Najua kabisa Bashe ni team lowassa na yupo karibu na Rostam, Hilo sio tatizo kwa sababu kama mtu ni kiazi kichwani ni kiazi tu, Bashe ameonyesha uwezo wa kiutendaji na kufuatilia sana hujuma za knye sector ya kilimo, Samia mwenyewe nadhani kwa mara ya kwanza baada ya baba wa taifa ndo kaonyesha utashi wa kisiasa wa kufanya mageuzi ya kilimo kweli mfano.
1. Kutenga billioni 900 knye kilimo mara nne ya bajeti tulizozoea
2.Kuanzisha na kufufua irrigations schemes Nchi nzima , huu utakuwa mwarobaini wa kudumu wa issue za ukame na hasara za hovyo hovyo knye kilimo.
3. Kuanzisha block farming itawasaidia sana vijana na wenye mitaji midogo ku organize resources and extensions services
4. Kugawa mashine za kupima udongo ni bonge ya step , zamani mpaka utume sample SUA usubiri miezi miwili majibu na gharama zaidi ya laki 2 kwa sisi tuliokuwa tuna mashamba Morogoro. Je wa mbinga au katavi angesaidikaje?
5. Kubwa kuliko lote ni kuachia soko huria, Rais angekuwa hana nia angeshazuia kupeleka mazao nje, ile ilikuwa ni kuwanyonya mno wakulima , badala ya kuacha soko liamue bei unalazimisha kupunguza demand ili bei iwe chini , ILIKUWA NI SERA YA HOVYO SANA. BORA KITOKE CHOTE mwaka kesho wote tutachangamkia fursa ya kufanya kilimo na wakulima watatajirika , Mbona hatupangi bei za bidhaa za viwandani? au bei za vyumba vya kulala wageni? Soko linaamua bei . Tuwaaachie wakulima soko liamue