Huna Wajibu wa kumtunza au kumhudumia Mzazi wako akiwa chini ya miaka 60 kama haumwi

Mleta mada umeona mindset za watu weusi?

Mtu mweusi
anazaa watoto kama investment.

Lengo la mtu mweusi kuzaa watoto ni ili watoto waje wamhudumie.

Hapa umegusa shina halisi la maana ya maisha ya muafrika, utapingwa na kila mtu.
Hata ufanyeje huwezi kuikimbia asili yako na ndiyo umeshakuwa hivyo huna namna.

Kama yupo hapa mtu anayeweza kusema mzazi asisaidiwe kwa kigezo chochote kile eg:umri maradhi ni kusema hela anatafuta za kazi gani?wema atamtendea nani ikiwa hata yule aliyemzaa na kumsomesha anajiuliza ampe au asimpe huyu ataweza kweli kumsaidia hata mlemavu?
 
Mimi niliwahi kuwa na dada wa kazi binti mdogo tu wa miaka 18, mshahara nilikua namlipa elf.50 kwa mwezi. Kitu Cha kushangaza ikifika tarehe tu mshahara kulipwa mama wa yule Binti anampigia simu mwanae atumiwe hiyo pesa.

Yule binti hakuwahi kutumia pesa yake hata kidogo maana akipokea tu mama ake anampigia na kumwambia shida kibao alizonazo huko alipo. Aisee nilikua namuhurumia sana lkn hakua na uwezo wa kumkatalia mama ake.

Wazazi inabidi tujitafakari sana, tuwape muda watoto watafute maisha. Wakishajipata watarudi kusaidia nyumbani, hii kumbebesha mzigo mtoto ni kumdidimiza aendelee kuwa masikini.
 
Mzazi ni mungu wa duniani.

Kushukuru ni kufungua milango ya baraka.

Mawazo haya ya kujitenga na wazazi wako Mwanaume, lazima utakuwa Umepewa na mkeo ambaye pesa zote anapeleka kwao.
Mke amtoe wapi huyu chakubanga?

Bado maskini sana huyu na bado mdogo,kuanza tu kuona kumsaidia Baba yake nor mama yake siyo jukumu lake huyu hawezi ishi na binti wa mtu.na hawa ndiyo wanataka kusaidiana maisha na mke hata wakijua ametoka kudanga.
 
Pole mkuu
 
Mke amtoe wapi huyu chakubanga?

Bado maskini sana huyu na bado mdogo,kuanza tu kuona kumsaidia Baba yake nor mama yake siyo jukumu lake huyu hawezi ishi na binti wa mtu.na hawa ndiyo wanataka kusaidiana maisha na mke hata wakijua ametoka kudanga.
Ulichoongea nini
utoto ndo unaomsumbua sababu unaweza ukawa na miaka hata 40 ila utoto ukawa unakusumbua

majukumu ya mwanaume ni pamoja na kusaidia wazazi wako ndo asili yetu wa afrika
Mada nyingi sana za huyu jamaa zinautoto mwingi sana na fantasy kama watu wakizifuata basi tutakua na jamii ya hovyo sana ya kila mtu abebe msalaba wake

Wanawake uwaonge na marafik zako uwanunulie bia ila iwe ni nongwa kumsaidia mzazi wako tunawatu wanafikra za hovyo sana
 
Kwa asili mtu akizeeka anakuwa less productive,kuna wakati tu utahitaji jeki kama sio MALI basi jeki ya HALI,
Kama watoto wako wa kuzaa hawawezi kufanya lolote kati ya hayo basi hiyo ni PATAPOTEA.

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Kwa asili mtu akizeeka anakuwa less productive,kuna wakati tu utahitaji jeki kama sio MALI basi jeki ya HALI,
Kama watoto wako wa kuzaa hawawezi kufanya lolote kati ya hayo basi hiyo ni PATAPOTEA.

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
Ukiwa kijana una-nguvu unaamini hizo nguvu utakua nazo milele kama mleta uzi anavyodhani
Ila kuna mda nguvu zinaisha inabidi uwe mpole
 
Watanzania wengi hatuwezi kukuelewa kwa sababu fikra zetu zimegandishwa na ujamaa wa Mwalimu.

Chanzo kikuu cha umasikini Tanzania ni umasikini wa kurithi na siyo wa kipato.

Yaani unakuta mtu ana kipato kizuri lakini kwa kuwa nyuma yake ana msururu wa ndugu wategemezi basi automatically anakuwa masikini.

Yaani unazaliwa na ukikua tu ndugu wanaanza kukuganda uwasaidie na utatue shida zao.

Mimi niliwahi kupewa jukumu la kujenga nyumba kwa babu sehemu ambayo baba zangu na baba wadogo walishindwa kujenga kwa zaidi ya miaka 40.

Nikawaambia siwezi kujenga hapo wakati mimi bado kwangu.

Waafrika tuna mambo ya ajabu sana!
 
Mke amtoe wapi huyu chakubanga?

Bado maskini sana huyu na bado mdogo,kuanza tu kuona kumsaidia Baba yake nor mama yake siyo jukumu lake huyu hawezi ishi na binti wa mtu.na hawa ndiyo wanataka kusaidiana maisha na mke hata wakijua ametoka kudanga.
Kila mwaka wanaenda Moshi ukweni,

Unakuta watoto aliowazaa, hawajui Babu Yao wa kiumeni, ni ukweni tu,

Wanawake tuishi nao Kwa akili asee!!
 
Baba kumbe ndiyo tabia yako unatufanyia!?

Na ukipata tatizo usitusumbue; utumie hizohizo hela!

Na mama nitamwambia!
 
Mtoa mada katumia akili nyingi sana huenda ni Uzi mzuri zaidi ktk hii wiki.

Wachangiaji wengi hawana critical thinking na wanakurupuka kumkosoa mtoa mada bila kuwaza mara mbilimbili na kufanya analysis.

Binafsi nitashare experience yangu:

Baada ya kupata kazi tu.. nikaanza kujumuishwa ktk ishu za familia hasa kulipia ADA wadogo zangu (Hapo mwanzo walikuwa wanalipiwa na Wazazi na Shule waliyosoma wao ni ghali sana na wapo watatu) haya nikawa najibana nalipa angalau nusu ya ada kwa wote watatu.

Ikumbukwe mimi nimesoma shule ya kidumu na mfagio na wazee walikuwa nauwezo wa kunisomesha ktk mabas ya njano ila wakanitupa huko.

Wananyumba huwa wamepangisha na wanakusanya kodi kila mwisho wa mwezi, kama mtoto ktk swala la mgao wala sijawahi kupata hata mia.. na wakikusanya maokoto hata taarifa hupati ila ww utapata taarifa za majanga tu kuna hiki kimeharibika kuna kile kinataka hela etc.. ila.maswala positive hutosikia taarifa achilia mbali mgao (siutaki mgao wenyewe).

Haya ilifikia muda nataka kuoa, wakaniwekea ngumu nisioe (akili yangu ikawa imejiongeza na kujua nini sababu ya wao kunikataza kuoa wakisema ni mapema kwamba nina umri mdg hapo nina 28), jambo ambalo wao walikuwa hawataki ni mm kuwa na majukumu na familia yangu ntakayoanzisha hivyo sitaendelea kuwapa hivyo vihela vya hapa na pale..

Familia za kimaskini ukiziendekeza hupigi hatua sana sana unabaki palepale kila siku.. mshahara unaingia unapitiliza kusolve ishu zao sometimes ubinafsi unasaidia sana kupata maendeleo.

Wazazi wawaache wototo wajiimarishe kiuchumi ndio wafaidike na sio mtu kajipata kdg tu tyr majukumu mnamjazia hapo hata kujiweka sawa bado na mnaenda mbali kumzuia ishu za msingi kbs kama kuanzisha familia yake ili muendelee kula hela zake kwa uhuru..

Kwani nan kasema nikiwa na familia yangu sitawasaidia? Mawazo ya kimaskini sana..
 
Wewe ndo HAMNAZO. Huyu Mtibeli yuko sahihi 100%. Tena hiki ni kilio cha wengi ila kimyakimya. Watu wanawasitiri tu wazazi wao ila ndani kwa ndani moto unawawakia. Mabinti wananyanyasika kwenye ndoa wazazi wanaishia kuwaambia NDOA NI UVUMILIVU kisa kuna maokoto wanapata kutoka kwa mkwe. Watu wengi imekuwa ngumu kuchomoka kwenye umaskini kwasababu ya kutumia muda na pesa zao kufanya majukumu ya wazazi wao kama vilw kusomesha wadogo zao. Watoto wa kwanza wengi huwa maskini na wale wa mwisho huwa na unafuu kwa kutokuwa na majukumu mengi. PUNGUZENI UNAFIKI tujiokoe kwenye umaskini.
 
Kinachonipa faraja ni kwamba, Ujinga wa muafrika hausababishwi na rangi yake, bali na vitu vingine hivyo basi,

Naikubali rangi yangu nyeusi ila naukataa Ujinga wa mtu mweusi.

Wewe kama unaamini ni jukumu lako kuhudumia wazazi wako hudumia, na kama unadhani ni jukumu la watoto wako kukuhudumia waambie wakuhudumie,

Kujaribu kukushawishi vinginevyo ni kupoteza muda, maana hata hujaelewa alichosema mleta mada.
 
Mleta mada umeona mindset za watu weusi?

Mtu mweusi anazaa watoto kama investment.

Lengo la mtu mweusi kuzaa watoto ni ili watoto waje wamhudumie.

Hapa umegusa shina halisi la maana ya maisha ya muafrika, utapingwa na kila mtu.

Lazima nilaaniwe na kupingwa na Watu humu.
Wakati hilo ni jambo lipo Wazi
 

Upo mbele yangu kwa kunielewa
 
Sishangai Mtibel kutoeleweka!

Alichoandika taikuni wa fasihi ni akili kubwa na kinaeleweka kwa wenye akili kubwa pia.

Ukipata shida kuelewa huu uzi, unapaswa kutathimini akili yako na siyo kushambulia mwandishi. Kila kitu kipo wazi.
shida ni kwamba, hakuna anayesoma ndani ya uzi
mtu anavamia heading na ku comment povu
 
Wazazi wengi wa kiafrika wanazaa watoto wengi ili wakishakuwa wakubwa waje kuwafanya watumwa nao wazazi wabaki kuwa mabwana wanaotumikiwa na watoto wao(hizi ni fikra za kimaskini na ufukara wa kutupwa); toka nimeligundua hilo na hali ya dunia iliyopo sasa nimejiapiza nitazaa watoto wachache hawatazidi wawili, ili nipate nafasi ya kujiimarisha kiuchumi na wao wakiwa wakubwa waendelee na maisha yao bila mimi kuwasumbua. am done.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…