Huna Wajibu wa kumtunza au kumhudumia Mzazi wako akiwa chini ya miaka 60 kama haumwi

Huwezi kubarikiwa kwa hiyari yako. Mtu anabarikiwa kwa wajibu kwa kutekeleza yanayompasa.
Kukupambania ni wajibu wao.
Na wewe unawajibu wa kuwapambania muda sahihi ukifika yaani wakiwa wazee.

Ndio maana kadiri ulivyokuwa unakua mkubwa ndivyo walivyokuwa wanakuacha na wajibu wao kwako ulikuwa unapungua ikiwemo kukutafutia chakula, mavazi na malazi.
We kama huwapendi wazazi wako au ndugu zako vunja undugu anzia na baba yako na mama yako alafu wafuate watu wengi
 
Mtoa mada katumia akili nyingi sana huenda ni Uzi mzuri zaidi ktk hii wiki.

Wachangiaji wengi hawana critical thinking na wanakurupuka kumkosoa mtoa mada bila kuwaza mara mbilimbili na kufanya analysis.

Binafsi nitashare experience yangu:

Baada ya kupata kazi tu.. nikaanza kujumuishwa ktk ishu za familia hasa kulipia ADA wadogo zangu (Hapo mwanzo walikuwa wanalipiwa na Wazazi na Shule waliyosoma wao ni ghali sana na wapo watatu) haya nikawa najibana nalipa angalau nusu ya ada kwa wote watatu.

Ikumbukwe mimi nimesoma shule ya kidumu na mfagio na wazee walikuwa nauwezo wa kunisomesha ktk mabas ya njano ila wakanitupa huko.

Wananyumba huwa wamepangisha na wanakusanya kodi kila mwisho wa mwezi, kama mtoto ktk swala la mgao wala sijawahi kupata hata mia.. na wakikusanya maokoto hata taarifa hupati ila ww utapata taarifa za majanga tu kuna hiki kimeharibika kuna kile kinataka hela etc.. ila.maswala positive hutosikia taarifa achilia mbali mgao (siutaki mgao wenyewe).

Haya ilifikia muda nataka kuoa, wakaniwekea ngumu nisioe (akili yangu ikawa imejiongeza na kujua nini sababu ya wao kunikataza kuoa wakisema ni mapema kwamba nina umri mdg hapo nina 28), jambo ambalo wao walikuwa hawataki ni mm kuwa na majukumu na familia yangu ntakayoanzisha hivyo sitaendelea kuwapa hivyo vihela vya hapa na pale..

Familia za kimaskini ukiziendekeza hupigi hatua sana sana unabaki palepale kila siku.. mshahara unaingia unapitiliza kusolve ishu zao sometimes ubinafsi unasaidia sana kupata maendeleo.

Wazazi wawaache wototo wajiimarishe kiuchumi ndio wafaidike na sio mtu kajipata kdg tu tyr majukumu mnamjazia hapo hata kujiweka sawa bado na mnaenda mbali kumzuia ishu za msingi kbs kama kuanzisha familia yake ili muendelee kula hela zake kwa uhuru..

Kwani nan kasema nikiwa na familia yangu sitawasaidia? Mawazo ya kimaskini sana..
Siamini kwamba huwezi endelea eti kwa sababu unasaidia ndugu zako huo ni uongo
Maisha hutakiwi kuyaogopa

Kama kila kitu cha kiafrika mnakikataa basi na huo ushoga wa wazungu muukubali
 
Ushoga ni tabia sio tamaduni.
Tofauti tamaduni na tabia.
Wazungu hakuna tamaduni ya ushoga.
 
ushauri wangu
DELETE HII MADA KWANI HAINA AFYA KWA JAMII
Wazazi ndio kila kitu hapa duniani; Wasaidie kwa kadri Mungu alivyo kubariki na wala haina uhusiano na umri

Hakuna kitu kisichokuwa na uhusiano na umri.
Hizo shule mmesomea ujinga?

Alafu kama unaakili nzuri huwezi kushindwa kuelewa mada hii inazungumzia nini.
Hakua sehemu nimesema mtu asisaidie mzazi wake ila nilichoandika ni kuwa sio wajibu mtu kumsaidia mzazi aliyechini ya Miaka 60 ambaye HAUMWI.
Ni hiyari au mapenzí.
 
Siamini kwamba huwezi endelea eti kwa sababu unasaidia ndugu zako huo ni uongo
Maisha hutakiwi kuyaogopa

Kama kila kitu cha kiafrika mnakikataa basi na huo ushoga wa wazungu muukubali
Maswala ya ushoga yanaingiaje hapa?

Ndio huwezi endelea ukizidisha misaada kama unabisha sawa.

Kusaidia kuna kiwango chake ndio maana hata maandiko yakaweka fungu la 10 at least 10% ya unachopata kitoe sadaka. Ila kifamilia unasaidia asilimia 80 ww unabaki na 20% utafanya nini cha maana?
 
HUNA WAJIBU WA KUMTUNZA AU KUMHUDUMIA MZAZI WAKO AKIWA CHINI YA MIAKA 60 KAMA HAUMWI.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mada hii inaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya Watu. Lakini nitakachojadili hapa ni Haki, kweli, akili na upendo kama ilivyo kwa Watibeli wote.

Kama ilivyo kwa mzazi hana wajibu wa kukutunza na kukuhudumia pindi ufikishapo umri wa kujitegemea yaani kuanzia miaka 21 hivi kwa sisi Watibeli. Na kwa sheria za dunia ni miaka 18. Basi ndivyo hivyohivyo kuwa mtoto hana wajibu wa kumtunza na kumhudumia mzazi au mlezi ambaye yupo chini ya miaka 60 ambaye HAUMWI(hana tatizo la kiafya).

Kuna kijitabia fulani cha kinyonyaji, dhulma, uvivu, na ukandamizaji ambao unafanywa na wazazi kwenda kwa watoto wao. Ambapo mzazi anazaa watoto idadi fulani anawapa na kuwatunza(wajibu wake) alafu wakishafikisha miaka 20 tuu wakaenda kujitafutia basi inakuwa nongwa. Mzazi hata miaka 50 haujui, miaka 60 ndio kabisa hatarajii leo wala kesho kuifikia. Mzazi ananguvu kabisa lakini kutwa kusumbua watoto na kuwatia watoto katika shinikizo isivyostahili.

Sio jukumu la mtoto kukulea na kukutunza ukiwa na umri huo. Wewe bado upo umri wa kujitegemea na kujihudumia. Kwa nini umpe mtoto mzigo? Kwa nini umdhulumu mtoto haki zake?
Kama sababu ni kuzaa na kumtunza hata yeye atazaa na kutunza watoto wake.

Kama ishu ni wajibu basi subiri muda ukifika mtoto atekeleze wajibu wake. Na kama atakutunza au kukuhudumia iwe kwa uwezo na mapenzi yake kwako na shukran na sio shinikizo.

Ni laana kubwa kumhudumia mtu isivyo halali. Kuhudumia mzazi kwa kushinikizwa yaani kunyonywa na kudhulumiwa ni laana ambayo wengi inawatafuna.

Sio ajabu unakuta Watu wengi tangu wakiwa vîjana wanateseka kuhudumia wazazi isivyostahili wakifikiria ndio baraka lakini miaka inaenda maisha yao hayabadiliki zaidi ya kuzidi kuwa maskini na fukara zaidi.

Ni sawasawa na mzazi amuone mtoto keshafikia umri wa kujitegemea alafu bado awe anamhudumia na kumtunza huo ni umaskini wa akili na roho. Lazima kizazi hiki kiwe fukara.

Ninajua ndoa nyingi zilizoharibika na familia nyingi kuanguka kisa wazazi kushinikiza huduma. Ni laana tupu. Wakati huo wazazi wananguvu kabisa.
Ninajua mabinti wengi wanaoteseka kwenye ndoa kisa wazazi wao wamewashinikiza watoto wao wabaki kwenye mateso ili wao wanufaike au walishanufaika na kumuuza binti yao.

Wengine huwashinikiza binti zao waolewe na wanaume wenyewe pesa hata kama hawapendwi na binti zao kwa kulenga kuhudumiwa na pesa za mkwilima wao.

Wapo vibinti vya kazi za ndani wanalipwa mishahara kiduntu kama elfu 30 mpaka 60 na bado wazazi wanataka gawiwo licha ya kuwa wazazi hao bado kiumri wanauwezo wa kufanya kazi na kujitafutia.

Wapo wazazi kiumri ni wadogo lakini wanawakosea watoto wao haki kwa kuwashinikiza watoto wao kwa matusi na kejeli kuwa hawafanyi kazi huko mjini kisa tuu hawatumiwi pesa. Jambo ambalo sio Haki na sio Upendo.
Wapo watoto wanajitutumua kuhakikisha wanahudumia wazazi wao kiugumuugumu, kwa kujikamua, na malalamiko ya nafsi wazazi kwa ubinafsi wao huona ni sahihi lakini sio sahihi kabisa.

Acheni watoto wakiwa na umri wa kujitafutia watafute na kujitegemea alafu wao kwa roho ya upendo wawatumie kwa hiyari yao na sio kuwadhulumu maisha na nguvu zao.

Watoto pia, acheni kudhulumu nguvu za wazazi wenu huku mkujua kuwa tayari mmefikia umri wa kujitegemea na sio kuwapa wazazi wenu mzigo, kuwanyonya na kuwakatili.
Mzazi asifurahie utu uzima wake aanze kukufikiria mtu mzima na ndevu zako kisa ati ni mtoto wake. Hiyo sio HAKI

Kumhudumia mzazi wako aliyemzee sio hiyari yako wala sio mapenzi yako kwake. Hiyo ni lazima, wajibu.
Bahati nzuri wazee hawana mahitaji mengi kama ilivyo kwa watoto.

Lakini kuhudumia mzazi aliyechini ya miaka 60 na haumwi hiyo ni hiyari na mapenzi tuu na sio lazima/wajibu. Unaweza ukafanya au usifanye na hakuna lolote litakupata.

Kumhudumia mtu anayeweza kujitegemea ni laana na kurudisha nyuma kizazi na ukoo wenu.
Lazima Watu wafanyekazi na wawajibike kwa maisha yao na ya wale wanaowahusu.

Huo ndio Utibeli. Ukweli, haki, upendo na Haki
Mimi nimemaliza, mwenye maswali anaweza kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mkuu sijasoma ila nadhani siko upande wako
 
Hizi roho za kichawi zirudishe kwenye ukoo wenu,, kusaidia mtu hautaji umri. Kuna watu mitaani wengine ni vijana na wanasaidiwa bila hata kuwa na nasaba nao.
Kama unauwezo wa kupata bundle na kuandika huu upuuzi hapa mshukuru Mungu wako usidhani na kujiona kuwa wewe ndo mwenye akili kuliko wote.

Ok fine mzazi yuko chini ya miaka sitini hana kazi, unatake home ya ten digits kuendelea uko tayari kwenda baa ili hali baba na mamako wanalala na kushinda njaa kwa sababu tu wako below 60, narudia hii roho ya kichawi peleka kwenye jukwaa la ukoo
 
HUNA WAJIBU WA KUMTUNZA AU KUMHUDUMIA MZAZI WAKO AKIWA CHINI YA MIAKA 60 KAMA HAUMWI.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mada hii inaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya Watu. Lakini nitakachojadili hapa ni Haki, kweli, akili na upendo kama ilivyo kwa Watibeli wote.

Kama ilivyo kwa mzazi hana wajibu wa kukutunza na kukuhudumia pindi ufikishapo umri wa kujitegemea yaani kuanzia miaka 21 hivi kwa sisi Watibeli. Na kwa sheria za dunia ni miaka 18. Basi ndivyo hivyohivyo kuwa mtoto hana wajibu wa kumtunza na kumhudumia mzazi au mlezi ambaye yupo chini ya miaka 60 ambaye HAUMWI(hana tatizo la kiafya).

Kuna kijitabia fulani cha kinyonyaji, dhulma, uvivu, na ukandamizaji ambao unafanywa na wazazi kwenda kwa watoto wao. Ambapo mzazi anazaa watoto idadi fulani anawapa na kuwatunza(wajibu wake) alafu wakishafikisha miaka 20 tuu wakaenda kujitafutia basi inakuwa nongwa. Mzazi hata miaka 50 haujui, miaka 60 ndio kabisa hatarajii leo wala kesho kuifikia. Mzazi ananguvu kabisa lakini kutwa kusumbua watoto na kuwatia watoto katika shinikizo isivyostahili.

Sio jukumu la mtoto kukulea na kukutunza ukiwa na umri huo. Wewe bado upo umri wa kujitegemea na kujihudumia. Kwa nini umpe mtoto mzigo? Kwa nini umdhulumu mtoto haki zake?
Kama sababu ni kuzaa na kumtunza hata yeye atazaa na kutunza watoto wake.

Kama ishu ni wajibu basi subiri muda ukifika mtoto atekeleze wajibu wake. Na kama atakutunza au kukuhudumia iwe kwa uwezo na mapenzi yake kwako na shukran na sio shinikizo.

Ni laana kubwa kumhudumia mtu isivyo halali. Kuhudumia mzazi kwa kushinikizwa yaani kunyonywa na kudhulumiwa ni laana ambayo wengi inawatafuna.

Sio ajabu unakuta Watu wengi tangu wakiwa vîjana wanateseka kuhudumia wazazi isivyostahili wakifikiria ndio baraka lakini miaka inaenda maisha yao hayabadiliki zaidi ya kuzidi kuwa maskini na fukara zaidi.

Ni sawasawa na mzazi amuone mtoto keshafikia umri wa kujitegemea alafu bado awe anamhudumia na kumtunza huo ni umaskini wa akili na roho. Lazima kizazi hiki kiwe fukara.

Ninajua ndoa nyingi zilizoharibika na familia nyingi kuanguka kisa wazazi kushinikiza huduma. Ni laana tupu. Wakati huo wazazi wananguvu kabisa.
Ninajua mabinti wengi wanaoteseka kwenye ndoa kisa wazazi wao wamewashinikiza watoto wao wabaki kwenye mateso ili wao wanufaike au walishanufaika na kumuuza binti yao.

Wengine huwashinikiza binti zao waolewe na wanaume wenyewe pesa hata kama hawapendwi na binti zao kwa kulenga kuhudumiwa na pesa za mkwilima wao.

Wapo vibinti vya kazi za ndani wanalipwa mishahara kiduntu kama elfu 30 mpaka 60 na bado wazazi wanataka gawiwo licha ya kuwa wazazi hao bado kiumri wanauwezo wa kufanya kazi na kujitafutia.

Wapo wazazi kiumri ni wadogo lakini wanawakosea watoto wao haki kwa kuwashinikiza watoto wao kwa matusi na kejeli kuwa hawafanyi kazi huko mjini kisa tuu hawatumiwi pesa. Jambo ambalo sio Haki na sio Upendo.
Wapo watoto wanajitutumua kuhakikisha wanahudumia wazazi wao kiugumuugumu, kwa kujikamua, na malalamiko ya nafsi wazazi kwa ubinafsi wao huona ni sahihi lakini sio sahihi kabisa.

Acheni watoto wakiwa na umri wa kujitafutia watafute na kujitegemea alafu wao kwa roho ya upendo wawatumie kwa hiyari yao na sio kuwadhulumu maisha na nguvu zao.

Watoto pia, acheni kudhulumu nguvu za wazazi wenu huku mkujua kuwa tayari mmefikia umri wa kujitegemea na sio kuwapa wazazi wenu mzigo, kuwanyonya na kuwakatili.
Mzazi asifurahie utu uzima wake aanze kukufikiria mtu mzima na ndevu zako kisa ati ni mtoto wake. Hiyo sio HAKI

Kumhudumia mzazi wako aliyemzee sio hiyari yako wala sio mapenzi yako kwake. Hiyo ni lazima, wajibu.
Bahati nzuri wazee hawana mahitaji mengi kama ilivyo kwa watoto.

Lakini kuhudumia mzazi aliyechini ya miaka 60 na haumwi hiyo ni hiyari na mapenzi tuu na sio lazima/wajibu. Unaweza ukafanya au usifanye na hakuna lolote litakupata.

Kumhudumia mtu anayeweza kujitegemea ni laana na kurudisha nyuma kizazi na ukoo wenu.
Lazima Watu wafanyekazi na wawajibike kwa maisha yao na ya wale wanaowahusu.

Huo ndio Utibeli. Ukweli, haki, upendo na Haki
Mimi nimemaliza, mwenye maswali anaweza kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kuna mambo ni magumu kujadili kama huna Imani ya Kiroho. Kama unauwezo wahudumie Wazazi wako kama huna muonbe Mungu akusaidie. Ipo nguvu kuwatumia Wazazi matumizi na pia ipo nguvu kwa mtoto anajuwa kumshika mkono mzazi wake. Bilget ni Tajiri mkubwa ila hawezi kataa akipelekewa Zawadi na mtoto wake. Au akihudumiwa jiulize kwanini? Kama Mungu alimjaribu Abraham akamtama amtolee sadaka nizaid sana kwa Wazazi wetu. Jifunze kuondoa mikosi na mabalaa kwa kutoa sadaka hasa kwa Wazazi wako na kwenda kuwaona hutojuwa thamani ya Wazazi wako mpaka wanakufa wewe ule nyama Wazazi wale mboga za majani utakufa utawaacha Wazazi🤐
Kijana mmoja akiwa mjini alisikia Wazazi wamepata mafuriko vijana wakauza kila kitu na kupukitisha mitaji kuwahengea Wazazi wakarudi mjini bila kitu wale madogo wanasema hawajuwi pesa zilitoka wapi ila walipiga pesa yakufa mtu. Leo ni matajiri. Walikuwa na uwezo kupotezea nakuendelea na maisha ila wakarudisha kwa Wazazi. 😭🤐
 
uanaharakati unavuruga sana taasisi za ndoa na familiia
 
Kuna mambo ni magumu kujadili kama huna Imani ya Kiroho. Kama unauwezo wahudumie Wazazi wako kama huna muonbe Mungu akusaidie. Ipo nguvu kuwatumia Wazazi matumizi na pia ipo nguvu kwa mtoto anajuwa kumshika mkono mzazi wake. Bilget ni Tajiri mkubwa ila hawezi kataa akipelekewa Zawadi na mtoto wake. Au akihudumiwa jiulize kwanini? Kama Mungu alimjaribu Abraham akamtama amtolee sadaka nizaid sana kwa Wazazi wetu. Jifunze kuondoa mikosi na mabalaa kwa kutoa sadaka hasa kwa Wazazi wako na kwenda kuwaona hutojuwa thamani ya Wazazi wako mpaka wanakufa wewe ule nyama Wazazi wale mboga za majani utakufa utawaacha Wazazi🤐

Msingi wa imani yako ni Biblia.
Embu tupe kisa kimoja ambacho mzazi anatakiwa ahudumiwe tena akiwa umri wa kufanya kazi na haumwi
 
Nimesoma tu heading nikagundua mtoa mada ni mtu ambae hamnazo.!

Ni mtu ambae kila anachokifikiria kichwani kwake anakiona Cha kukileta mbele ya jamiii na kujiona genius.

Usipowapa furaha wazazi wako unataka kuwapa wakina nani.?? Maisha ni Nini kwako kama unajiweza na huku ukiwapa kisogo wazazi wako eti tu kisa wapo chini ya miaka 60.

saidia wazazi wako kwa kile ulicho nacho Wala hutapungukiwa chochote na zaidi baraka zitaongezeka katika utafutaji wako.!

Usisubiri mzazi afe ili uje kuonyesha fahari katika mazishi mbele ya jamii na marafiki WA kazini kwako

Note.
Maisha ni mafupi sana Miaka inaenda kama upepo siku si nyingi na sisi tutakuwa wazee kama walivyo wazazi wetu. Tusaidie ndugu na jamaa zetu

Nb.taikon WA fasihi ni mtoto mdogo Ambae hajui maisha yanataka nini. Yeye anajua mtu ukishapata Hela basi imeisha unafanya unavyoweza.kumbe sio kweli Kuna sehemu Hela na umaarufu havifiki

Be humble mzee sio Kila kitu Cha kuandika mtandaoni ' WE zombie.
Jamaaa kaongea ukweli yaan ndio inatakiwa hivyo kumzaa mtoto sio sababu ya kumbebesha mzigo www umeishi duniani karibu miaka 60 huna kitu umeshindwa kujitunza halafu unataka binadamu mwenzako ambae nae hana kitu akuangaikie kwa kitu ulichoshindwa wewe kama unataka kuwa fair usizae tuone kama kuna lawama au mzigo utapata duniani
 
HUNA WAJIBU WA KUMTUNZA AU KUMHUDUMIA MZAZI WAKO AKIWA CHINI YA MIAKA 60 KAMA HAUMWI.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mada hii inaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya Watu. Lakini nitakachojadili hapa ni Haki, kweli, akili na upendo kama ilivyo kwa Watibeli wote.

Kama ilivyo kwa mzazi hana wajibu wa kukutunza na kukuhudumia pindi ufikishapo umri wa kujitegemea yaani kuanzia miaka 21 hivi kwa sisi Watibeli. Na kwa sheria za dunia ni miaka 18. Basi ndivyo hivyohivyo kuwa mtoto hana wajibu wa kumtunza na kumhudumia mzazi au mlezi ambaye yupo chini ya miaka 60 ambaye HAUMWI(hana tatizo la kiafya).

Kuna kijitabia fulani cha kinyonyaji, dhulma, uvivu, na ukandamizaji ambao unafanywa na wazazi kwenda kwa watoto wao. Ambapo mzazi anazaa watoto idadi fulani anawapa na kuwatunza(wajibu wake) alafu wakishafikisha miaka 20 tuu wakaenda kujitafutia basi inakuwa nongwa. Mzazi hata miaka 50 haujui, miaka 60 ndio kabisa hatarajii leo wala kesho kuifikia. Mzazi ananguvu kabisa lakini kutwa kusumbua watoto na kuwatia watoto katika shinikizo isivyostahili.

Sio jukumu la mtoto kukulea na kukutunza ukiwa na umri huo. Wewe bado upo umri wa kujitegemea na kujihudumia. Kwa nini umpe mtoto mzigo? Kwa nini umdhulumu mtoto haki zake?
Kama sababu ni kuzaa na kumtunza hata yeye atazaa na kutunza watoto wake.

Kama ishu ni wajibu basi subiri muda ukifika mtoto atekeleze wajibu wake. Na kama atakutunza au kukuhudumia iwe kwa uwezo na mapenzi yake kwako na shukran na sio shinikizo.

Ni laana kubwa kumhudumia mtu isivyo halali. Kuhudumia mzazi kwa kushinikizwa yaani kunyonywa na kudhulumiwa ni laana ambayo wengi inawatafuna.

Sio ajabu unakuta Watu wengi tangu wakiwa vîjana wanateseka kuhudumia wazazi isivyostahili wakifikiria ndio baraka lakini miaka inaenda maisha yao hayabadiliki zaidi ya kuzidi kuwa maskini na fukara zaidi.

Ni sawasawa na mzazi amuone mtoto keshafikia umri wa kujitegemea alafu bado awe anamhudumia na kumtunza huo ni umaskini wa akili na roho. Lazima kizazi hiki kiwe fukara.

Ninajua ndoa nyingi zilizoharibika na familia nyingi kuanguka kisa wazazi kushinikiza huduma. Ni laana tupu. Wakati huo wazazi wananguvu kabisa.
Ninajua mabinti wengi wanaoteseka kwenye ndoa kisa wazazi wao wamewashinikiza watoto wao wabaki kwenye mateso ili wao wanufaike au walishanufaika na kumuuza binti yao.

Wengine huwashinikiza binti zao waolewe na wanaume wenyewe pesa hata kama hawapendwi na binti zao kwa kulenga kuhudumiwa na pesa za mkwilima wao.

Wapo vibinti vya kazi za ndani wanalipwa mishahara kiduntu kama elfu 30 mpaka 60 na bado wazazi wanataka gawiwo licha ya kuwa wazazi hao bado kiumri wanauwezo wa kufanya kazi na kujitafutia.

Wapo wazazi kiumri ni wadogo lakini wanawakosea watoto wao haki kwa kuwashinikiza watoto wao kwa matusi na kejeli kuwa hawafanyi kazi huko mjini kisa tuu hawatumiwi pesa. Jambo ambalo sio Haki na sio Upendo.
Wapo watoto wanajitutumua kuhakikisha wanahudumia wazazi wao kiugumuugumu, kwa kujikamua, na malalamiko ya nafsi wazazi kwa ubinafsi wao huona ni sahihi lakini sio sahihi kabisa.

Acheni watoto wakiwa na umri wa kujitafutia watafute na kujitegemea alafu wao kwa roho ya upendo wawatumie kwa hiyari yao na sio kuwadhulumu maisha na nguvu zao.

Watoto pia, acheni kudhulumu nguvu za wazazi wenu huku mkujua kuwa tayari mmefikia umri wa kujitegemea na sio kuwapa wazazi wenu mzigo, kuwanyonya na kuwakatili.
Mzazi asifurahie utu uzima wake aanze kukufikiria mtu mzima na ndevu zako kisa ati ni mtoto wake. Hiyo sio HAKI

Kumhudumia mzazi wako aliyemzee sio hiyari yako wala sio mapenzi yako kwake. Hiyo ni lazima, wajibu.
Bahati nzuri wazee hawana mahitaji mengi kama ilivyo kwa watoto.

Lakini kuhudumia mzazi aliyechini ya miaka 60 na haumwi hiyo ni hiyari na mapenzi tuu na sio lazima/wajibu. Unaweza ukafanya au usifanye na hakuna lolote litakupata.

Kumhudumia mtu anayeweza kujitegemea ni laana na kurudisha nyuma kizazi na ukoo wenu.
Lazima Watu wafanyekazi na wawajibike kwa maisha yao na ya wale wanaowahusu.

Huo ndio Utibeli. Ukweli, haki, upendo na Haki
Mimi nimemaliza, mwenye maswali anaweza kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Hauna nidhamu wewe.
 
Inatakiwa wazazi watafute namna waweze kujitegemea kipindi cha uzeeni, ni kama ushauri yaani

Lakini ikishatokea hayupo vizuri na unaweza kumsaidia, hata kama yupo under 60, hamna namna nyingine zaidi ya kumhudumia
Shida watu hawajamuelewa yeye hajakataa mtu kumhudumia mzee wake ila amesema sio lazima kama hajafika miaka 60... Yaani kama ambavyo hata kisheria mzazi hawajibiki kwa mwanae baada ya miaka 20 vivo hivyo kuna umri ambao mtoto hawajibiki kwa mzazi wake labda kwa mapenzi yake... Hapo sasa inategemea uhusiano wa mtoto na mzazi... Yaani wanaivaje?
 
Back
Top Bottom