Hussein Bashe: Hatutapeleka mbolea, mbegu wala wanunuzi wa Pamba Kisesa

Kauli kutoka kwa Kiongozi mwenye upeo mdogo!
Wewe Bashe umejiridhisha kwa utafiti upi kuwa madai ya Mpina hayakuwa kweli!
Unaposema Sisi Serikali,je uamuzi wa kutopeleka Mbegu na Wanunuzi ni uamuzi wako binafsi au ni maamuzi ya Baraza la Mawaziri!?
Acha kulewa madaraka, fuata Sheria ktk utendaji wako!
 
Hayo ni maneno ya Samia Suluhu kupitia waziri wake.
 
Mabillion ya sukari yamemlevya huyu Bashe
 
Mpina mpuuzi mmoja. Anailetea hasira serikali nzima hajui ni kwa maumivu ya wakulima wake mwenyewe.

Kawa mjinga sana huyo mwananzengo analaumu bila ya kuwa hata na chembe ya ukweli wa hicho anachokilaumu.
 
hata kama kuna kauli zimetolewa kukosoa serikali lakini kudhani kuwanyima huduma wananchi ili kumkomoa mpina ni ujinga uliopitiliza na kwa hili si tu alipasa aombe radhi wana kisesa bali watanzania kwa ujumla wake.
Mpina mbunge wao pia asimame na kuomba radhi kwa hizo tuhuma zake kwa serikali kuu, Huwa serikali zinaongozwa na binadamu sio malaika.

Unapoibuka na kujua kulaumu kwa kila jambo angalau uwe na suluhisho la hicho usichokiunga mkono.
 
Kwanini hizo mbolea ziwe hazifai kwenye jimbo lako pekee na kwa wengine zitumike bila ya shida yoyote ile?.

Mpina ni mjinga tu, ana hasira za kwanini Rais Samia anaongoza nchi muda huu anasahau kuwa Mpango wa Mungu huwa haupingwi kwa nguvu za kibinadamu.
 
Bashe alipokuwa back bencha alikuwa na akili sana ila sasa nimeprove km serikali ya Tz INADUMAZA UWEZO na AKILI za watumishi!!!
 
Ameshindwa kushughulica na Mpina sasa anashugulika na watanzania.
 
Kwamba majimbo yote yana mazao sawa, mahitaji sawa na uhitaji wa virutubisho na mbolea sawa ? Au kama majimbo mengine wanakubaliana na substandard na wewe ukubaliane nayo ?

Yeye ameongea kama mwakilishi wa jimbo lake na sio mwakilishi wa majimbo ya Tanzania, hivyo huenda yeye anaona it can be better..., kwahio kama option ni kuacha kupeleka basi waache ila wasichukue Kodi wala kulazimisha watu sehemu ya kuuza...;
 
Huyo Mpina ajifunze kuongea vitu katika mtazamo ulio chanya sio kila kitu kwake ni kibaya tu, anakuwa kama kachanganyikiwa hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…