Humphrey Polepole: Wahuni hawatashinda, CCM ni taasisi kubwa inayoweza kupambana na wahuni.

Huyu mzee atulie nyumbani alee wajukuu kama anao. Kuendelea kuita watu wahuni ilhali yeye ndiye alikuwa kiongozi wa genge la wahuni wanunuzi wa binaadamu na wajasiliamali wa kisiasa, atafanikiwa kuwachota akili nyinyi mazuzu ! Huyu jamaa akiwa kwenye uongozi sikuwahi kusikia akikemea uhuni au unyama wowote uliotendeka zama zake anatoa wapi moral authority ya kuita wenzake wahuni?
 
inawezekana Polepole naye akawa ni mhuni..

Lakini ukweli ulio wazi, tukipambana na kutokomeza wahuni ndani ya CCM tutakuwa tumeiponya nchi mapema..
 
Umewaondoa wahuni na wewe wahuni wanakuondoa kwa vile ni baba wa wahuni.
 
mwisho wa hii vita ya chakubanga na wahuni utakua mbaya sana ccm.
Bado hujaijua ccm wewe...
Huyo polepole mwenyewe anaweza kuwa anasetiwa na ccm wenyewe,,
Hukumuona sumayi akiikanyaga katiba ya ccm hadi mkamkaribisha kamati kuu cdm? [emoji23][emoji23]
 
Kwani wewe ni mmoja wa wahuni?
Na kama sio muhuni kwa nini unabanwa na uhuni?
 
Kwa hyo hapo ugomvi NI CCM kwa CCM.
Pole pole wewe hapo NI wa kuja tu.2025 Safari inakuhusu
 
Mh. Polepole njoo huku, huyu hapa tena... spana zako si za karne hii - ati anataka mdahalo na wewe !!

 
Polepole yupo sahihi, Chama kikishakuwa na WAHUNI wengi hakiwezi kusonga mbele !! sisi wananchi tunamuunga mkono.
Polepole yuko sahihi Ccm ni taasisi kubwa jiulize lowasa na membe walishindwaje? Ndo utamwamini polepole anachosema
 
inawezekana Polepole naye akawa ni mhuni..

Lakini ukweli ulio wazi, tukipambana na kutokomeza wahuni ndani ya CCM tutakuwa tumeiponya nchi mapema..
Ni kweli, yawezekana matatizo haya ya nchi tuliyonayo yamesababishwa na WAHUNI wachache ndani ya CCM, tumuunge mkono Polepole ili tuwatokomeza.

Yeye mwenyewe kaapa kuendelea kufukiza moshi ndani ya shimo ili waibuke wengi, tayari mwingine huyu hapo kaibuka na hoja yake kwamba polepole hata nguo ya chama ya kuingilia kwenye kikao cha kuteuliwa kuwa katibu mwenezi alifanya kupewa mlangoni na Nape.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…