Huna changamoto za kiafya, Umefika miaka 35 huna mtoto, usingizi unautoa wapi kwamfano ?

Huna changamoto za kiafya, Umefika miaka 35 huna mtoto, usingizi unautoa wapi kwamfano ?

Mnaharibu NATURE kwa misimamo yenu ya kukalilishana ujinga, ninyi mnaozaa zaa hovyo kama panya mkiulizwa kwanini mnazaa hamna sababu ya msingi, na wengi wenu ni masikini choka mbaya, mlivyo wabinafsi mnaleta viumbe duniani ili waje kirithi mateso ya ufukara wenu huu ni unyama.

Hakuna haja ya kuwa na watoto kama hujui maana ya maisha na dhumuni la kuleta viumbe duniani.

Mnazaa kwa mazoea na bila utaratibu, ndio haya matokeo ya umasikin nchini na muendelezo wa machokoraa mitaani, kukimbia mimba+majukumu ya kulea, ukwepaji wajibu wa malezi kwa watoto.

Hakuna umuhimu wa kuwa na watoto huu ujinga wa kukalilishana umepitwa na wakati, ni muda sasa watu waamke waache kuishi kwa mazoea.

Nature ya dunia inataka uishi kwa mipaka, sheria na taratibu ambapo ili uishi na kufanya jambo lazima liwe na sababu.

Wengi humu mkiulizwa kwanini mnazaa mtasingizia sijui mpate warithi ambao hamna vya kuwarithisha, wengine wanasema walete chata duniani(upuuzi), wajinga wengine wanadai ni agizo la Mungu kuijaza dunia, sijui ni utaratibu gani mnautumia kuijaza dunia kwa kuleta viumbe msioweza kuwalea wala kuwapa maisha na maadili bora wanaishia kuwa vibaka, mashoga, wezi, majambazi, wala unga na hawa watoto wasio na heshima.

Acheni kuzaa kama wanyama, jiheshimuni.
Uzi ufungwe
 
Unataka mtt umejipanga kumlea au ndio kwenda kumtupa Kwa bibi au mashangazi mtt apate manyanyaso ya kimwili na saikolojiaa...
 
Muombe Mungu sana kwa kufanikiwa kwako maana hujui kesho yako pia waombee na hao wengine sio kwamba wameshindwa bali ni sehemu ya maisha
 
Furaha yenu ni Familia, Furaha yetu ni Pesa.
 
Kuna kina sisi ambao hatuko tu tayari kwa hayo majukumu ya uzazi na ulezi, kuwa mzazi especially kuwa mama si jambo tu la kukurupuka eti kisa una kizazi, halafu mtoa mada usijisahaulishe namna kila siku mnawatukana single mothers humu halafu hapa unasema watu wazae tu hata bila ndoa acheni unafiki nyie
 
Back
Top Bottom