Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mna roho mbaya wakuuNdo lugha zao,utasikia nimekumiss hatari [emoji16]
Nakubaliana na mdau aliyesema usimuonee hurum mwanamke.
Yani na nilimpa sababu ya msingi tu...nkamwambia nfanyie mchakato kodi inabidi nilipe lakini alinifungia vioo ma.ma.eMshipa wa huruma ukaamua kuukata kabisa.
Aaah kabisa bro , Usimuonee huruma kwa kutegemea kupata kitu fulani ukimpa mpe tu kama umesaidia stranger usiemjua lakini kama unatoa ukitegemea utaendelea kusimika nafasi yako kwenye moyo wake asee utapigwa nyundo ya kichwaKuna wahuni watakuja kucoment
"Usimuonee huruma mwanamke"
Nshamsaidia msister hivi total 250k shida kweli kweli kwamba atanrudishia
Hadi leo ni mwaka aliniblock na urafiki ulikufa
Hawa viumbe sinaga huruma nao tena
Hapo tamaa za maisha mazuri zimeuzidi uwezo wake. Na watu kama hao nikumuomba Mungu tu tusioe mwanamke au mwanamke asiolewe na watu wa aina hiyo. Ni watu hatari. Ukimjuq mtu km.huyo mapema hata kama umemuoa achana nae tu mapema mtasumbuanaUnapotaka kumsaidi mtu inahitaji wewe unakwenda kutoa msaada uwe makini. Ninaposema umakini namaanisha uwe na uhakika kweli ninaekwenda kumsaidi ni mhitaji na kweli ana shida.
Nitatoa story kwa ufupi kuhusu huyu Bi dada ambae ni rafiki yangu kipindi cha nyuma.
Tulifahamiana vipi..
Nilimfahamu siku nimekwenda eneo lake la kazi, nilikwenda kumuona rafiki yangu (msela) basi akawa kanitambulisha kwa huyo bi dada.
Ilipita week kadhaa kisha nami nilianza kufanya kazi nae ofisi moja, mimi huyo dada na rafk yangu wa kiume na wengineo.
Kiukweli dada huyo ni mcheshi kiasi chache na mkalimu, nilipenda uwepo wake yeye kuwa mmoja wa wafanyakazi wenzangu.
Ni mama wa mtoto mmoja na anaishi na Mume.
Alipenda sana utani wa inshu za mapenz, na rafiki yangu wa kiume alikua anapenda hizo mada basi siku tukiwa kazini wote stori zinakua nyingiii.
Kama unavyojua wanawake wapenda kupewa pewa vitu na wanaume, mimi nilimtongoza kimasihara (sikuwa nimempenda ila nilimtamani kwa kuwa ni Pisi kali) alipokataa ndio ikawa msaada kwangu, tukawa na Mipaka, hawezi kuchukua kitu changu bila kuomba na akaacha kuniomba omba hela na ofa za hapa na pale.
Alibaki kuwa rafik kwangu.
Ilipita miezi kadhaa tukaja kutawanyika wote watatu, mmoja akaenda Mwanza, mwingine Kigoma, mwingine Bukoba.
Huyo dada kwa sasa anatafuta Kazi mkoa aliopo ( anasaka connection) na anadai kaacha na mumewe, wamezinguana, japo mimi niliishi kumsihi kuwa Asimuache mumewe kwani wanafanana hasa kwenye madhaifu, wanaweza kuvumiliana asitegemee kupata Mwanaume mwingine wa kumfaa zaidi ya huyo aliye nae,
Nilimshauri kuwa changamoto zenu za kimaisha jitahidini kuzitatua kama Familia.
Katika story mbalimbali na matukio kadhaa Niligundua yafuatayo kuhusu huyu bi dada.
~ Ilikua, Mchungaji akija mwisho wa Mwezi pale kazini bi dada alihusika kwenye sifa(Nyimbo) na n.k
Japo nilikuja kutambua alikua mkristo jina tu, hamuabudu Mungu kwa roho na kweli.
~ Alikua akiniambia siku akipata ajira Serikali atamuacha mume wake, na niligundua ni kwa sababu anamdhalau mumewe kwamba kwenye utafutaji hayuko vizuri. (Hatoi pesa ya kutosha KWA ajili ya familia)
nilimwambia si wazo jema lakini hakunielewa.
~Aliniambia pia siku hizi hapendi kumpa unyumba mume wake, yaki ikifika usiku anatamani kulala tu na hana muda wa mapenz na mumewe, hufanya tu malachache pale inapobidi.
mapenzi yake yote aliyaelekeza kwa mtoto wake wa kiume.
Main Point.
Juzi alinitafuta na kuniambia Yupo kwenye interview ya Kazi.. shirika fulani na anasubiri majibu.
Alidai kunimiss sana hadi kutamka maneno makali ya ushawishi wa kingono kuonesha ananipenda ( Lakini niligundua hizi ni njia za wanawake kuwalainisha wanaume wafungue wallet).
Akanipa na taarifa kuwa kaisha achana na mumewe, tulipoendelea na Mazungumzo, aliniambia kwamba Nimkoposhe fedha sh. Laki 2.
Nilimjibu hiyo pesa sina kwa lugha nzuri tu, na nilimwambia nitakutumia hela hata elfu 50 tu ili uongezee na sihitaji unirudishie.
Akasema sawa.. then alinipa taarifa kuwa ana mgonjwa ambae ni mama yake (Kalazwa)
Nikamuuliza unakwenda lini sasa kumuona, akijibu kuwa inanibidi tu nimtumie hela, najua atanielewa kwa kuwa huku nilipo sijakamilisha kilicho nileta na nimeishiwa pesa.
(Alipo yeye na alipo mama yake nauli ni zaidi ya Laki moja na nusu)
Kiukweli Maisha ni Magumu hasa kwa sisi vijana tulioanza utafutaji katika sector binafsi.
Baada ya hayo mazungumzo nilijiuliza Mwaswali yafuatayo..
Kiukweli Moyo wangu umetokea kuchukizwa nae to the Maximum.
Nimeona hana akili.
Na pia kama hana hela ya kumtumia mama yake kwanini asiwaambie kwao ukweli hali halisi kuwa hana fedha na majukumu hayo angewaachia ndugu wa kiume na baba yake, kwani baba yake uwezo wa kifedha upo.
Binafsi nimegundua kuna watu wanajifanya niwahitaji lakini si kweli, bali wanaongozwa na tamaa za haraka za kufanikiwa na kutaka kuonekana wakifanya makubwa na ilihali hawana chochote.
Ni hayo tu 👏
Definitely....Kuna haja pia ya kuangalia mtu wa kumuomba msaada!
Mzee acha kabisaHahaha akala mitaa[emoji23]
Soma Uzi wa Robert ,,unasema usimuonee huruma mwanamke wa kustahiki huruma kidogo ni mama ako na Dada zakoNshamsaidia msister hivi total 250k shida kweli kweli kwamba atanrudishia
Hadi leo ni mwaka aliniblock na urafiki ulikufa
Hawa viumbe sinaga huruma nao tena
Ila Kwa dada zako huwezi Wala lazima upewe penziiiii .Soma Uzi wa Robert ,,unasema usimuonee huruma mwanamke wa kustahiki huruma kidogo ni mama ako na Dada zako
Jamaa lina shobo naye sana. Ona kumbe lilikataliwa. Now wanaligeuza chuma ulete. Kweli ushamba mzigoSi kwamba unahasira za kukataliwa mkuu..?[emoji23]
Stori ili ibalance muite na huyo dada aeleze tusije mnanga dada wa watu kumbe kunamazito ndani yake!