Huna Wajibu wa kumtunza au kumhudumia Mzazi wako akiwa chini ya miaka 60 kama haumwi

Na hiyo ndio Haki na Mungu anavyotaka ufanye.
Huna huwezi wa kumlaani yeyote kisa hakuhudumii na upo umri wa kujitegemea.
Biblia inasema amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu. Tena mtoto wake.
Kuna haja wakati unatenga bajeti ya kusomesha watoto wako, Mzazi naye kujitengea bajeti yake ya Siri ya kujihudumia Uzeeni.

Imagine unatumia Millioni 12 Kwa Mwaka kwenye kulipa ada za watoto vipi kama ingekuwa unaitunza ili ikusaidie Uzeeni?

Wazazi itabidi tushtuke, watoto wameshaanza kutuwashia taa nyekundu 😜
 
Wazazi wa kiafrika huwezi walaumu ni mfumo wa maisha ya kiafrika upo hivyo
Wengi wetu hata sahivi ukiaambiwa unatakiwa uende india lazima upitishe bakuli

Mfumo wetu wa maisha ni wa kubangaiza kuanzia kwa serekali mpaka kwa wananchi

Kumsaidia mtu ni utu.

Mzazi wako mwenyewe hana wajibu wa kukutunza wala kukuhudumia ukishafikisja umri wa kujitegemea.
Halikadhalika na yeye akiwa umri wa kujitegemea huna wajibu wa kumtunza wala kumhudumia.
Isipokuwa ni hiyari na mapenzi yako au yake tuu kwako.
 
Kama kumsaidia mtu ni utu
Kwanini hutaki kusaidia wazazi wako eti mpaka wafikie miaka 60
Wewe huna utu wala upendo na kupitia nyuzi zako tumejua tabia yako

Mkuu una-fantasy sana kuna kundi kubwa la vijana wanamiaka 25 na zaidi wanaishi kwa wazazi wao,
Kama huna upendo wa kusaidia watu utatafuta visingizio kama vyako vya kutokusaidia
 
Sio sahihi ulichoandika hapa


Kuna familia zimesomesha mtoto kwa shida , basi ukipata nafuu ya maisha saidia

Familia zetu sio za kizungu
 
Sio sahihi ulichoandika hapa


Kuna familia zimesomesha mtoto kwa shida , basi ukipata nafuu ya maisha saidia

Familia zetu sio za kizungu
Mleta uzi ni mtoto bado hajui maisha

Kuna watu wamejinyima ili usome wengine wameuza mashamba, wengine wameshindwa hata kununua nguo au vitu vizuri ili wewe usome
What if mzazi wako asifikishe miaka 60 akafia hapo na miaka 55 au 56 jambo ambalo liko ndani ya uwezo wako lifanye usisubjrie mpaka ufikie miaka flani sababu hakuna ajuaye kesho

Leo hii wanahitaji msaada wako unawaambia mpaka wafikishe miaka 60 aiseee ni kauli iliyojaa roho mbaya
 
Mimi kwakweli nashukuru wazazi wetu wanajiweza siyo tegemezi, maana wameshajiandalia vitega uchumi vya kutosha, viwasaidie pindi watakapokuwa hawana uwezo tena wa kutafuta pesa
 
Uko sahihi kbsa
 
[emoji16][emoji16][emoji16]
 

Mkuu mimi nimesema tuu kwa sababu yanayotokea kwenye jamii ninayaona.
Achana na hawa wanaojifanya humu wanamoyo wa kusaidia wazee wao. Ilhali huku mtaani mambo ni tofauti Kabisa.

Wazazi wanaopeta huku mtaani ni wale wanaopokea pensheni zao au wale wenye miradi kama nyumba na uwekezaji mwingine.
Lakini wengi wa wazee kwenye hii nchi wanataabika sana.

Na sababu kubwa ni kujidanganya na ubinafsi. Zingatia uongo ni sehemu ya ubinafsi.

Wapo wazee wanateseka hii dunia hujapata kuona. Na sio kwamba hawakutunza watoto wao vizuri noop!

Ninapoandika hapa kwa vijana werevu wanatakiwa wachukue kama tahadhari vinginevyo watakumbuka maneno yangu
 
Sio sahihi ulichoandika hapa


Kuna familia zimesomesha mtoto kwa shida , basi ukipata nafuu ya maisha saidia

Familia zetu sio za kizungu

Na kuelewa.
Ila na wewe jaribu kuelewa nilichoandika.

Tatizo mnafikiri Taikon anaandika kama mwendawazimu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kumbuka kuwa mzazi ndio kakutengenezea njia ya hicho ulichonacho au hivyo ulivyo. mzazi anayejiweza hawezi kuwategemea watoto wake, wakati mwingine watoto hutoa Kwa upendo tu. Hebu FIKIRIA wazazi wako walivyokuwa wanahangaika wakati una umwa ,kupelekwa shule na mavazi. Kijana Leo unaleta dharau Kwa wazazi wako unajiona umejipataaaa
 
Bora nimejua mapema

Watoto wakifika miaka 27 tu nawaondoa Kwa lazima nyumbani waniache na Mama yao tufurahie maisha yetu ya Uzee 🤗
 
Nakubaliana na andiko hili
 
Bora nimejua mapema

Watoto wakifika miaka 27 tu nawaondoa Kwa lazima nyumbani waniache na Mama yao tufurahie maisha yetu ya Uzee 🤗

Kwanza mtoto akiwa umri wa kujitegemea alafu ukawa unamfuga hapo nyumbani ni unatengeneza mazingira ya kumfanya awaze urithi wake kwako.
Pili unamtengenezea mazingira ya kubweteka na kujinyima haki ya kujipigania na kujifunza kujitegemea.

Wazee wengi walioouwa na watoto wao walikuwa wakiishi na watoto wao.
 
Kuna reply nimemjibu kama hivi hajaijibu
🤣🤣🤣 Atarudije akiwaza Malaya na masela uchwara wanavyokula pesa zake akiwa baa huku akijua kabisa aliye hustle kumsomesha hata mia hajamtumia mwaka mzima
 

Mkuu mtu kutoa kwa upendo sijakataa. Nazungumzia wazazi wanaowashinikiza watoto wao wawatunze ilhali watoto wenyewe ndio kwanza filamu inaanza, hawajajipata.
Alafu Wazazi wenyewe umri bado ni wa kutafuta yaani wapo miaka 45-59.

Fikiria binti wa kazi analipwa elfu 50 anamiaka labda 19 mama yake anamiaka 42 lakini bado huyo mama anamshinikiza mtoto wake ahudumiwe familia.
Hivi huoni hapo kuna dhulma?
 
Kumbe ni muhimu kuwatimua mapema nyumbani.

Kuna Daktari mmoja alikuwa anatufundisha somo la hesabu Chuo Kikuu alikuwa anatania kwamba;

Ili kuwafanya watoto akili zichaji na waondoke mapema nyumbani basi Jenga nyumba ya vyumba viwili.

Eti kimoja wewe na Mkeo na kingine wajaze watoto wako humo

Atakayejisikia aibu ataondoka kwenda kuanza maisha ya kujitegemea 😜

Ngoja Wazazi tuanze kitumia hii mbinu 😜
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…