Hussein Bashe amechoka Uwaziri na kuamua kumchafua Rais Samia kwa Watanzania?

Ndugu zangu Watanzania,

Nimesikitika sana, kusononeka sana,kushangazwa sana,kuumia sana ,kutoamini macho na masikio yangu kwa kile nilichokiona na kusikia maneno na kauli za waziri wa kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe. Maneno ya Mheshimiwa Waziri yakisema kuwa serikali haitapeleka huduma za Dawa,mbegu na hata wanunuzi katika jimbo la kisesa kwa makosa ya mbunge wao ambaye alisema kuwa serikali hupeleka vitu feki hadi wanunuzi wa bei ndogo.

Nimejiuliza hivi Mheshimiwa waziri anaweza vipi kutamka maneno ya namna hiyo hadharani? Ndio uongozi huo? Nani kampa jeuri hiyo? Nani kamuagiza kutamka maneno hayo? Nani kamfundisha kuwa ndio serikali inavyofanya mambo yake hivyo? Vipi siku mbunge akisimama Bungeni na kusema kuwa serikali imepeleka Dawa za binadamu feki na wahudumu wasio na sifa jimboni kwake? Je, atatoa amri kuwa jimbo hilo lisipewe hata kidonge kimoja na kuwataka wahudumu waache kutoa huduma? Je Wagonjwa wangapi watakufa kwa kukosa dawa? Wagonjwa wangapi watafia wodini na milangoni kwa kushindwa kupokelewa na kupewa huduma? Kosa litakuwa la nani?

Vipi siku mbunge akisimama bungeni akasema kuwa jimboni kwake walimu hawafundishi vizuri na wanashinda wanaendesha bodaboda na wakike wanashinda wanauza vitambaa mitaani? Je waziri atafunga shule na kuondoa walimu wote jimbo hilo? Vipi mwingine mbunge akitokea akasema polisi wa jimboni kwake wanaonea Wananchi? Je waziri atafunga vituo vyote vya polisi na kuondoa askari wote katika jimbo hilo?

Hivi hiyo itakuwa ni serikali ya aina gani? Nani ataielewa? Nani ataiunga mkono? Nani atafurahishwa na maamuzi hayo? Nani ataelewa umakini wa serikali hiyo? Hivi maamuzi kama hayo ya Mheshimiwa Hussein Bashe ndio uongozi huo? Kwanini hajakwenda kufanyia kazi na kufanya uchunguzi wa tuhuma na malalamiko ya Mbunge na kisha kuja kupinga hadharani na kuwatoa hofu wananchi wake?

Je mbunge wa kisesa alichaguliwa na wananchi wote? Vipi wale ambao hawakumchagua na hawamuungi mkono na wala hawakubaliani na kauli zake? Wao unawasaidiaje? Je huduma kwa wananchi walipa kodi ni wajibu wa serikali au hisani? Ni takwa la kisheria au ni maamuzi ya waziri na hisia zake na maelewano yake na mbunge wa jimbo husika?

Halafu inakuwaje Mheshimiwa waziri aseme kwa kiburi kabisa kuwa AMEAMUA na kama mbaya na iwe mbaya.je yeye ni Rais? Amepoka madaraka ya Rais? Anapata wapi kiburi na majivuno ya kutamka kauli hiyo ambayo haiwezi kutamkwa hata na makamu wa Rais wala waziri Mkuu wala naibu waziri Mkuu? Kwa hiyo anaposema yeye ameamua anamaanisha kuwa yeye ndio alfu na omega na mwenye kauli ya Mwisho?yeye ndio Mkuu wa Nchi? Ndio Amiri Jeshi Mkuu wetu?

Kwanini anamshusha na kumvunjia heshima Mheshimiwa Rais na kuonekana kana kwamba siyo kitu? Kwanini anamchafua na kumdharau Mheshimiwa Rais na kuonekana kama hana uwezo wala nguvu ya kumfanya chochote kile na kwamba pasipo yeye haiwezekani mambo yakaenda? Hivi Mheshimiwa amejikwaa ulimi au ameteleza? Alidhamiria kusema hivyo au ni kujisahau?

Kwanini kiongozi ngazi ya Uwaziri ujidhalilishe na kuidhalilisha serikali na mamlaka ya uteuzi kiasi hicho? Nini kipo nyuma ya pazia ya kauli ya Mheshimiwa Waziri? Kwanini waziri ushindwe kudhibiti hisia zako? Kwanini ushindwe kuchunga ulimi wako? Kwanini ushindwe kutumia Busara,hekima na kuwa mtulivu uzungumzapo? Je hiyo ni kauli ya serikali nzima?

Halafu inakuwaje Mh Waziri aseme kuwa atakwenda kuwauliza wananchi wa kisesa kama wanamtuma mbunge wao kuzungumza azungumzayo? Je kwanini asingekwendwa kuzungumza kwanza na wananchi kabla ya kutoa maneno na kauli yake ambayo haikubaliki bila kujali itikadi za kisiasa? Na vipi kama wangesema kuwa wanaunga mkono kauli za mbunge wao? Je waziri angewanyima huduma au angepaswa kufanya uchunguzi wa madai na malalamiko ya Wananchi?

Napingana katika mambo mengi na Mheshimiwa Luhaga Mpina. Lakini pia nilikuwa namuunga mkono Mheshimiwa waziri katika mambo mengi Tangia akiwa mbunge mpaka waziri na hata hapa nimewahi kuandika kumpongeza ,lakini katika hili sikubaliani naye hata kidogo.

Mwisho mbona wabunge wa upinzani walikuwa kwa miaka yote wanapinga kila bajeti ya serikali inayopelekwa bungeni na ya kila wizara na bado wakawa wanapelekewa miradi mbalimbali ya maendeleo majimboni kwao na kupewa pesa za mfuko wa jimbo?

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Mkuu mara ya mwisho Tanzania kufanya uchaguz ilikuwa 2015 hzo nyngne ilikuwa kuwaachia wagonjwa wa akili kama knabashe kunda bungen kusubria maposho na upgaji mda ukfka 2025 watahara kwa mdomo hii nchi syo yakupelekwa kama gar bovu
 
Ndugu zangu Watanzania,
Nimejiuliza hivi Mheshimiwa waziri anaweza vipi kutamka maneno ya namna hiyo hadharani? Ndio uongozi huo? Nani kampa jeuri hiyo? Nani kamuagiza kutamka maneno hayo? Nani kamfundisha kuwa ndio serikali inavyofanya mambo yake hivyo?.
Ukiondoa uchawa na kujikombakomba kuliko pitiliza kwa Rais Samia hadi kuonekana kama taahira fulani, ukweli unabaki you one of the few wenye good brain!.
Hili ndio bandiko lako la kwanza la kizalendo lenye objectivity ya kutanguliza mbele maslahi ya taifa, na sio bandiko la kichawa!.
Hongera sana for this!.
Naomba nikufinye sikio, kama unataka bright future CCM, kuwa mnafiki!, ukiwa mkweli wa kiwango hiki, make sure you are independent.
2. Stay away from powerful people!, Husein Bashe is very powerful, good brain, high IQ, very bright and brilliant, he is no nonsense man!
P
 
Kwa sasa Afrika ingekuwa ni Nchi moja, basi mtu pekee Mwenye uwezo wa kuifanya Afrika ikawa kama ulaya na kuwafanya wazungu kuja kuomba kazi na kutafuta maisha barani Afrika angekuwa ni Mmoja tu Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka ,jasiri muongoza njia na nuru ya wanyonge.kwa hakika maendeleo ya Bara la Afrika yangepaa kwa kasi kama ndege vita .kama ilivyo kwa sasa hapa nchni ambapo tunashuhudia miradi mbalimbali ya maendeleo ikijengwa kila sehemu.
Sio bure wewe unavutaga bange za chooni.
 
Mwandishi umeegamia upande mmoja haukumskiliza Mh. Bashe alivosema hadi mwisho, alisema hivi "ataenda kuonana na wananchi wa kisesa na kuwauliza kama zile tuhuma anazozitoa mbunge wao ni tuhuma ambazo na wao wanaziamini zipo basi serikali haitapeleka kweli hizo dawa lakini kama sio maoni yao bali ni ya mbunge binafsi basi serikali itapeleka huduma kama kawaida bila kujali maneno ya mh. Mpina"
 
Back
Top Bottom