Huna sababu ya kuwa baba wa kambo hasa ukiwa chini ya miaka 45

Mwenye summary plz
 
Unazungumzia jambo gani Mkuu?
Maisha mkuu:
"Maskini hali atakacho anakula apatacho;kuna wakati unajikuta umevutwa tu mahala ambapo hata wewe mwenyewe hukupatarajia, lakini ukajihisi upo salama na mwenye amani basi unaamua kutulia,sikwamba ni chaguo bali pamekufaa.basi ni ipi Busara,Hekima ama Akili kutulia mahala hapo au kuendelea kupambana ili tu ukidhi tamaa yako!?
Kuna wakati uliwahi kuzungumzia kuhusu akina mama shupavu waliowahi kuwabeba waume zao (vijana wadogo)na kupata mafanikio makubwa ya kiuchumi na kifamilia. (Kumbukumbu"Khadija bint khuwailah wa mtume muhamed(S.A.W)
Mariam magdalena wa Yesu(A.S)
Bi Sara wa (......)na wote hao walikuja kuoa waschana wadogo baada ya mafanikio waliyoyapa kutoka kwa wake zao wakubwa.(Hao wake wakubwa wote ni Single mother)
 

Amfanyie single mother ubaya kwa kosa gani? Kwa sheria ipi?

Mbona unafanya watu hasa wanaume kama hamnazo!

Kwenye hoja ya wanaume wana maujinga mengi sana. Hiyo naweza kukubali na ndio maana kila mara nawaambia wanawake wawe na ujuzi, wajitunze, wajitambue na wafanye kazi za kujipatia kipato.
Ili wanaume wajinga wakifanya ujinga ngoma isiwalalie wao.

Siku zote mhanga ndiye anatakiwa kujihami. Nafikiri hili unalijua
 
Hujasoma wananipigia simu

Atakupopoa Hadi ukome😁,
 
HUNA SABABU YA KUWA BABA YA KAMBO HASA UKIWA CHINI YA MIAKA 45.
Mimi nimelelewa na baba wa kambo na alinipenda kama mwanae wa kumzaa na mimi nilihemshimu kama baba yangu mzazi na mpaka leo ninamheshimu sana licha ya kuwa alishafariki. Kwa wema wake huo leo hii nina maisha mazuri. Ninachojaribu kusema ni kwamba hizi mada zina agenda ambayo sio nzuri sana. Jitahidini kuwa fair kwenye judgements zenu.
 
Hivi haujui ya kuwa mwanaume hasa waliochafukwa hupeleka trauma kwa weakes link hasa ngazi ya familia... Kama sio mtoto ni mwanamke.. So ukija na mada hizi zina wa pump wanaume washenzi kuwa I can do this to this woman because of her past failure(kama kuzalishwa) wakati mda mwingine alikutana na janaume la hovyo huko... Sasa na wewe unamwongezea maumivu kwa kumjaji kisa kazalishwa!

Sikatai kuna wanawake wajinga pia ila judgements huongeza more catastrophes

Katika maisha unaweza kujihami lakini human nature huwa na madhaifu hasa ikishaangukia kwenye mahusiano. Pesa na utajiri in most cases sio weapon but huwa ni chocheo la uharibifu especially kama hakuna hekima
 

Hiyo ni moja kwa mia moja.
Unataka wababa wakambo waanze kutema nyongo hapa?

Kitu kuwa kibaya hakitakuwa kibaya kwa watu wote. Na kitu kuwa kizuri hakitakuwa kizuri kwa watu wote.

Ila itabaki hivi kibaya ni kibaya na kizuri ni kizuri.
 

Mkuu hao wanaume wa aina hiyo basi hawastahili kuwa hata Mume au kuwa Baba.

Ndio maana kuna sehemu nimesema kabla hujawa Baba wa kambo lazima ujiulize ni kweli unahakika upo tayari kuwa Baba wa kambo. Yaani ujue changamoto na matokeo yanaweza kwenda tofauti na ulivyopanga.

Mathalani, mtoto sio wako umemlea tangu akiwa mdogo, lakini inaweza kutokea siku akakuambia wewe sio babaake na ni kweli sio babaake mzazi. Je umejiandaaje kihisia ikitokea hivyo?

Vipi akimkubali babaake aliyemtelekeza na kukuacha wewe upo tayari?
Au ndio ile utaanza kuleta uhalifu na kuua watu?

Huwezi kuona hoja hizi kwa sababu bado unatumia hisia.

Nilikuambia mimi Nina Mama, mabinti, na pia ndugu za kike.
Usifikiri unahuruma kunizidi kisa ninasema ukweli unaogopwa na wengi
 
Unatushauri nini sisi tuliooa wanawake tayari wana watoto zaidi ya wawili mkuu? Tuwaache au

Ninachojua mpaka mwanaume anaoa alishajua na kufanya uamuzi
Sahihi.

Nitashangaa mtu awe ameoa kwa kukurupuka. Hajui alikuwa anataka nini kwenye maisha yake
 
Nilikuambia mimi Nina Mama, mabinti, na pia ndugu za kike.
Usifikiri unahuruma kunizidi kisa ninasema ukweli unaogopwa na wengi
Hakuna ukweli wowote hapo hizo ni personal beliefs na experience.. Sio universal truth..

Nakubali mtu kujitathmini ila swala la malezi ni baina ya hao watu wawili waliopendana. Shida ya mtoto kukataa mzazi ni ya mtoto. Imagine kuna watu wamezaa watoto kabisa na ni wao lakini mtoto anamkataa mzazi live. So issue kubwa ni how one is treated and how one faces the circumstances.
 
Baba wa Kambo acheni kuchapa watoto wadogo wa wake zenu mnajidhalilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…