Huu hapa mchongo wa kufanya kwa kijana apate hela ya kula

aise

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2018
Posts
5,175
Reaction score
16,488
Huu mchongo ni kwayule kijana ambaye amepinda na maisha ya mtaani.

Kuna michongo mingi ya kufanya ili "kusogeza siku" huku ukisubiri inshu ya maana.

Huu ni mmoja wapo.

KUGONGA KOKOTO.

KUGONGA KOKOTO ndoo moja ni 200, kwahiyo ukikomaa kwa siku wastani unaweza kugonga ndoo 30.

200 × 30 = 6000 ambayo ni hela inatosha kwa matumizi kidogo ya kusogeza siku kwa kijana aliyepinda.

Fanya hii kazi huku ukisubiri michongo ya maana.
 
Ndoo 30 za kokoto unapata kwa muda gani?
 
Kwenye 6000/= toa 3000/= ya kununua Malaya ....

Ndiyo maana nimesema ni hela ya "kusogeza siku" na matumizi madogo madogo.
Ukinunua malaya kwa 3,000 hayo ni matumizi yako.
Hakuna hela ya kujenga kwa kazi hii, ni hela tu ya kuzugia.
 
Ndoo 30 sio mchezo ni nyingi sana
 
Hili wazo lako sijui umefikiria nini

Anyway kila mtu ana haki ya kuzungumza lakini kwa ndoo 30 x200 sio jambo rahisi,

Ushawahi kugonga kokoto?

Bora ungeshauri apite majumba kadhaa kuomba hata order za manunuzi ya mboga mboga na viungo vyake,apate asilimia chache katika manunuzi pamoja na gharama ndogo ya kumfikishia nyumbani kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…