Humu JF kuna kasumba ya kuwa dharau wale join 2020 kuendelea

Kitu ambacho najivunia hapa Jf nimeJoin 2017 nimelikuta Jf ya ile ya moto inayompa mtu mpaka arosto .

Kusema ukweli mtu akiwa joined kuanzia 2020 na kuendelea automatically Kuna kadharau huwa sisi MaLegend kanatuingia maana kipindi hiko ni zama za simu za mikopo na IDs nyingi za hovyo kama wakina Mpwayungu waliJoin zama hizo , na lazima tujiulize ulikuwa wapi au ulikuwa wapi wakati wenzako kipindi hiko tukaitoa na kutafuta madini Jf au ulikuwa unashinda Fesibuku ukishindana kujipost ? πŸ˜‚ πŸ˜†

Anyway , japo akili haipimwi na muda wa KuJoin Jf na Kuna wakongwe wengi tu Vilaza ila , πŸ†” yako ikiwa joined chini ya 2020 Kuna kaConfidence kanaingia ndio maana loose Nut pamoja kuwa na IDs nyingi ila inamuuma mpaka Leo nilivyoizima ID yake kongwe ya Maghayo ambayo joined 2014. 🀣

Ukongwe Jf raha sometimes nanyanyasa watu unakuta namvimbia " mtu mwenyewe joined 2022 unajua nini kuhusu Jf wewe ?
 
Wakongwe brand inawabeba kumbuka hata wahuni huzeeka mkuu
 
Tunadharaulika sana bwashee πŸ˜‚

Me JF nimeanza kutumia tangu 2018 japo nilikuwa naingia kuchukua ushauri tu maana JF kila unachokiwaza humu kishawahi kuzungumziwa.

Muda wote nilikuwa naingia kama guest tu mpaka nilivyopata wito wa kuwa mchangiaji rasmi ndo nikajiunga rasmi 2023
 
Wanasema Wana πŸ†” zao zamani watumie hizo , Mimi mtu nikamdharau mwaka alijiunga halafu aniambie mambo ya ID za zamani namuona kichwani loose Nut , kutolinda ID ni kukosa umakini
 
Wanasema Wana πŸ†” zao zamani watumie hizo , Mimi mtu nikamdharau mwaka alijiunga halafu aniambie mambo ya ID za zamani namuona kichwani loose Nut , kutolinda ID ni kukosa umakini
Sembuse mke ana achwa ndio I'd? Nani asiye kujua siku unajiunga humu bwashee? Nani asiye jua chanzo cha utani wenu na mghayo ?tukisema madgo acheni ujuaji tunawajua bwashee 🀣
 
Fikiria tu kizazi cheni mna secretarybird kwa nini tusiwadharau ? πŸ˜‚πŸ€£

Enzi za Jf together party mlikuwepo ? kitambo na hicho tunakutana pamoja .

Kipindi hicho 2015 , 16 ,17 ,18 kosa vyote ila sio bando la Jf . Celebrities Kuna warumi , Chit chat Kuna show Kali kuwahi kutokea ya DJ sepetu akifanya interview na Warembo Jf , show ilikuwa πŸ”₯ watu wanajaa mpaka Dada yangu Shadeeya anaunguza mboga nyie 2020 mtatuambia Nini ? 🀣

Kuna mengi sana Jf 2020 mmekosa , hamjajui na sidhani kama yatakuja tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…