Husda: Dada( Graduate) huko Nigeria, alishwa sumu na rafikiye ( mfanyakazi mwenzake) Kwa sababu kapandishwa CHEO kazini.

Utajua Kwa kutazama chanzo na matokeo
Chanzo cha matokeo kitakusaidia vipi kujua huu ni uchawi au si uchawi?

Tupe mfano wa kuthibitisha huu ni uchawi, na si kitu kingine chochote ambacho hukielewi tu.
 
Hapana. Husda ni husda, roho mbaya ni roho mbaya.

Mtu anaweza kuwa na husda na roho mbaya bila ya kuamini uchawi.

Huja define uchawi ni nini bado.
Ukishakuwa tu na husda na roho mbaya automatically unakuwa mchawi
 
Issue ya vyeo au madaraka ni ya kibinadamu sio ya kitaaluma. Hata usome vipi huwezi ondoa tabia za kiasili za binadamu kama husda, chuki, roho mbaya, hasira n.k.

Kuna mamilioni ya watu ambao wamesoma hiyo Prussian education system lakini hawauani kwa sababu ya vyeo, huyo dada hii ni tabia yake tu
 
Ukishakuwa tu na husda na roho mbaya automatically unakuwa mchawi
Hapana.

Mtu anaweza kuwa na husda na roho mbaya halafu asiwe mchawi.

Uchawi ni kitu tofauti, uchawi upo kwenye kuroga mtu.

Unaweza kumchukia mtu bila ya kumroga, hapo hujafanya uchawi, una chuki naye tu.

Chuki si uchawi.

Mimi siamini uchawi. Lakini naweza kuwa na roho mbaya, naweza kuwa na husda.
 
Chanzo cha matokeo kitakusaidia vipi kujua huu ni uchawi au si uchawi?

Tupe mfano wa kuthibitisha huu ni uchawi, na si kitu kingine chochote ambacho hukielewi tu.
Kama matokeo hayaendani na chanzo cha kisayansi Basi tunasema huo ni uchawi.

Mfano ili upate maji unahitaji 2 Oxygen plus 3 hydrogen.

Kama utapata maji bila ya 2Oxygen plus 2Hydrogen then tunasema huo ni uchawi.

Umetumia sayansi isiyo julikana kufikia matokeo yanayo julikana
 
Utajuaje matokeo hayaendani na chanzo cha kisayansi wakati hiyo sayansi yenyewe huijui yote?

Ukimchukua babu aliyefariki Africa miaka 200 iliyopita umfufue leo, umuoneshe TV, umuoneshe ndege zinavyoruka, umuoneshe tunavyowasiliana kwenye internet, umuoneshe madawa yanavyoponesha, ataona huu ni uchawi tu.

Hata kama hayo yote ni sayansi tu, hakuna uchawi.

Sasa na wewe unajuaje huo unaofikiri ni uchawi ni uchawi kweli na si kitu kingine ambacho hukijui tu?
 

Atakuwa na haki ya kuamini kwamba ni uchawi Kwa sababu Kwa definition ya uchawi, internet miaka mia 2 iliyo pita Inge fall kwenye category ya uchawi, Kwa sababu still bado ingekuwa ni sayansi ( maarifa ya Siri/ yasiyo julikana na public)

Na huo ndio msingi wa uchawi wenyewe.

Msingi wa uchawi ni usiri mkubwa Sana ndio maana mchawi akitoa Siri anakuwa.

Kwa sababu akitoa Siri hizo kila mtu atajua maarifa Yao na kila mtu akijua maarifa Yao then uchawi unakuwa hauna mantiki Tena Kwa sababu inakuwa Sio Siri Tena.

Hata hiyo internet yenyewe ukisoma" The history of internet" utagundua kwamba ilikuwa inatumika kama silaha ya kijeshi na ni watu wachache walikuwa wanaweza kutumia internet na computer Kwa ujumla wake.

Serikali kuu ya dunia ili ruhusu matumizi ya internet Kwa umma baada ya wataalamu wa internet ku develop advanced IT technology ambayo isinge athiriwa na umma kuwa na basic knowledge ya computer na internet.


Hata kama hayo yote ni sayansi tu, hakuna uchawi.

Sasa na wewe unajuaje huo unaofikiri ni uchawi ni uchawi kweli na si kitu kingine ambacho hukijui tu?

Ndio maana inaitwa sayansi ya Siri yani uchawi . Kutokujua kwangu Mimi ndo kunafanya uitwe uchawi
 
Binadamu hajazaliwa kuwa na chuki anajifunza. Mfano Temeke mwaka 2013 kuna shule ya kilokole ilifungwa Kwa sababu walikuwa Wana wafundisha watoto chuki.

Mwalimu anawapa watoto chocolate anawaambia " Mnaiona hii ? Hii ya Yesi hii"


Baadae ana waonyesha vitu Vibaya Vibaya anawaambia " Mnaona hii? Ya mtume hii, ya mtume hii"

Shule bado inayo nafasi ya kumuondolea binadamu uwezo wa kuwa na husda
 
umechanganya mambo, elimu iwe ya ukoloni au ya wapi inahusiana vp na roho binafsi ya mtu. We una shid ana elimu
 
Unajuaje uchawi ni sayansi?
 
sumu siyo uchawi, hayo mambo yapo dunia nzima acheni kujitukana.
Hujaelewa somo.

Sijasema sumu ni uchawi.

Ninakueleza kwamba, mtu anayeamini uchawi uchawi hata kumuua mwenzake kwa sumu si tatizo. Licha ya kusoma mpaka Masters.

Yani epistemology yake haimzuii kuua kwa sumu.

Sijasema sumu ni uchawi.

Umeelewa?
 
Chuki, Roho mbaya na husda makazini ni JANGA katika jamii yetu watu weusi
 
Sema ukiacha unafiki sehemu za makazini watu wanachukiana Ile real ,hata yule aliyemzidi mwingine mshahara bado anamchukia ...Ni kweli watu hasa wasomi wanaenda sana kwa waganga sijui tatizo liko wapi?


Kiufupi kwa Sasa haya mambo ya kuonesha mafanikio Yako binafsi kwenye mitandaoni hata status za Whatsapp si njema ...Sisemi kwamba utarogwa maana sidhani kama uchawi una nguvu kiasi hicho ila Kuna Ile chuki mpaka mnakosa ushikiriano.


Hata kama umepata Mtoto basi mfiche ,chukua likizo Yako kimya kimya (maternity\paternity leave) ...Kuna watu hawapati watoto basi wanachukia wengine wakipata ...
 
Hao watoto hawakufundishwa, ila walichochewa tabia ambayo ipo tayari ndani mwao, ukifika nchi zilizoendelea ambazo zina mitaala unayoisifia utakuta tabia hizihizi za husda kama Bongo tu....kama una exposure kama mimi utanielewa vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…