Mimi sio mpenzi sana wa siasa za watu ila napenda kukiri kuwa so far, kati ya watu ninaowaona wana akili na wanaweza kushika vizuri kijiti kutoka kwa Mama Samia coming 2030 ni Ndug. Hussein Bashe. Ana vision zisizotofautiana sana na Mama Samia hasa kwenye uwezeshaji, uwekezaji na biashara ivo si vibaya Chama changu kikaanza kumuandaa sasa kama alivyoandaliwa Ben Mkapa na Jakaya Kikwete.
Ninamuona Kama mtu smart, mwenye mawazo chanya yenye kujenga biashara na uwezo wa Taifa katika kukamata fursa za dunia hasa kiuwekezaji na kibiashara ambapo huu ndo Mwenendo wa Dunia yetu kwa sasa!
Nirudi kwenye mada, Leo BBC wametoa habari juu ya kilimo cha Cacao Kyela. Nilifika Kyela mwaka jana 2021 nikitokea Mbaba Bay na kusema kweli kuna potential kubwa sana kwenye zao la Cacao ambayo Tanzania Bado hatuja iutilize vizuri. Wakulima hawajahamasishwa kulima zao hili kwa wingi na pia elimu sahihi bado haijatolewa katika kuhakikisha zao hili linalimwa kwa wingi, kwa ubora na kumnufaisha Mtanzania.
Maeneo ya kwetu Nyasa, Ludewa na Kyela yanaonekana yanafaa sana kwa kilimo cha Cacao na yakitumika vizuri kwa wakulima kuhamasishwa kulima kwenye mashamba makubwa kwa ubora ni hakika hata Tanzania tunaweza kuwa na Brand yetu ya chocolate kama nchi zingine.
Naomba kama Serikali inavyoweka mkazo katika kilimo cha chikichi ambacho ingawa kitaliondolea Taifa letu na uhaba wa mafuta na kama Serikali ilivyoanza kuweka nguvu kwenye kuhamasisha watu kulima korosho kufikia kutoa hadi Miti kwa wakulima basi serikali ihakikishe pia unaweka nguvu kwenye zao hili la Cacao. Najua unaweza sana basi fanya hili.
Naamini uwezo unao na utafanyia kazi ushauri wangu.