Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi, ilikuwaje ukawa Mbunge wa Mkuranga, mkoa wa Pwani, na sasa unaenda kugombea urais Zanzibar?

Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi, ilikuwaje ukawa Mbunge wa Mkuranga, mkoa wa Pwani, na sasa unaenda kugombea urais Zanzibar?

Ngoja nikuambie kitu mkuu.

Hivi unajua kuna wazanzibari waliozaliwa bara? Na unakubaliana na mimi kwamba kuna wasukuma waliozaliwa zanzibar? Na unajua kwamba kuna wamakonde waliozaliwa Musoma? Hao je tunawaitaje? Kuzaliwa kwao Musoma au Kagera kunawatoa umakonde wao?

Kama jibu ni sio hiyo ndiyo case ya Hussein Mwinyi pia. Hivi unajua kwamba hata baba yake aliwahi kuwa mbunge wa Mkuranga ? Mkuranga inaweza kuwa sehemu yake tu aliyoianzia siasa lakini kama asili yake ni Zanzibar basi alirudi nyumbani
 
Mbona ni kinyume chake? Kamuulize Bakhresa
Bakhresa ni muwekezaji kama ilikuwa hujui. Na kama unasemea uleradi wa Fumba town si wake. Tofauti na hoteli na visima vya mafuta ni nini kingine anamiliki?
 
Mapinduzi Mapinduzi Daima.

IMG-20200817-WA0044.jpg
 
Hata mimi nilijiuliza sana swali hili, ila sikuelewa inakuawje mtu alipewa kugombea ubunge Pwani yeye akiwa ni mzanzibari alipita au alikabidhiwa tu ubunge.

Hussein hajawahi kuwatumikia Wazanzibari kwa Uwakilishi au ujumbe wowote ule leoanakuja awe Rais wa Zanzibari ni wangapi watamuelewa au inatumika cheo cha baba yake kuwaelimisha wazanzibari na kuawlazimisha wamkubali.

Uzoefu wa kufanya kazi zanzibari kama mkazi hana, uwezo wa kuwasaidia wazanzibari kutokana na ukaribu wao na yeye hana, hapa pagumu sana, huyu ni mtu wa bara
 
Huyu dawa yake na Zanzibar kungekua kuna wajumbe nao ambao wanawapigia kura wagombea watatu wa mwanzo. Na hao wajumbe wawe kutoka Zanzibar hasa.

Asingekatiza round huyu. Sema ndio hivyo wajumbe wa Zanzibar hawana vikao hivyo kule
 
CCM haijawahi kushinda zanzibar bali ni kuchakachua tu na 2015 mlishindwa vibaya sana na Maalim seif akatangaza matokeo mmeshindwa japo na pia mlichakachua kura.
Hakuna mgombea yeyote anaeshindwa asiseme ameibiwa kura. Na mwaka huu hali ni mbaya maana na yule baba wa demokrasis U.S.A anashutumiwa kuiba kura.
 
Hata mimi nilijiuliza sana swali hili, ila sikuelewa inakuawje mtu alipewa kugombea ubunge Pwani yeye akiwa ni mzanzibari alipita au alikabidhiwa tu ubunge, Hussein hajawahi kuwatumikia Wazanzibari kwa Uwakilishi au ujumbe wowote ule leoanakuja awe Rais wa Zanzibari ni wangapi watamuelewa au inatumika cheo cha baba yake kuwaelimisha wazanzibari na kuawlazimisha wamkubali, uzoefu wa kufanya kazi zanzibari kama mkazi hana, uwezo wa kuwasaidia wazanzibari kutokana na ukaribu wao na yeye hana, hapa pagumu sana, huyu ni mtu wa bara

Nitajie Waziri wa Ulinzi wa Zanzibar?
 
Hili suala linachanganya, na ninahofia wahafidhina wa Kizanzibari watalitumia kutusumbua kwenye kampeni...

Si ajabu kuwa mbungewa mkuranga mkoa wa pwani kwani wazazi wake walitokea Pwani na si wazaliwa wa zanzibar
 
Hili suala linachanganya, na ninahofia wahafidhina wa Kizanzibari watalitumia kutusumbua kwenye kampeni.

Je, Hussein Mwinyi ni Mtanganyika au ni Mzanzibari? Ilikuwaje akagombea Mkuranga, mkoa wa Pwani?...
Ni sawa James Joseph David kusoma form 1 mpka six katika Islamic secondary school ...jambo la kawaida
 
Zanzibar wasipotumia fursa ya Lissu na Seif katika uchaguzi huu CCM wakimtaka wanaweza kumpachika Uzanzibari hata Serukamba na kuwa Rais wa Zanzibar na Waunguja wasifanye kitu.
Hio fursa itumike mara ngapi?

Kuna uchaguzi ambao CCM Zanzibar ilishinda kihalali?

CCM bara inailinda CCM Zanzibar, wameonekana CCM Zanzibar wapumbavu wakatafutiwa mbara awaongoze 😀
 
Unashindwaje kujua vitu vidogo hivi. Kuwa mbunge ktk jimbo lolote Tanzania bara lazima uwe na sifa moja muhimu miongoni mwa sifa zilizoanishwa ktk sheria na kanuni za uchaguzi; sifa yenyewe ni lazima uwe mtanzania. Sasa kila Mzanzibari ni Mtanzania, hivyo, mzanzibari anaweza kugombea popote nchini ili mradi amekidhi vigezo vingine.
Hili suala linachanganya, na ninahofia wahafidhina wa Kizanzibari watalitumia kutusumbua kwenye kampeni.

Je, Hussein Mwinyi ni Mtanganyika au ni Mzanzibari? Ilikuwaje akagombea Mkuranga, mkoa wa Pwani?

Hii siielewi, anayeelewa anifahamishe
 
Mwinyi ni Mzanzibar kwa asili yake. Amekuwa mkaazi wa mkuranga hivyo alikuwa na sifa za kugombea huko. Sifa kuu ya kugombea zanzibar ni uwe mzaliwa kwa asili au uwe umekaa (kuishi zanzibar miaka 5 mfululizo). Kwa sifa hizo ndio akaenda Zanzibar kugombea ubunge. Hadi anapendekezwa alikuwa mbunge kutoka Zanzibar.
Una uhakika unachokiongea
 
Mzanzibari yoyote anaruhusiwa kugombea chochote huku bara kwa maana ya muungano ila mbara wa huku hana ruhusa ya kugomnea chochote cha upande wa zanzibar.
 
Back
Top Bottom