upinzani hawaelewi waungane au wasiungane, hawajui nani awe mgombea, hawajui kauli mbinu ni ipi...? Ndio unafka wakati huyu anaimba ubwabwa,Huyu anasema Bata na huyu ananadi Bata Demokrasia....!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…