Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Ngoma ikisifiwa mlio ujue iko karibu kupasuka. Kelele na majigambo ya BRN yalipelekea MH Rais kuja na msemo "Ukitaka kazi ngumu iwe nyepesi mpe Msomali".
Ghafla Jana Bashe alitoa kauli tata ya kwamba "serikali" haitapeleka mbolea, mbegu wala wanunuzi kwenye Jimbo la Kisesa ili Mbunge wa Jimbo hilo anayetuhumu kwamba mbolea na mbegu za Pamba zilizopelekwa mwaka jana huko Kisesa zilikuwa feki na wanunuzi walikwenda kununua pamba toka kwa wakulima walitoa bei ya chini isiyorejesha gharama za wakulima na kuwapa faida.
Bashe anaposema Serikali haitapeleka inaonyesha kauli yake inatoka Baraza la Mawaziri.
Na kama ni kauli binafsi tunatarajia Mh. Rais afanye kama aliyofanya Kwa Waziri wa Kura feki.
Mbegu na mbolea za ruzuku zinanunuliwa kwa fedha za walipa kodi wakiwemo wa Kisesa.
Hivyo kuchukua kodi na huku hupeleki huduma Kwa kisingizio cha Mbunge wao kukutuhumu ni udikiteta
Badala ya kufanya uchunguzi ili kuona kama maneno ya Mpina yana ukweli yafanyiwe kazi au kama ni ya uongo achukuliwe hatua, Waziri anakuja na approach ya ukewenza kwenye fedha za Umma?
Soma pia: Waziri Bashe kujiuzulu muda wowote kumfuata Kinana