Hussein Bashe ni janga kubwa kwa taifa letu. Hatufai leo, hatufai kesho na hatufai kesho kutwa!

hakuna asiyefanya kazi na hakuna anaetegemea chakula cha kupewa! tofautisheni kwamba kilicho waathiri wakulima sio uvivu ni ukame! msilete ukuda kwenye mambo ya maana
 
Kwa hiyo wewe mwenye akili unamlaumu Bashe kwa ukame au sijakuelewa? Nilidhani unajiongelea wewe lakini naona unaongelea wakulima. Nimekwambia masoko yamejaa vyakula kama suala la bei juu basi ongezeni uzalishaji mbona simple tu au mpaka mletewe wataalam? sasa wewe weka makosa ya Bashe tukujibu kwa hoja. Bashe ni mtu smart na miaka inayokuja anayofanya leo watakuja kumshukuru. Ukulima isiwe wito kama mlivyoangamiza elimu na walimu wito. mkulima ni mfanya biashara ataamua amuuzie nani kwa bei gani ni mali yake.
 
ufaransa mkate ulipanda bei watu wakaingia kuandamana nyinyi mnalelewa na wazazi wenu bado hata bei chakura hamuijui
 
Tatizo la Bashe ni Samia!
Bashe hana uwezo wa kufunga mipaka ya nchi hii wala kuifungua.
Mwenye mamlaka ya kufunga mazao yasiuzwe nje ya nchi ni #Samia kama Rais wa JMT.
Na soo #Bashe kama waziri wa wakulima!

Mnataka Bashe aseme Ukweli halafu muanze kumtumia wahuni wenu wa Uvi-waviCCM?

Bashe anasoma alama za Nyakati,ndio maana jana alikataa kutumika na Samia!
 
Najua kabisa Bashe ni team lowassa na yupo karibu na Rostam, Hilo sio tatizo kwa sababu kama mtu ni kiazi kichwani ni kiazi tu, Bashe ameonyesha uwezo wa kiutendaji na kufuatilia sana hujuma za knye sector ya kilimo, Samia mwenyewe nadhani kwa mara ya kwanza baada ya baba wa taifa ndo kaonyesha utashi wa kisiasa wa kufanya mageuzi ya kilimo kweli mfano.

1. Kutenga billioni 900 knye kilimo mara nne ya bajeti tulizozoea
2.Kuanzisha na kufufua irrigations schemes Nchi nzima , huu utakuwa mwarobaini wa kudumu wa issue za ukame na hasara za hovyo hovyo knye kilimo.
3. Kuanzisha block farming itawasaidia sana vijana na wenye mitaji midogo ku organize resources and extensions services

4. Kugawa mashine za kupima udongo ni bonge ya step , zamani mpaka utume sample SUA usubiri miezi miwili majibu na gharama zaidi ya laki 2 kwa sisi tuliokuwa tuna mashamba Morogoro. Je wa mbinga au katavi angesaidikaje?
5. Kubwa kuliko lote ni kuachia soko huria, Rais angekuwa hana nia angeshazuia kupeleka mazao nje, ile ilikuwa ni kuwanyonya mno wakulima , badala ya kuacha soko liamue bei unalazimisha kupunguza demand ili bei iwe chini , ILIKUWA NI SERA YA HOVYO SANA. BORA KITOKE CHOTE mwaka kesho wote tutachangamkia fursa ya kufanya kilimo na wakulima watatajirika , Mbona hatupangi bei za bidhaa za viwandani? au bei za vyumba vya kulala wageni? Soko linaamua bei . Tuwaaachie wakulima soko liamue
 
ufaransa mkate ulipanda bei watu wakaingia kuandamana nyinyi mnalelewa na wazazi wenu bado hata bei chakura hamuijui
mimi ni mkulima mzoefu na mkubwa kiasi ekari zaidi ya 800 naongea kwa uzoefu na wa kutoa ajira zaidi ya 40 , najua uchungu wa kukopa bank kulimia , unavuna vizuri ,halafu serikali inafunga mipaka hapo una deni la M 400 la bank
 
ufaransa mkate ulipanda bei watu wakaingia kuandamana nyinyi mnalelewa na wazazi wenu bado hata bei chakura hamuijui
Fanya kazi tu kuna watu wengi hata bajeti ya chakula haifikirii kabisa, wanawaza budget inayoumiza ni kusomesha watoto private universities Canada au Europe ndo kidogo inaumiza kama wapo zaidi ya watatu wanne
 
Nadhani mama karuhusu ndo maana hawagongani maneno
 
Usalama upo sana tu. Ndio maana kuna ghala la taifa. Chakula hakijawa haba, wengi wenu mnacholalamikia ni bei. Ni kweli sote inatuathiri, lakini acha tu iwe hivyo ili kilimo kimlipe vilivyo mkulima.
 
Usalama wa chakula hauletwi kwa kufunga mipaka, huko ni kuleta njaa. Anachofanya Bashe ndicho kitahakikisha usalama wa chakula nchini.
 
Tafuta hela acha kulia lia......
 
Hii vita kali sana...πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Si jana tu kuna mdau kamfungulia uzi kumfagilia....???
 
Bajeti ni bil 750 sio bil 900
 
Zoezi hili likiwa endelvu, kufika 2025 uchumi wa mkulima, nchi na usalama wa chakula vitakuwa vimebadilika kabisa. Kwa hili Bashe anastahili pongezi sana.
 
majungu hayajengi, wabongo punguzeni majungu na fitina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…