Huna Wajibu wa kumtunza au kumhudumia Mzazi wako akiwa chini ya miaka 60 kama haumwi

Hizi laana ulizonazo zilitoka kwa wazazi wako baada ya kukataa kuwaudumia na huku ukijua wazazi wako ni maskini, bado unakuja hapa kushawishi vijana wa leo nao waangukie kwenye laana kama zako, UKALAANIKE PEKE YAKO, MBWA WEE.
[emoji16][emoji16]
 
Topics zake nyingi zipo kinadharia zaidi kama filamu vile!
 

Kibongo bongo kama Mzazi anafikiria kutunzwa na kuhudumiwa na watoto jua wapo watoto wenye fikra hizo hizo kuwa wao hawakûtaka kuzaliwa ila ni kiherehere cha wazazi wao kuwazaa hivyo wao ndio wanawajibu wa kuwatafutia Maisha.
Ndio hapo hapa mjini watoto hawataki kutoka nyumbani na mzazi huna chakufanya na ukileta Ngebe wanakumaliza.

Mzazi anayetegemea mtoto ilhali yupo umri wenye nguvu hana tofauti na mtoto anayetegemea mzazi ilhali yupo umri wa utafutaji.
Ni vile Watu hawataki ukweli
 
Sahihi Mkuu

It is possible play your part
 
[emoji1545][emoji1545]
 
Tunafukuzia hiyo akaunti ya siri😄😄 mzee mpaka uteme laana zote lakini pesa ndio tumeshazipiga hivyo
Hiyo akaunti ya Siri Bora wale Hela watu wa Benki lakini sio nyie

Watoto wa miaka hii wamebadirika sana, full kuwawinda Wazee wao na kuwaombea wafe mapema
 
Wazazi wa kesho nimesoma comment zenu .

Inaonekana kuwa ni lazima mtoto amsaidie mzazi .

Kuna wazazi baada ya watoto kuweza kutafuta /siyo kujitegemea ni kutafuta wameacha kabisa kujitafutia na kutegemea watoto .

Siyo haki kabisa narudia Tena siyo haki, mzazi anazo/unazo nguvu kabisa unamlazimisha mtoto akusaidie Kwa kigezo Cha kwamba mbona nilikulea huku ukitoka matusi na laana . Ukimjengea kijana hofu ..

Ni nani aliyefanikiwa Kwa kutizama nyuma?

Badala ya kuwa msaada wewe ambaye umekula chumvi nyingi na maarifa mengi unayafanya maarifa yako obsolete , Ukitegemea Leo Ione kesho kweli ?

Wazazi /Vijana wa Leo Mimi na wewe tubadili hii mindset ..

Tujiwekeze vilivyo in the end tuwe na win win situation tusiwe ni wakuchukuwa tuuu
 
Mtoa mada amezaliwa kwenye familia ya uchumi wa Juu au uchumi wa Kati. Kwa maana aidha wazazi wake wote ni watumishi wa serikali au walishaga jipata kijana amakuta Mali zipo, ndyo maana amepata muda wa kufikilia na kutoa hizo tafakuli zake! Hivyo basi kwa Upande wake yupo sahihi.

Lakini kwa SISI tuliozaliwa kwenye tabaka la uchumi wa chini, baba na mama na Ndugu na jamaa wote ni wakulima wa jembe la mkono hatuwezi kuwa na MAWAZO kama hayo ya mtoa Mada.
 
Hiyo akaunti ya Siri Bora wale Hela watu wa Benki lakini sio nyie

Watoto wa miaka hii wamebadirika sana, full kuwawinda Wazee wao na kuwaombea wafe mapema

Mzazi anawinda mtoto apate kazi
Na mtoto anawinda mzazi apate kiinua mgongo chake.
Hatari sana
 

Sio kwéli.
Mimi ni mzaliwa wa familia ya chini
 

Upo positive Sana
 
Twende kisheria mzazi asipo muhudumia mtotowake anashitakiwa sio! Je mzazi anaweza kumshitaki mtoto kwa kutomuhudumia?
Achana na sheria ndugu, nenda kwenye uhalisia. Hujui wakati mwingine sheria humnyima mtu haki maana zinatungwa kwa malengo kuumiza wengi na kufurahisha wachache. Umewahi kuskia mtu kaua hadharani lakini kashinda kesi.

Achana na mambo ya kwenye makaratasi, nenda kwenye vitendo.
 
Unajua kusoma sana siyo kuelimika. Naweza kusema mleta mada kasoma lakini inaonekana hajaelimika Bali kaathiriwa na vyeti vya darasani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…